Mkuu
Mmawia , kwenye upatikanaji wa wabunge wa EALA, wabunge hao wanachaguliwa na mabunge ya nchi husika. The bottom line ni uchaguzi unafanywa na Bunge. Kwa Tanzania mchakato wake unapitia two stages
1. Uchaguzi wa wagombea kwenye ngazi ya vyama. Mchakato huu kwa CCM ndio umekwenda vizuri, waliochaguliwa wamechaguliwa kwa haki, na tulioshindwa, tumeshindwa kwa haki kwa kuzidiwa sifa na waliochaguliwa
EALA: Waliopitishwa CCM, ni Kwa Haki!, Tulioachwa ni kwa Haki, Tumezidiwa Vigezo!. Thanks4 for Support, Nimekubali Matokeo Kiroho Safi! Kazi Iendelee!
Baada ya mchakato huu, CCM ilipaswa ichague angalau majina mawili kwa kila nafasi ili kulipa Bunge fursa ya kuchagua.
Kilichofanyika hapa ni majina ya walioteuliwa na CCM yakapelekwa kwenye party caucas ya CCM, wakaibuka na majina 8 kwa zile nafasi 8 za CCM ndio yakapelekwa Bungeni.
2. Bunge kupokea majina kutoka kwenye vyama vya siasa, kisha wabunge ndio wafanye uchaguzi kuwachagua wabunge wa EALA. Ni vyama vya upinzani pekee ndio vimepeleka bungeni majina na bunge kuchagua, lakini kwa zile nafasi 8 za EALA za CCM, hakukuwa na uchaguzi because there was no choice to choose from, bali kuthibitisha wale 8 wa CCM.
Hili ni Bunge la 4 la EALA, mabunge yote matatu yaliyotangulia, Bunge la JMT, lilichagua wabunge wa EALA by choices from vyama vya siasa ikiwemo CCM ambayo ilichagua majina mawili mawili. This time CCM ndio imechagua wawakilishi 8 na kulipa Bunge kuwathibitisha tuu na sio kuwachagua!.
P