Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) - Mkapa Stadium | Yanga SC v Simba SC

Yanga huwa hatuna maneno mengi, kazi kazi.
Tafadhalini sana Mikia hatutaki kuwatafuta baadae, tumechoka tabia yenu ya kukimbia kila muonapo mambo magumu kama inavyoenda kuwa hii leo.
.Unataka unidai nini
 
Hawa mwanitesa united (man u) mbona wanataka kunitisha, kwa rekodi zangu za haraka haraka simba na man u wakicheza kwa siku moja lazima mmoja apoteze pointi, kama sikosei ni mara moja simba alishinda na man u akashinda.
 
Hawa mwanitesa united (man u) mbona wanataka kunitisha, kwa rekodi zangu za haraka haraka simba na man u wakicheza kwa siku moja lazima mmoja apoteze pointi, kama sikosei ni mara moja simba alishinda na man u akashinda.
Ngapi ngapi huko?
 
Baadaye msimulaumu Manula
 
Wakati wowote mpira utaanza uwanja wa Mkapa

Naaaam mpira umeanza hapa uwanja wa Benjamin Mkapa, dakika 90 za jasho na damu

Yanga SC 0-0 Simba SC
 
Yanga leo anapigwa kuanzia tatu
Na Luis a.k.a konde boy lazma awe man of the match
 
05' kwenye Ligi Kuu Tanzania VPL hakuna bao kwa pande zote mbili

Mpira unachezwa sana katikati huku kila timu ikijaribu kupenya kufikia lango la timu pinzani

Yanga SC 0-0 Simba SC
 
10' Yanga wa tatu ambazo hazikuzaa mabao

Ni Free Kick kuelekea Yanga SC ngoja tuone. Inapigwaaaa inaokolewa.
 
Kama kawaida yangu nataka nibane pumbu Yanga wasipate goli.
mliopo uko uwanjani Yanga wapo upande upi kaskazi au kusi?
 
15, Yanga wanakosa nafasi ya wazi baada ya mpira wa krosi kuzagaaa na kuokolewa na Manula

Yanga SC 0-0 Simba SC
 
20' Free Kick kuelekea Simba SC

Inapigwaaaa, inaokolewa na mabeki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…