Lijue Bunge la Afrika Mashariki na Jee Uchaguzi wa Wabunge wa CCM EALA Ulikuwa ni Uchaguzi Kweli Au Kiini Macho cha Uchaguzi?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,
Hii ni makala ya Jumapili ya Leo

Kwa Maslahi ya Taifa, inaendelea na makala elimishi za kuijua Jumuiya ya Afrika Mashariki, leo ni makala elimishi kuhusu kulijua Bunge la Afrika Mashariki, EALA na kiini macho cha uchaguzi wa Wabunge wa EALA wa Tanzania uliofanywa na Bunge letu!. Kilichofanyika kwenye uchaguzi wa EALA ndani ya Bunge letu, kunaacha maswali ya kujiuliza, hivi sisi Watanzania, "Do we real know what we need and what we want?!", "if we do, we wouldn't have let this joke of an election just passby!". Bunge letu lilipaswa kuletewa majina angalau mawili mawili kwa kila nafasi, halafu Bunge ndio lichague!. Kilichofanyika ni Bunge lilipelekewa majina ya kuchagua, uchaguzi uliofanyika ni wa mbunge mmoja tuu wa kutoka upinzani na kuthibisha majina 8 ya CCM!. Ili uchaguzi ufanyike, there must be choices to choose from, if there was no choices to choose from, huo haukuwa ni uchaguzi, ulikuwa ni kiini macho cha uchaguzi!.

Declaration of Interest
Kwa vile mimi nilishiriki mchakato wa uchaguzi huu ndani ya chama, nikashindwa kwa vigezo na kukubali kushindwa EALA: Waliopitishwa CCM, ni Kwa Haki!, Tulioachwa ni kwa Haki, Tumezidiwa Vigezo!. Thanks4 for Support, Nimekubali Matokeo Kiroho Safi! Kazi Iendelee! hivyo makala hii sio ya kutema nyongo ya kushindwa EALA bali hii ni makala elimishi kuelimisha umma kuhusu Bunge la Afrika Mashariki na kuwatendea haki Watanzania kwa kuwaonyesha matundu kwenye paa letu, hivyo kujua sisi Watanzania tunakwama wapi!.

leo tunamalizia mfululizo huu kwa SURA YA TISA: LIJUE BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI, JEE UCHAGUZI WA WABUNGE WA EALA ULIOFANYWA NA BUNGE LETU NI ULIKUWA UCHAGUZI KWELI AU NI KIINI MACHO CHA UCHAGUZI?.

Sura hii inajumuisha Ibara ya 48 mpaka Ibara ya 65. Bunge la Afrika Mashariki ni chombo kilichaonzishwa ili kutekeleza majukumu ya kutunga sheria za Jumuiya.

Ibara ya 48 inahusu Muundo wa Bunge.
Bunge lina wajumbe 9 wa kuchaguliwa kutoka kila nchi na wajumbe 9 ambao wataingia kwa nyadhifu zao. Hawa ni mawaziri 7 wa wizara za Nje na Katibu Mkuu wa jumuiya na Mwanasheria Mkuu wa EAC.

Spika atakuwa na madaraka ya kumwalika mtu yeyote ambaye mchango wake utahitajika katika kujadili hoja yoyote iliyoletwa mbele ya Bunge.

Ibara ya 53 inahusu Spika wa Bunge.
Spika atachaguliwa kutokana na wajumbe wa Bunge. Cheo hiki kitashikwa kwa mzunguko kati ya Nchi Wanachama.

Ibara ya 49 inahusu Kazi za Bunge.
Mbali na wajibu wa kutunga sheria, Bunge la jumuiya litakuwa pia chombo cha kuendeleza mahusiano na mbunge ya kitaifa ya Nchi Wanachama kwa mambo yanayohusu jumuiya.

Bunge litakuwa na kazi ya kupitisha bajeti ya jumuiya. Kabla ya kupitisha bajeti, Bunge litaangalia na kutathmini ripoti za shughuli za Jumuiya. Kazi nyingine ya Bunge itakuwa ni kujadili mambo yote yanayohusu jumuiya na kupeleka mapendekezo kwenye Baraza la Mawaziri. Bunge litakuwa pia na kazi ya kupendekeza majina ya watu kwa ajili ya uteuzi wa nafasi za Katibu Mkuu na maofisa wengine wateule wa jumuiya.

Utaratibu wa Kutunga Sheria
Utungwaji wa sheria utaanza kwa kupelekwa muswada Bungeni. Ikiwa muswada utapitishwa na Bunge, Spika ataupeleka kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi ili wautolee kibali.

Wakuu wa Nchi wakiukubali, unakuwa sheria. Wakiukataa utahesabika kuwa umepitwa na wakati.

Kupitishwa kwa muswada wa sheria na Wakuu wa Nchi unataka makubaliano ya Wakuu wote wa Nchi. Iwapo Mkuu mmoja wa Nchi atakataa, bado muswada huo hauwezi kupita.

Kanuni za Bunge
Bunge lina uwezo wa kutengeneza kanuni zake. Sheria na kanuni hizi zaweza kuhusiana na uwezo, haki, kinga ya wabunge na utaratibu wa uendeshaji wa shughuli zake.

Miswada ya kupelekwa Bungeni inaweza kupendekezwa na mjumbe yeyote. Lakini miswada hii iwe inahusiana na shughuli za Jumuiya na sheria zilizoainishwa katika Mkataba wa Jumuiya, kufuati Tanzania kupeleka majanga EALA, Tangu kuundwa kwa EALA, hakuna mbunge yoyote wa Tanzania, amewahi kupeleka muswada wowote!, Wabunge wa Kenya na Uganda pekee ndio wanaotamba mule!, Tanzania ipo ipo tuu kama hatupo!, au ni tupo tuu kama watazamaji zaidi kuliko washiriki!.

Uchaguzi wa Wabunge
Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki watachaguliwa na Bunge la Taifa la kila Nchi Mwanachama. Kwa hiyo, kila anayetaka kugombea itabidi akapigiwe kura na Bunge la nchi yake. Kwa Tanzania sio kila anayetaka, bali kila aliyepitishwa na chama cha siasa!.

Kila nchi itachagua wabunge tisa, ambao watakuwa siyo wabunge katika bunge la nchi husika. Uteuzi wa wabunge hao utaangalia uwiano wa uwakilishi wa vyama mbalimbali vya siasa vilivyoweza kuingia katika bunge la nchi husika. Uteuzi utaangalia pia jinsia na uwakilishi mwingine muhimu katika kila Bunge la nchi, husika.

Sifa za kuchaguliwa kuwa Mbunge katika Bunge la Jumuiya:
Awe ni raia wa Nchi Mwanachama
Awe na sifa ya kuchaguliwa kuwa mbunge katika nchi yake kulingana na sheria na taratibu za nchi hiyo. Wabunge wa EALA sio wabunge wa vyama, wala Bunge la EALA sio Bunge la kupiga siasa. Nchi majirani zetu, hutangaza nafasi hizi, raia wake huziomba sio kupitia vyama, ili kupata watu wenye uwezo.

Kwa sisi Tanzania, nafasi hizi hugombewa kupitia vyama, mimi kama mwandishi wa habari, nimekuwa nikihudhuria vikao vya Bunge hili, ukiangalia jinsi wabunge wa nchi za wenzetu wanavyochangia mada na mijadala, ukilinganisha ni michango ya wabunge wa Tanzania, kusema ukweli, ukiondoa wabunge wawili watatu waliokuwa active mule, kiukweli kabisa katika EALA iliyopita, Tanzania tulipeleka majanga!.

Kufuatia Tanzania kupeleka majanga EALA iliyopita, fursa ya EALA ilipojitokeza tena, kwanza mimi nami kama Mtanzania mwingine yeyote, pia nilitupa karata yangu, lakini pia nikatoa ushauri wa jinsi ya kupata watu mahiri. Nilishauri
  1. Kwa waliokuwa wawakilishi wetu kwenye Bunge hilo ambao wanataka kuwania tena nafasi hizo ili kuendelea kwa awamu yao ya pili, waulizwe katika uwakilishi wao, ndani ya Bunge hilo kwa miaka 5 iliyopita, wamechangia nini na wamelisaidia nini taifa?. Hili ndio Swali la Mhe. Msukuma kwa mmoja wa wagombea.
  2. Wagombea wa set agenda za Tanzania kama nchi anazotaka kwenda kuzipigania kwenye EALA na kupewa dakika 5 za kujieleza kwa lugha ya Kiingereza safi kilicho nyooka!. Moja ya sababu za baadhi ya wawakilishi wetu kuwa mabubu kwenye mijadala ya kuchangia hoja za Bunge la EALA, ni mtiririko wa Lugha, yaani kuongea Kiingereza safi fluently.
Kufuatia Watanzania 'kuwakataa wapinzani' kwenye sanduku la kura, kupitia uchaguzi mkuu 'huru' na wa 'haki' kufuatia Tanzania kuendesha chaguzi zetu kwa mutatis mutandis, ni Mbunge mmoja tuu huku Bara toka upinzani ndio amechaguliwa, tena kuchaguliwa kwake ni kwa bahati tuu ya Mtende, kufuatia wananchi wa jimbo lake kumuadhibu mbunge wao, kwa kitendo chake cha kushabikia uvunjifu wa katiba katika ukomo wa uongozi, ile ya "Atake Asitake", hivyo wananchi wakaamua kumpiga chini. Hivyo Bunge hili ni Bunge la chama kimoja predominantly, hivyo katika nafasi 9 za EALA, CCM ikapata nafasi 8 na upinzani nafasi 1.

Kiini Macho cha Uchaguzi Wa Wabunge wa EALA Bunge la Tanzania.
Sifa kuu ya kuchaguliwa EALA ni uraia wa nchi husika na (e) has proven experience or interest in consolidating and furthering the aims and the objectives of the Community.
Uchaguzi wa Wabunge
Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki watachaguliwa na Bunge la Taifa la kila Nchi Mwanachama. Kwa hiyo, kila anayetaka kugombea itabidi akapigiwe kura na Bunge la nchi yake.

Haki ya kila Mtanzania Kupiga Kura Ipo, ila Haki ya Kupigiwa Kura, Imeporwa!.
Kwa mujibu wa Ibara ya 5 ya Katiba ya JMT, kila Mtanzania aliyetimiza umri wa miaka 18, anaruhusiwa kupiga kura na kuchagua viongozi wake. Haki hii ya kila Mtanzania kuruhusiwa kupiga kura kuchagua viongozi wake, ilipaswa kwenda sambamba na kila Mtanzania kuwa na haki ya kupigiwa kura.
Hili nimelizungumza kwa kirefu hapa Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.

Kipengele hiki cha wagombea uongozi kudhaminiwa na chama cha siasa ndio kimeligharimu taifa hili kukosa viongozi wazuri kwa mizengwe tuu!. Kati ya wagombea 186 wa EALA, kulikuwa na watu fulani 4 ambao mimi nawafahamu, wana good track records, they would have made the best of the best EALA MPs!, lakini kwasababu ya ubatili huu wa kudhaminiwa na chama cha siasa, kati ya wanne hao, the good ones, ni mmoja tuu ndio alipitishwa na CCM na akaenda kuchinjiwa kwenye vikao vya CCM!.

Kiukweli kabisa, dhulma hii inalikosesha taifa letu viongozi wazuri!, hili nimeishaliandikia sana tuu Je, jicho la Rais Samia litauangazia Ubatili huu ndani ya Katiba yetu unaopora Haki ya Msingi, uliochomekewa kibatili ili kuuhalalisha?

Bunge letu limeweka uwiano wa wabunge 8 kutoka CCM na Mbunge 1 wa upinzani, CCM kikateua majina 8 kwenda kupigiwa kura bungeni!, yaani nafasi ni 8, CCM ikateua majina 8 kupigiwa kura na wabunge!, hebu tuambiane ukweli, Bunge lilikuwa linachagua au ni kiini macho tuu cha kuthibitisha chagua lo CCM?. Kwa maoni yangu, kiukweli kabisa, CCM imelikosea sana Bunge letu, na kuwakosea Watanzania kwa kulipatia Bunge letu wabunge 8 wa CCM, kwa ajili ya Bunge kuwathibitisha tuu!, something which is not right at all!.

Mkataba wa Afrika Mashariki umesema Mabunge yatachagua, toka uchaguzi wa kwanza wa EALA, vyama vilipeleka majina angalau mawili mawili kwa kila nafasi, halafu Bunge ndio likachagua, this time around, CCM ndio imechagua majina 8 na kulipa Bunge sio kuchagua, bali kuthibitisha tuu, chaguo la CCM!. Kwa tafsiri yangu, maana ya kuchagua, there must be some choices to choose from!, kama nafasi n inane, halafu unawapelekea majina 8!, huko ni kuchagua au kuthibitisha tuu?. Hivi tukikiita kilichofanyika Bungeni kwa wabunge wa EALA, ni Bunge letu tukufu kufanywa rubber stamp ya chaguo la Chama, jee sasa tunarejea kwenye Party Supremacy au….?!

Kwa maoni yangu, uchaguzi wa wabunge wa EALA uliofanywa na Bunge letu, Bunge limefanya uchaguzi wa kumchagua mbunge mmoja tuu wa upinzania ambapo ndio pekee kwenye choices, na kuwathibitisha wabunge 8 wa chaguo la CCM!.

Kufanya kosa sii kosa!, kosa ni kurudia kosa!, kama mwanzo tulipeleka majanga EALA, halafu tukarudia makosa yale yale!, unategemea nini?. Tena hapa naomba kutoa pongezi kwa Mbunge wa Geita, Dr. Joseph Kasheku Musukuma, swali lake, ndilo limeliokoa Bunge letu, angalau kuliondoa kokoro moja tuliopeleka EALA!.

Japo mimi ni mwana CCM, lakini pia ni mzalendo kwa taifa langu, kunapotokea mgongano wa kimaslahi kati ya maslahi ya CCM na Maslahi ya Taifa, mimi nitatanguliza mbele maslahi ya Taifa kwanza ndipo nije kwenye maslahi ya chama.

Tanzania ni nchi yetu sote, ni mali ya Watanzani wote wa vyama vyote, kunapokuja kwenye issues serious za kitaifa kama kuchangua wawakilishi wa nchi, tulipaswa tuweke pembeni siasa za vyama na kutanguliza mbele maslahi mapana ya Taifa.

Mungu Ibariki Tanzania.

Wasalaam
Paskali
 
Hata hili Bunge lina uhalali?

2020 tulikuwa na uchaguzi au uchafuzi?

Kama Bunge lenyewe si halali, hao wawakilishi wanaowachagua kwenda Bunge la Africa Mashariki wana uhalali gani?

CCM hii unayoiunga mkono, ndio CCM hiyo hiyo isiyotaka Tume Huru ya Uchaguzi Kama ambavyo haitaki tuwe na wagombea binafsi. Hivyo, ukipenda boga, penda na ua lake.
 
Pascal hivi ule uchaguzi wa ndani kupitia kura za maoni 2020 ulioshiriki jimbo la kawe wagombea mlikuwa 183 kama nakumbuka vzr..hivi chama kikongwe kama ccm kinakosa mfumo mzuri wa kuchuja wagombea kabla ya kupigiwa kura na bado ukaamini kinazo sifa za kuwa fair??? Wapi..na wakati gani??badala ya kulaumu kilichofanyika kwenye uchaguzi EALA..jilaumu wewe kwanza kuweka imani kwa watu wasiostahili ccm kwamba watakuwa fair this time wakati jana hawakuwa fair!
 
Kwani Hilo umelijua Leo? Wapinzani walipokuwa wanalalamiki hukuona Hilo. Au kwa kuwa limekugusa wewe. Eti mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu ni mchungu!
 
Kile siyo chama ni genge la matapeli watanashati walio vaa suti.
"Kama Mwasisi wake Mwalimu Nyerere aliikataa CCM na kusema CCM si Mama yake,nyinyi wanyonge ni nani mpaka mlazimishe kuwamo hu mo ndani ya icho chama?? Mwachieni Mama na wanawe wakina Nape, January, Mwigulu na Ridhiwan et al ambao wanaona kile chama na hii nchi ni urithi kutoka kwa Baba na Babu zao"
 
Mpaka Leo huwa sielewi Kwa Nini paskali hataki kujiunga na vyama vya ukombozi(upinzani) Kang'ang'ana tu na CCM Kwa Nini???!
Pascal Mayalla alitarajia kubebwa tangu enzi za kakake MEKO pamoja na kakake kumwambia ananjaa sana bado hakujielewa.. lkn kila kona anayojaribu anatupiliwa mbali angelijua hili nadhani angejirekebisha
 
Mayalla wewe mwenyewe Kuna uzi hapa ulipongea kabisa kuwa wabunge waliopatikana kutoka ccm wote walipatikana kihalali.
Mkuu Mmawia , kwenye upatikanaji wa wabunge wa EALA, wabunge hao wanachaguliwa na mabunge ya nchi husika. The bottom line ni uchaguzi unafanywa na Bunge. Kwa Tanzania mchakato wake unapitia two stages
1. Uchaguzi wa wagombea kwenye ngazi ya vyama. Mchakato huu kwa CCM ndio umekwenda vizuri, waliochaguliwa wamechaguliwa kwa haki, na tulioshindwa, tumeshindwa kwa haki kwa kuzidiwa sifa na waliochaguliwa EALA: Waliopitishwa CCM, ni Kwa Haki!, Tulioachwa ni kwa Haki, Tumezidiwa Vigezo!. Thanks4 for Support, Nimekubali Matokeo Kiroho Safi! Kazi Iendelee!

Baada ya mchakato huu, CCM ilipaswa ichague angalau majina mawili kwa kila nafasi ili kulipa Bunge fursa ya kuchagua.
Kilichofanyika hapa ni majina ya walioteuliwa na CCM yakapelekwa kwenye party caucas ya CCM, wakaibuka na majina 8 kwa zile nafasi 8 za CCM ndio yakapelekwa Bungeni.
2. Bunge kupokea majina kutoka kwenye vyama vya siasa, kisha wabunge ndio wafanye uchaguzi kuwachagua wabunge wa EALA. Ni vyama vya upinzani pekee ndio vimepeleka bungeni majina na bunge kuchagua, lakini kwa zile nafasi 8 za EALA za CCM, hakukuwa na uchaguzi because there was no choice to choose from, bali kuthibitisha wale 8 wa CCM.
Hili ni Bunge la 4 la EALA, mabunge yote matatu yaliyotangulia, Bunge la JMT, lilichagua wabunge wa EALA by choices from vyama vya siasa ikiwemo CCM ambayo ilichagua majina mawili mawili. This time CCM ndio imechagua wawakilishi 8 na kulipa Bunge kuwathibitisha tuu na sio kuwachagua!.
P
 
kitu kidogo sana unashindwa kukieleza ni kwamba chama chako bado kinashindwa kutembea kidemokras hili ndio tatizo lenu kuu. tarajio lilikuwa kura ipigwe ndani ya bunge lkn uhuni waliouzoea Chama chako cha lumumba kuzoea kucheza rafu .... kinacheza rafu mpaka ndani yake hili ndio tatizo SUGU. MMETEULIWA MAJINA NA CHAMA KIMEPITISHA NA BUNGE LENU LIKAITIKIA TU NDIOOOO.
 
PASKALI, nje ya mada!!embu siku moja tuletee wasifu wa wakili Murtaza Lakha(na picha yake ili tumjue)wengine mwaka ule wa 1976 hatukuepo!
 
Mkuu Mwala, haya usemayo ni kweli, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kuzungumzia dhambi ya ubaguzi, baada ya kuwabagua wapinzani, sasa tumeanza kubaguana sisi kwa sisi, wenyewe kwa wenyewe!, na hata kukulana, sasa tunakulana wenyewe kwa wenyewe!.

Kwenye EALA, CCM imepitisha watu wazuri kisha CCM hiyo hiyo ikawachinjia baharini baadhi yao!, na kutumia kokoro kuyabeba baadhi yale mazagazaga na makorokocho yao!, simply because ...
Ila pia ndio maana watu kama sisi tuko CCM kumsaidia chama kirudi kwenye line.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…