Lijue kundi la Wajamaa CCM linalojulikana kama Sukuma Gang

Lord Denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
23,491
Reaction score
57,973
Amani iwe nanyi Wanabodi.

Baada ya kulielezea kundi la Wanamtandao napenda tena kuwaletea Uchambuzi mdogo kuhusu kundi kinzani la Wajamaa ndani ya Chama cha Mapinduzi. Hawa wanajulikana kama Sukuma Gang au Chato Gang.

Kuna nadharia nyingi zimeenea kwa miaka kadhaa kuhusu uwepo wa Kundi la Sukuma Gang.

Nadharia hii ilianza kupata ushawishi huko Twitter ya zamani ambayo kwa sasa inajulikana kama X.

Kwa kifupi kiuhalisia hakujawahi kuwepo na kundi la Sukuma Gang. Jina hili lilipata umaarufu kutokana na kuhusishwa na aliyekuwa Rais wa Awamu ya 5 Bwana John Pombe Magufuli. Hii ni kutokana na Magufuli kuwaamini sana na kuwapa nafasi Makada wenye misimamo mikali ya Kijamaa wanaotoka Kanda ya Ziwa hasa kabila la Wasukuma na Makabila Madogo yanayohusiana na Wasukuma ( Watu wa Kanda ya Ziwa)

Historia ya kundi hili la Wajamaa wenye siasa kali wa Chama inahusishwa na wafuasi kindakindaki wa Sera za Ujamaa na Kujitegemea zilizoasisiwa na Rais wa Kwanza wa Tanganyika na Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Watu hawa mwanzoni hawakuwahi kuanzisha Kundi lao. Hawakuwahi kuwa na kundi bali walikuwa wana aminiana tu kama Watu wenye mawazo na misimamo inayofanana.

Baada ya kufeli kwa Sera za Kijamaa chini ya Serikali ya Awamu ya Kwanza watu hawa walianza kukosa ushawishi kwenye Chama na Serikali hivyo kufanya wengi kutopenda kuonesha misimamo yao wazi wazi.

Tofauti na Kundi la Mtandao ambalo liliundwa rasmi kabisa na kuhusisha watu wenye mipango madhubuti ya kuitawala hii nchi kwa muda mrefu, hawa wajamaa kwa miaka mingi hawakuwahi kuwa na mawazo hata ya kuanzisha kundi na kutambulika rasmi.

Baada ya kundi la Mtandao kushindwa kuweka mtu wao mwaka 2015. Magufuli aliyefanikiwa kushika uongozi wa nchi alianza kuona dalili za kuanza kupangiwa cha kufanya na kundi la Mtandao.

Ili kujihami Magufuli alianza kutafuta Wana CCM wenye misimamo mikali ya kijamaa ili ajenge upya nchi nje ya ushawishi wa kundi la Wanamtandao. Kutokana na Magufuli kuanza kujenga rasmi kundi la Wazalendo wenye misimamo mikali huku akitumia watu wengi kutoka Kanda ya Ziwa ilipelekea kundi hili kuitwa rasmi Sukuma Gang au Chato Gang.

Kwa kukosa uzoefu, Sukuma Gang ilishindwa kuwa madhubuti toka chini. Hii ni kwa sababu hawakuwa na watu, hawakuwa na mizizi. Hawakuwa na mipango ya pamoja na hawakuwa na common goal.

Kwa kuwa kundi la Wana Mtandao lilianza tangu mwaka 1993 na 1994 ilimuwia vigumu sana Magufuli kuweza kushindana na Wana Mtandao waliokita mizizi kwenye sekta zote nyeti kuanzia ulinzi na usalama, utumishi wa umma, biashara hadi huduma za kijamii.

Hadi sasa kundi la Wajamaa linajaribu kuji organise na kujifunza kutokana na makosa waliyofanya ili waweze kuirudisha CCM ya kijamaa na watawale nchi kwa milengo ya kijamaa.

Mazuri ya Kundi la Wajamaa wa CCM (Sukuma Gang)

1. Wanatizama sana maslahi ya watu wengi ambao ni wananchi wa kawaida. Mipango yao muda mwingi ni ya kulinufaisha kundi kubwa la Wananchi masikini.

2. Wana itizama Nchi zaidi kuliko maslahi yao binafsi.

Mapungufu (Madhaifu) yao;
1. Wana roho mbaya sana. Wana amini sana kwenye ubabe na hata kupoteza maisha ya mtu kwa njia zozote zile. ( Hasa anayeenda kinyume na mawazo yao). Hawapendi kushindana kwa hoja. Kidogo tu Wanakupoteza. Rejea jaribio la mauaji ya Tundu Lissu.

2. Ni wagumu sana kusoma siasa za dunia na kubadilika kutokana na mabadiliko ya Dunia. Wana misimamo mikali ambayo inaweza kuifanya nchi kukwama kiuchumi kama zilivyo Venezuela na Cuba.

3. Wana kasumba ya kuamini kila mwenye fedha ni mwizi hivyo kuwashughulikia vibaya.

4. Pamoja na kuwa Wajamaa wana vi element vya Ufisadi na unafiki. Ubaya wao zaidi kwenye hili Wana tabia ya kudhurumu mali za watu. Hili limefanya elites kutowakubali sana. Pia wana vitabia vya kujilimbikizia na kupenda kuwa na mali nyingi suala ambalo ni nje ya misingi ya imani za kijamaa.

Kwa maelezo haya ni vigumu sana kusema nchi inalihitaji kundi lolote kati ya haya mawili ( Wana Mtandao vs Sukuma Gang)

Kikubwa nchi ipate Katiba Mpya

No Reforms No Election ✊️ ✌️

Cc. DR HAYA LAND 30 JR
 
Kuna nadharia nyingi zimeenea kwa miaka kadhaa kuhusu uwepo wa Kundi la Sukuma Gang.

Nadharia hii ilianza kupata ushawishi huko Twitter ya zamani ambayo kwa sasa inajulikana kama X.

Kwa kifupi kiuhalisia hakujawahi kuwepo na kundi la Sukuma Gang. Jina hili lilipata umaarufu kutokana na kuhusishwa na aliyekuwa Rais wa Awamu ya 5 Bwana John Pombe Magufuli. Hii ni kutokana na Magufuli kuwaamini sana na kuwapa nafasi Makada wenye misimamo mikali ya Kijamaa wanaotoka Kanda ya Ziwa hasa kabila la Wasukuma na Makabila Madogo yanayohusiana na Wasukuma ( Watu wa Kanda ya Ziwa)

Historia ya kundi hili la Wajamaa wenye siasa kali wa Chama I ihusishwa na wafuasi kindakindaki wa Sera za Ujamaa na Kujitegemea zilizoasisiwa na Rais wa Kwanza wa Tanganyika na Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Watu hawa mwanzoni hawakuwahi kuanzisha Kundi lao. Hawakuwahi kuwa na kundi bali walikuwa wana aminiana tu kama Watu wenye mawazo na misimamo inayofanana.

Baada ya kufeli kwa Sera za Kijamaa chini ya Serikali ya Awamu ya Kwanza watu hawa walianza kukosa ushawishi kwenye Chama na Serikali hivyo kufanya wengi kutopenda kuonesha misimamo ya wazi.

Tofauti na Kundi la Mtandao ambalo liliundwa rasmi kabisa na kuhusisha watu wenye mipango madhubuti ya kuitawala hii nchi kwa muda mrefu, hawa wajamaa kwa miaka mingi hawakuwahi kuwa na mawazo hata ya kuanzisha kundi na kutambulika rasmi.

Baada ya kundi la Mtandao kushindwa kuweka mtu wao mwaka 2015. Magufuli aliyefanikiwa kushika uongozi wa nchi alianza kuona dalili za kuanza kupangiwa cha kufanya na kundi la Mtandao.

Ili kujihami Magufuli alianza kutafuta Wana CCM wenye misimamo mikali ya kijamaa ili avenge upya nchi nje ya ushawishi wa kundi la Wanamtandao. Kutokana na Magufuli kuanza kujenga rasmi kundi la Wazalendo wenye misimamo mikali huku akitumia watu wengi kutoka Kanda ya Ziwa ilipelekea kundi hili kuitwa rasmi Sukuma Gang.

Kwa kukosa uzoefu, Sukuma Gang ilishindwa kuwa madhubuti toka chini. Hii ni kwa sababu hawakuwa na watu, hawakuwa na mizizi. Hawakuwa na mipango ya pamoja na hawakuwa na common goal.

Kwa kuwa kundi la Wana Mtandao lilianza tangu mwaka 1993 na 1994 ilimuwia vigumu sana Magufuli kuweza kushindana na Wana Mtandao waliokita mizizi kwenye sekta zote nyeti kuanzia ulinzi na usalama, utumishi wa umma, biashara hadi huduma za kijamii.

Hadi sasa kundi la Wajamaa linajaribu kuji organise na kujifunza kutokana na makosa waliyofanya ili waweze kuirudisha CCM ya kijamaa.

Mazuri ya Kundi la Wajamaa wa CCM (Sukuma Gang)

1. Wanatizama sana maslahi ya watu wengi ambao ni wananchi wa kawaida. Mipango yao muda mwingi ni ya kulinufaisha kundi kubwa la Wananchi masikini.

2. Wana itizama Nchi zaidi kuliko maslahi yao binafsi.

Mapungufu (Madhaifu) yao;
1. Wana roho mbaya sana. Wana amini sana kwenye ubabe na hata kupoteza maisha ya mtu kwa njia zozote zile. ( Hasa anayeenda kinyume na mawazo yao). Hawapendi kushindana kwa hoja. Kidogo tu Wanakupoteza.

2. Ni wagumu sana kusoma siasa za dunia na kubadilika kutokana na mabadiliko ya Dunia. Wana misimamo mikali ambayo inaweza kuifanya nchi kukwama kiuchumi.

3. Wana kasumba ya kuamini kila mwenye fedha ni mwizi hivyo kuwashughulikia vibaya.

4. Pamoja na kuwa Wajamaa wana vi element vya Ufisadi. Ubaya wao zaidi kwenye hili Wana tabia ya kudhurumu mali za watu. Hili limefanya elites kutowakubali sana.

Kwa maelezo haya ni vigumu sana kusema nchi inalihitaji kundi lolote kati ya haya mawili.

Kikubwa nchi ipate Katiba Mpya

No Reforms No Election ✊️ ✌️
bashite yupo kundi gani hapo, manake na yeye ni msukuma na ana roho mbaya.
 
Wajamaa wasipokuwa wajamaa matajiri na matapeli wa madaraka.

Kwa wanaowahubiria uzalendo ni kuwa maskini ila wao ni matajiri,hovyo kabisa hao.

Watu wa hivyo wapigwe vita maana Dunia hawataki ni waharibifu.
 
Tatizo lao kuu ndo hilo
 
bashite yupo kundi gani hapo, manake na yeye ni msukuma na ana roho mbaya.
Bashite alikuwa recruited na kundi la Wanamtandao katika kumvuruga Lowassa.

Ni kijana wa kulelewa na Marehemu Samweli Sitta aliyekuwa Spika wa Bunge na Mwana Mtandao Mwandamizi.

Ni usukuma uliomfanya ajikute kundi la Sukuma Gang.

Huyu ni ndumilakuwili. Anaenda na upepo.
 
Hakuna mjamaa pale bhana usidanganye watu.
Mtu anatembelea v8 huyo ni mjamaa gani? Au ujamaa ni kulitaja jina la julius kambarage tu???
Hilo ni moja ya mapungufu yao makubwa yanayofanya wasikubaliwe na elites wa nchi hii.
 
Hili kundi halipo ni nadharia tu.

Yaliyopo ni makundi mawili, 1.wenye njaa vs 2. walishiba.
Kuwepo na kutokuwepo kumeelezewa vizuri mwanzo kabisa wa huu uzi.

Kuhusu njaa na kutokuwa na njaa nakubaliana na wewe. Makundi haya mawili yanafanana kwenye jambo moja la msingi. Vita ya Madaraka.
 
Haya makundi ni ya kimaslahi zaidi. Sio lazima kabila liwe msukuma ili mwanasiasa awe kundi la sukuma gang.

Sawa na Msoga gang, sio lazima mtu awe mkwere ili aweze kujulikana kuwa ni wa kundi hilo.

JPM hakuweza kuficha kuwathamini watu wa njia moja na yeye, akimsikia mtu anaongea kwa lafudhi ya kisukuma tayari anamuweka kwenye orodha ya vijana kwa ajili ya vyeo na nafasi. Walikuwemo wahaya kina Bashiru Ally, Wazinza kina Biteko.

Baadae wakaongezeka watendaji serikalini wenye mlengo mmoja na JPM, kina Sabaya waliolia siku ya kumuaga pale uwanja wa Taifa.

Kundi likapoteza nguvu baada ya kifo cha mwanzilishi, limebakia na chuki za Pole Pole na uanaharakati wa Mpina. Mwingine ni mkurugenzi mkuu wa zamani wa TPA.
 
Ukweli ndo huo. Makundi haya yanafanana kwenye hilo suala la uchu wa madaraka na maslahi binafsi.

Na kiuhalisia kwa sehemu kubwa yanaiumiza sana Tanzania kuliko kuisaidia.

Suluhisho pekee ni Vyombo vya dola kulazimisha nchi inapata Katiba Mpya iliyo bora inayowaweka Wanasiasa chini ya Mifumo na kuwaondoa kuwa sauti ya mwisho kuamua Fate ya Taifa hili.
 
Kutaja kabila la wasukuma, Tena kutumia jina "Gang" Kisha kulihusisha na Wajamaa, ni mparaganyiko mkubwa sana wa kifikra.

Ukabila tulishauvuka zamani sana.

Tusiingie mtego wa wahuni kutugawa.

Tabaka lililopo ni Hilo la watu maskini sana ,(wasionacho)vs wanaojilimbikizia utajiri kwa rushwa na upendeleo(Walionacho).

Habari za ukabila weka Pembeni.
 
Naona kama contradiction maana kundi hilo hilo liwe linajali sana maslahi ya wananchi na nchi kiujumla kuliko maslahi yao binafsi ila hapo hapo hilo kundi pia ni mafisadi na waroho wa madaraka.

Au mimi sijaelewa?
 
Back
Top Bottom