Mimi ni mwenzio ubingwa bado tunaweza kuupata kabisa ila kwa 'kujipanga' vizuri....Timu yetu kwa sasa ipo hapo ilipo kutokana na nguvu za mtu mmoja- Zahera- ambaye ana uwezo mkubwa wa saikolojia ya wachezaji...ila hasaidiwi...ameanza kuchafuliwa na baadhi ya viongozi wa Simba kwa kumtuhumu hili la lile kwamba alijaribukuisaidia Vita...yeye ni binadamu na anaweza kukata tamaa...hakuna tamko la maana lililotoka kwa wanayanga kushutumu kauli hizi za baadhi ya viongozi wa Simba...ninavyowafahamu Simba sasa hivi wanaandaa mkakati wa kumuondoa Zahera kwa kuwatumia baadhi ya viongozi wa serikali...Simba walianza kuibomoa Yanga kwa kumuondoa Kakolanya kwa mbinu chafu kwa kumtumia wakala wake ambaye ni kiongozi wa Simba...Yanga hawakulalamika officially...suala la Kakolanya lingeweza kumweka pabaya yule wakala...lakini viongozi wa Yanga kwa kuwa hawajui mbinu chafu zinazoelekezwa kwa Yanga wamekaa tu bila kufanya chochote...