Imeshacheza na Tabora United yenye wachezaji muhimu wasioweza kucheza mechi ile ikashinda 3-0 ikawa kicheko na nderemo eti wanaongoza ligi. Kituo kilichokuwa kinafuata ni kucheza na Fountain gates ambayo imezuiliwa na FIFA kusajili kutoka na deni la mbrazil Rodrigo, hivyo ingecheza na wachezaji wa kuungaunga na wasiokuwa na muunganiko ili kuipatia tena pts 3 na muunganiko. Tabia hii iliisaidia Azam na Fei toto kuifunga magoli mengi Tabora United iliyocheza n awachezaji 7 uwanjani bila kuwa na wachezaji wa akiba na kumsaidia Azam kupata pts 3 zilizosababisha kushika nafasi ya pili kwenye ligi hali iliyoigharimu Simba kwenye msimamo wa ligi, na Fei TOTO kufunga magoli 3 ya haramu yaliyosababisha awe na magoli 19 ya kufunga. Isingekuwa hii mechi ambayo Azam walipata pts 3 na magoli mengi huenda Simba ndiye aliyekuwa anashiriki CAF champions badala ya Azam fc.