Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara Simba SC, leo Februari 26, 2019 wanashuka dimbani wakiwa ni wageni kumenyana na Lipuli FC katika mchezo wa marudiano wa raundi ya pili msimu huu 2018/2019
Mchezo huo unapigwa katika Uwanja wa Samora mkoani Iringa majira ya saa kumi za jioni
======
Kikosi cha Simba kitakachoanza dhidi ya Lipuli FC: Aishi Manula, Zana Coulibaly, Mohamed Hussein, Yusuph Mlipili, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin,Clatous Chama, John Bocco, Meddie Kagere na Emmanuel Okwi
Benchi la Simba: Deo Munishi, Asante Kwasi, Hassan Dilunga, Said Ndemla, Haruna Niyonzima, Rashid Juma na Adam Salamba
Kikosi cha Lipuli kitakachoanza; Yusuph Mohamed, William Gallas, Paul Ngalema, Ally Sonso, Haruna Shamte, Fred Tangulu, Seif Karihe, Jimmy Shoji, Paul Nonga, Daruwesh Saliboko na Steve Mganga
Benchi la Lipuli; Abdallah Makangana, Novalty Lufunga, Shaban Adda, Issa Rashid, Ibrahim Job, Keneth Masumbuko na Mussa Nampaka
UPDATES:
FT: Lipuli FC 1 - 3 Simba SC
>>> Ni patashika katika dimba la Samora mjini Iringa, Simba wanaanza na bao likifungwa na Clatous Chama dakika ya 6.
>>> Lipuli FC wanasawazisha dakika ya 18 kupitia kwa Paul Nonga.
>>> Ni yule yule Mwamba wa Lusaka, Clatous Chama anaingia tena kimiani na kuipatia Simba goli la 2 mnamo dakika ya 44
View attachment 1032721
>>> Meddie Kagere anaifungia Simba bao la tatu dakika ya 58.
View attachment 1032731