Haya ngoja twende hivi basi; Wachezaji ambao hawakushiriki dhidi ya rivers utd ni 3 ( Aucho, Mayele na Djuma) lakini hawa wachezaji 3 walikuwepo mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Zanaco ambapo yanga ilifungwa ikiwa nyumbani. Zanaco imeshika mkia kwenye kundi lake ambalo limeongozwa na Al ahly Tripol na pia huyo Zanaco kafungwa mechi zote mbili na Al ahly tripoli.
Nasisitiza , Al ahly Tripoli kamfunga Zanaco home and away. Zanaco alimfunga huyu anaeongoza ligi ya NBC akiwa na kikosi chake hiki hiki anachoshindia ligi. Je hapo vipi , NBC ni ngumu kuliko CAF Confederation?