Ligi ya Mabingwa Afrika | Uwanja wa Taifa, Dar: Simba SC 1-1 UD Songo. Simba yatolewa kwa faida ya goli la ugenini iliyopata UD Songo

Ligi ya Mabingwa Afrika | Uwanja wa Taifa, Dar: Simba SC 1-1 UD Songo. Simba yatolewa kwa faida ya goli la ugenini iliyopata UD Songo

Kiukweli hata roho haiumi! Tuna timu bora sana. Simba wasifanye mabadiliko yoyote msimu ujao tunakuwa mabingwa wa Africa!
Mnatimu bora,timu ipi baada ya kufanyika sub ya Dilunga,kule bench kulikuwa hamna mchezaji wa kubadilisha matokeo na wale Wabrazil ni mmepigwa ,wale ni kama wauza miogo wa Coco Beach ila wao Wanauzia Copa Cabana beach Brazil.
 
Kutolewa kwa Rollers na Orlando Pirates lipo la kujifunza.

Shabiki Nambamoja

Wakati Simba ikiwa imeweka kambi Afrika Kusini kujiandaa na msimu mpya, michezo yake mikubwa ya kirafiki ilikuwa dhidi ya Township Rollers na Orlando Pirates

Michezo yote walitoka sare ya bao 1-1

Ni kipindi hicho mashabiki wa Simba walikuwa wakiibeza Yanga iliyokuwa imeweka kambi mkoani Morogoro wakisema kuwa inacheza na vitimu vidogo, wao wanacheza na wakubwa wenzao

Kilichotokea sasa, Yanga iliyokuwa Morogoro, imeiondosha Rollers iliyoweka kambi Afrika Kusini mwezi mzima!

Orlando Pirates nayo imeondolewa na Green Buffalos ya Zambia kwa kuchapwa mabao 2-1

Hawa ndio wenzetu walisema ni timu kubwa walizopimana nazo huko Afrika Kusini

Kocha Mwinyi Zahera amedhihirisha kuwa mpira ni mbinu tu, mengine yote ni mbwembwe

Haijalishi umeweka kambi wapi, muhimu ni kuwa na mbinu stahili ili uweze kushinda mchezo

Pia michezo ya kirafiki wakati mwingine sio kipimo sana cha uimara wa timu

Kikubwa tuwaombee ndugu zetu wasivurugane na tumuombe Mzee Kilomoni atulie kwanza maana akileta maneno hasira zote zitahamia kwake.

kila mtu karudi nafasi yake Yanga wakimataifa , Simba wa mchangani.
Umenikumbusha tena Haji alikuwa anaweka picha za dhihaka kabisa eti Yanga ipo Morogoro. Simba team kubwa kuwa na msemaji kama yule ni upumbavu.
 
Hakuna cha mpira kudunda hapo. Wamepigwa tu hawajui mpira. Wanajua taarabu hao. Pamoja na kutolewa utamsikia taarabu zinazowadanganya za manara
Yaani kama zile dkk za mwanzo walipakatwa aisee na wangekuwa makini wale Du Songo wangepata bao mbili za haraka haraka.

Ila kwa hili wamejifunza.
 
Back
Top Bottom