SAHIHI...
Wanajamii kushirikiana kwa wema ama uovu hili jambo halijaanza leo na wala halitakwisha leo...
Hili ndilo linalokumbusha
umuhimu wa Kujitafuta Kiroho (Kiingereza > " Soul Searching")...
Hata hapa na sasa, tuseme Septemba 2025 - Mei 2026, kinachoendelea ni fursa ya wanajamii kujitafakari na kudhamiria kujisahihisha;
siyo kuendekeza mambo ya "ushabiki-matukio-Hasi' ama 'Uchawa' ama 'Unafiki'...
Hii "
Novena ya Kanisa Katoliki" ipo kiufundi kabisa, si jambo la mzaha -- ndiyo mlango wa uponyaji wenyewe kwa taifa!
Wakati mmoja, siku za mbele, katika mwelekeo wa siku zenye kheri jambo hili la kuhakikisha wanajamii wanakuwa na mwangaza wa kweli kwa ajili ya 'UTU na Kujichagulia' litakuwa ni shughuli ya taasisi itakayokuja kufahamika kama '
Vituo vya Utamaduni'; kwa leo unaweza kusema hili ndilo jambo linaloyakinishwa kwa '
Utaasisi wa Dini' katika 'Maisha na Ustawi wa Wanajamii kupitia 'Uhuru wa Kuabudu'...
Ndiyo, itashangaza kusema --
kesho yeyote ni 'mawezekano ya Kikwantumu', hakuna kesho 'iliyokazika' (Kiingereza > "Fixed"); kwa hivyo mtu yeyote asidanganyike na 'Unabii' ama 'Tabiri' ama 'Ramli'; mtu yeyote (1) mwenye kuona yale ya wakati ujao. ama (2) kuyahisi yajayo kwa 'mafahamu wa Kiroho' -- ikiwa kweli ameona yafaa kuyazungumza, kwa sehemu hayo 'yajayo', basi lazima atakuwa na muktadha akilifu wa 'dirisha fulani la matazamio'...
'Dirisha la Matazamio' ni namna ya Uono na Ufirikirifu Mifumo uliyo ni tata, kwa kuwa
sayansi ya kuyasoma 'matukio' ama 'mseto wa matukio yumkini' ni kitu ambacho wanajamii, waliowengi, bado hawajajijengea uzoefu na umahiri; japo ujuzi wa haya unafunguo zake kwa ajili ya kutafsiri -- kutafsiri kana je, ni 'Mkondo Wakati Upi' unaofanania kutukia kutegemeana na 'Mlima wa Dhamiri za Utu' -- Utu jamii kisomoni?
Mambo ya 'Sala na Kazi' si chochote bali ujuzi, utundu na ufundi wa kuchochea Akili na Utambuzi wa/katika Jamii kwa ajili ya Dhamiri na Nia; ili '
Mlima wa Dhamiri' ujiseti kulingana na 'Dirisha la Matazamio'; kwa mfano, kwenye mapokeo ya Ukristo, kuna muktadha akilifu wa dhamira na Udhamirifu kwa ajili ya 'Mapenzi yako yafanyike Duniani kama Mbinguni'... Hili kiufundi ni kitu ambacho kwenye Sayansi ya Ufahamu na Mafahamu inatambulika kama kuseti 'Vekta Dhamirifu'(Kiingereza > "Vectored Intention"); Sisi sote tuna ishi kwa dira na makusudi -- dira na makusudi katika kujitafsiri 'Matendo yetu' na 'UISHO wetu' kwa wakati hata wakati -- Mambo ya "Kujichagulia"...
Wakati Mmoja, sehemu kubwa ya UMMA utakuja kutambua
'Sala ya Bwana' ni ufunguo kwa 'Dirisha la Matazamio' kwa ajili ya kushiriki Kheri ya wale wenye 'Neema'... Hapa kwetu Tanzania, Shauri la Kikatiba juu ya UTU lina msingi wa 'Dirisha la Matazamio' kwa ajili ya UJAMAA na KUJITEGEMEA; kwa hivyo kinachoendelea kwa sasa, ile kuonekana wanajamii wasanuana kuhusu '
Mbivu na Mbichi' za Utaifa wao, ni fursa ya mageuzi makuu ya Kiutamaduni kwa Taifa la Tanzania...
Kwa mtu yeyote anayeweza 'KUSALI katika NEEMA ya SALA ya BWANA', kwake itakuwa wazi -- Kitu cha kwanza katika 'Kujitafuta kiroho' ni kuitafuta 'AMANI ya BWANA wa ULIMWENGU' (Kiarabu > " Rabil-al-alamini"); Kwenye mapokeo ya Uislamu,
Suurat Faatiha ni Muktadha akilifu wa Sala ile ile ya Bwana kwa msingi wa 'NIA'... MAISHA-KUISHI-UISHO ni 'NIA na UPENDO'--Mambo ya 'Unyoofu na Mapenzi Mema'...
NIA na UPENDO katika 'AMANI ya BWANA wa ULIMWENGU' ndiyo hutengeneza, katika sisi, ile nasibu ya 'Vekta Dhamirifu' kwa ajili ya kukusudia
'HAKI na AMANI' katika UJAMII wetu...
TOFAUTI zetu, zile za
kukosa KOHERENSIA na SINEJIA kwa ajili ya 'Makusudi yenye Kheri' za UJAMII ndiyo Mwanzo wa "Dhiki na Faraja" katika MAISHA-KUISHI-UISHO ilivyo ni 'UMOJA ama UTENGANO'; Kwenye Sala ya Bwana, 'Vekta Dhamirifu' ya Kwanza ni Kudhamiria 'Amani'; inayofuata, ya pili, ni muktadha akilifu wa Kudhamiria 'Haki'...
SASA, Kutolandana kwa
'vekta Amani' na 'vekta Haki' katika akili na mioyo ya wanajamii wenyekushiriki mapana fulani ya Mazingira, Ustawi na Utamaduni ndiyo mwanzo kwa nasibu za thawabu ama/na madhambi; kwa kuwa wanajamii wenyewe wanaweza kubagaizana na kubanangana kwa kukosa 'mwelekeo muafaka' kwa ajili ya ule muktadha akilifu wa kheri ya pamoja. Hili lafanya "kusahihisha na Kujisahihisha' ni bidifu (Kiingereza > "Imperative") kwa ajili ya 'Kuyanyoosha Mapito yetu' kama viumbe wenye Usentienti-Konsayansi-Nuru ya Ufahamu...
'Kuyanyoosha Mapito yetu' kama viumbe wenye Usentienti-Konsayansi-Nuru ya Ufahamu; kulingana na ukadinali wa 'Sala ya Bwana' ndiyo asili ya '
Vekta Udugu'; ambavyo Udugu ni udhamirifu endelevu wa nia kwa ajili ya 'Kusamehe/Kusamehana/Kusamehewa na CHANZO cha Kheri na UZIMA JAMII'; kuna "uunje Ndani wa Dhamiri/Udhamirifu"--MAISHA-KUISHI-UISHO ni Unje-Ndani wa "
Kazi za Roho Mtakatifu'; sisi sote tunaishi na kuwepo kwa 'Neema za Uzima'--Uzima wa Kiroho. Kwa hivyo, asili 'madhambi' ama 'thawabu' ni 'makandokando ya Nia na Dhamiri' zetu kama viumbe wenye kuishi katika ulimwengu wa madhahiri...
Analojia za 'Madhambi' ama 'Thawabu' si kitu cha dhahania, kwa kuwa chochote kile tunachokitenda kimawazo, kimwili fiziki, pumzi za dhamiri hufuzu ile 'sifa-tabia-hadhi' ya kuwa ni 'Dhambi' ama 'Thawabu'... Kwenye Mapokeo ya Ukristo haya mawili, dhambi na thawabu, husemwa ni muktadha akilifu wa (1) 'kupungukiwa na Utukufu / Radhi ya Mungu' ama/na(2) 'Kustahili Malipo Mema', kulingana na 'Nia na Dhamiri Zetu' wakati mmoja hata mwingine... Katika mapokeo ya Uislam, Suurat Fatiha huakisi haya haya kwa muktadha akilifu wa '
Hatma za UTU, Kujichagulia na Wakati' ...
Sala ni
kuomba kuongozeka vema katika kheri za Utu kadiri ya Kile kinachotujalia Rehema na Neema za Maisha na huku kumbe 'Rehema na Neema' zinaweza kutafsiriwa isivyokheri katika Mtu/Mwanajamii kama fursa ya kutawaliana, kudhulumiana na kudhuriana kwa jina la 'Ontolojia ya Taasisi'; mambo ya 'Ushawishi-Kushawishika-Kushawishi'...
Katika 'Sala ya Bwana', muktadha akilifu wa
'Vekta Udugu' na 'Vekta Uhuru' ndiyo ufunguo wa 'Marejeo Ngamani'; Katika Ulimwengu, wa wanajamii wenye nasibu ya Utashi, mashauri ya 'AMANI na HAKI' daima hugubikwa na Undumilakuwili wa 'Dhamira na Nia zetu' ilivyo nasibu pereniali ya 'Kwenda Tezi na Omo'. Hili lafanya "Kujichagulia" daima ni ufunguo wa 'Kurejea katika Kitovu cha Fahamu na Mafahamu' kwa namna inayoakisi 'Ukubuishi wa Fahamu na Mafahamu'.... Mambo ya 'Gurudumu la Dhamma'...
Maisha-Kuishi-Uisho ni
'Ukubuishi wa Fahamu na Mafahamu' ilivyo ni 'Mambo ya Nyakati'; ambavyo UTU wetu ni sehemu ya 'fumbo la Uzima' ilivyo ni CHANZO/MUNGU/UMUNGU... Kiufundi, Mungu ni Uzima unaoyakinisha mema na maovu vilevile, kwa hivyo ni unaivu kudhani eti 'Roho wa Mungu' yupo ndani ya 'Mtu Mwema' halafu hayuko kwa 'Mtu asiyemwema'...
Mungu ni
'Nguvu yenye Utukufu' ambayo sisi sote tunaifuzu kwa uwema ama uovu--Uwe ni (1) 'Muuaji/Mzinzi/Mlevi/Mlozi/Mlaghai' ama (2) 'Mwenyehuruma/Mseja/Mndoa/Mwanasala/Mwanabaraka/Muungwana''; kinachobainisha mawili haya kwa wakati ni 'Uweza-Utayari-Umahiri' wako mwenyewe katika "Kujichagulia".
'Uweza-Utayari-Umahiri' wako mwenyewe katika "Kujichagulia" ndiyo
ufunguo wa maajabu na mastaajabu ya UZIMA ilivyo ni Ukubuishi wa Fahamu na Mafahamu; ambavyo 'Mtu wa Sala na Kazi' anaweza kubayanisha 'Ushirika wake wa Kiroho" kwa wale wote waliowema na waovu na huku 'Mtu Muovu' hawezi kubaini ya kwamba chochote kile kisichochema anachomtendea mwenzake, kuna namna yeye mwenyewe anaishi kustahili kutendewa hivyo na kuonja upande wa pili wa 'dhamira na matendo' yake--haya ndiyo mambo ya 'Karma'; anachokipanda mtu kwa 'dhamira na matendo ' ndicho anacho/atachokivuna wakati mmoja hata mwingine...
Vituo vya Utamaduni, katika siku za mbele zenye umma wenye Utimamu wa Akili na Mafahamu, haya mambo yatakuwa yakifahamika katika umma wa wengi na tena kwa 'Ujuzi-maarifa-maarifu' ilivyo ni Ku-JUA ilivyo bora. Hili lafanya 'Sala na Kazi' ndiyo kipimo cha UTU na Kazi; kinachoanza daima ni UTU halafu Kazi huakisi tu UTU wenyewe... Hili ndilo linalokumbusha shauri la '
Utafuteni Kwanza Ufalme wa Mbingu na Haki yake na Mengine mtazidishiwa'...
SASA, kuna mambo ya kiufundi kuhusu 'Sala'; leo hii kinachofahamika na wengi kama 'Sala' bado ni Ujuujuu mno wa Shauri la Ukweli wenyewe khasa wa Mambo... Ikibidi kukosoa 'dosari za kiufundi' na wanajamii wenyewe na tena kuhusiana na 'Sala na Kusali' hili itakuwa ni kusema wazi wazi,
'kusali siyo kumpangia Mungu cha Kufanya'.... Ikiwa unalazimika 'kuomba kwa kumpangia Mungu' basi utambue kuna kupata ama kukosa...
Kiufundi, Sala ni Unyenyekevu na Kutambua japo unaweza kuwa unajua jambo, Mungu ana-JUA ilivyobora; hivyo tafuta kustahiki 'Hekima ya Mbingu/BWANA/Mola' ili ikujaalie ku-JUA ilivyobora na basi kuziongoza njia zako...
Kiufundi, Sala ni dhamiri ya Kujitakasa ili ustahili yale yaliyosafi kwa NIA na Dhamiri kwa kuwa Mungu ni 'Usentienti katika Nguvu yenye Utukufu' -- Usentienti katika Nguvu na Utukufu kiasi kwamba ni 'Uweza' na 'Utayari' wako kwa wakati utafuzu kile unachostahili ili kuwa kipitishi cha 'Ufalme na Nguvu'... Mambo ya kuweza kufanyika ni kipitishi kwa 'Mapenzi Ya-Ke'(Ufalme wa Mbingu')....
Kiufundi, Sala ni dhamiri ya kutakasa mapana ya UTU na Utamaduni ili FURAHA, AMANI na MAPENZI MEMA vitawale UZIMA wa JAMII yeyote -- jamii yenye kustiri uwepo wako kama Mmoja wa wanajamii; ambavyo
Uwepo wako kama 'Mtu wa Sala na Kazi' ni 'Baraka ya Wazi ama Iliyositirika' miongoni mwa wanajamii wenyewe. Hili lafanya, Daima Uwepo wa 'Watu wa Sala na Kazi' ni mbaraka wa Neema hata kwa mambo yasiyotarajiwa na wanajamii -- wanajamii wanaoishi nao na kushiriki 'mambo ya nyakati'...
Basi ndiyo yawa,
hata Taifa nalo ni Ujamii -- Ikiwa wanajamii hawa wanaoongozeka vema katika 'Sala na Kazi', basi hata 'Ulinzi na Usalama' wao hautaishia kwenye
mambo ya mtu kumtegemea mtu mwingine kitaasisi na miundo ya utendaji kijamii; kwani kuna '
ngazi nne za sala'--mambo ya kujijengea uweza na uwezo wa kutenda kimwili, kihisia, Kiakili na Kiroho...
Wakati mmoja isije kushangaza kwa Umma wa Watanzania,
haya yote yamesitirika kwenye heraldri ya Taifa la Watanzania kama 'Ngao ya Ustawi' na 'Pembe za Ndovu'... Mambo ya 'Ulinzi wa Malaika wa Utamaduni na Jadi'; Kwa kuwa UHURU-UDUGU-HAKI-AMANI ni Ukadinali wa '
Marejeo ya NIA kwa SURA ya NCHI na Tawala'...
UJAMAA na KUJITEGEMEA ni 'Fumbo la Imani'... Kule watu wa Sala na Kazi walioasisi taifa hili wamekusudia TUELEKEE HUKO kwa Vekta Dhamirifu za 'Sala ya Bwana'....