Kutolewa kwa Rollers na Orlando Pirates lipo la kujifunza.
Shabiki Nambamoja
Wakati Simba ikiwa imeweka kambi Afrika Kusini kujiandaa na msimu mpya, michezo yake mikubwa ya kirafiki ilikuwa dhidi ya Township Rollers na Orlando Pirates
Michezo yote walitoka sare ya bao 1-1
Ni kipindi hicho mashabiki wa Simba walikuwa wakiibeza Yanga iliyokuwa imeweka kambi mkoani Morogoro wakisema kuwa inacheza na vitimu vidogo, wao wanacheza na wakubwa wenzao
Kilichotokea sasa, Yanga iliyokuwa Morogoro, imeiondosha Rollers iliyoweka kambi Afrika Kusini mwezi mzima!
Orlando Pirates nayo imeondolewa na Green Buffalos ya Zambia kwa kuchapwa mabao 2-1
Hawa ndio wenzetu walisema ni timu kubwa walizopimana nazo huko Afrika Kusini
Kocha Mwinyi Zahera amedhihirisha kuwa mpira ni mbinu tu, mengine yote ni mbwembwe
Haijalishi umeweka kambi wapi, muhimu ni kuwa na mbinu stahili ili uweze kushinda mchezo
Pia michezo ya kirafiki wakati mwingine sio kipimo sana cha uimara wa timu
Kikubwa tuwaombee ndugu zetu wasivurugane na tumuombe Mzee Kilomoni atulie kwanza maana akileta maneno hasira zote zitahamia kwake.
kila mtu karudi nafasi yake Yanga wakimataifa , Simba wa mchangani.