Lijue kundi la Wanamtandao. Kundi linalosemwa kuiongoza Tanzania tangu 1995 hadi sasa

Ndo maana nilimuuliza Membe hajawai kua hata DG wa Tiss hata kua Boss wa PSU sasa nguvu alizitoa wapi Mambe alikua kachero lank yake ilikua hajifaka nilioweka hapo
Kwani Tendewa alipokuwa anafanya kipindi cha Lowassa mwaka 2015 alikuwa DG wa TISS?

Kwani Mshauri wa Rais Kheri anayeongoza kundi la Wasiojulikana ni DGIS?
 
Amani iwe nanyi wanabodi

Ukiambiwa kuhusu uwepo wa kundi hili unaweza kusema hizi ni stori za Kusadikika. Ila Ukweli ulio wazi ni kwamba hizi sio stori za kusadikika, sio series za kihindi, kituruki wala kikorea.

Ili kulifahamu kundi hili unapaswa kuufahamu mfumo wa Chama cha Mapinduzi wa kumpata mgombea wao Urais tangu wakati wa Chama Kimoja.

Kwa wasiofahamu Chama cha Mapinduzi hujulikana kama Chama dola kwa sababu ndo kilikuwa Chama pekee cha siasa nchini Tanzania miaka michache baada ya Uhuru hadi mwaka 1992 tulipoingia rasmi kwenye mfumo wa vyama vingi.

Kwa sababu hiyo vyombo vya ulinzi na usalama vilikuwa na nafasi kubwa sana kwa siasa za ndani za Chama hiki. Kwa kifupi ili uwe Mgombea Urais wa CCM ilikuwa ni lazima Idara ya Usalama ya Chama watoe taarifa ya kukusafisha na kusema unafaa kuwa Rais. Ikumbukwe Idara hii ndo baadae ilikuja kujulikana kama Kamati ya Maadili ya Chama na ni bahati mbaya Idara hii imekuwa vilevile tangu wakati wa Chama kimoja hadi sasa.

Kundi la Wanamtandao ni kundi lililoundwa baada ya Nyerere kuondoka kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi. Kundi hili liliongozwa na Makada wenye ushawishi na mizizi ya vyombo vya dola ndani ya CCM.

Kundi hili liliundwa kwa mjumuiko wa Makada mbalimbali waliokuwa Watumishi wa Idara ya Usalama, Jeshi la Wananchi, Wafanyabiashara, Wanazuoni na wengineo wengi hasa kutokana na Serikali ya Awamu ya Pili kufungua milango ya Kiuchumi na kuachana na Uchumi wa Kijamaa.

Dhumuni kuu la kuundwa kwa kundi hili ndani ya CCM ilikuwa ni kukamata Uongozi wa CCM na Taifa kwa kipindi kirefu. Kundi hili lilijipanga ku dominate siasa za nchi hii kuanzia 1995 hadi kwenye uhai wote wa Taifa la Tanzania.

Kundi hili liliandaa vijana, wataalam wa masuala ya kiuchumi na ku recruit kila waliyemuona anafaa kwa maslahi mapana ya kundi lao.

Baada ya Taarifa kumfikia Mzee Nyerere wakati wa Uchaguzi wa 1995. Mzee alitoka Butiama kurudi Dar ili kusimamia show kundi hili lisikiteke Chama. Uzuri kwa kuwa ulikuwa Uchaguzi wao wa Kwanza, Kundi hili halikufanikiwa kuchukua Uongozi wa Chama na Nchi mwaka 1995.

Kosa kubwa alilolifanya Mkapa ni kupuuzia nguvu ya Kundi hili hivyo kwa kuwa walikuwa na nguvu aliendelea kuwaacha kwenye nafasi nyeti. Walikamata Idara za Fedha za Chama kwa Rostam kuwa Mweka Hazina wa Chama, Kikwete aliendelea kuwa Waziri wa Mambo ya Nje huku akiitumia nafasi hiyo vilivyo kulijenga kundi hili ndani na nje ya nchi.

Mzee wa Vijisenti aliendelea kuwa Mwanasheria wao makini, Lowassa akiwa mwanamikakati mkuu wa ndani huku Bernad Membe akijenga vizuri mahusiano ya kundi hilo na Idara ya Usalama.

Walifanikiwa kuweka watu kwenye nafasi mbalimbali za Uongozi chini ya Mkapa na pia walifanikiwa kukwapua hela nyingi sana BOT kupitia sakata la EPA ili kujijengea ushawishi wa kifedha.

Kufikia mwaka 2005 Kundi hili lilikuwa kama Kansa ambayo imeshaila nchi nzima. Kwa kuwa Nyerere alishatangulia mbele ya Haki mwaka 1999, Mkapa hakuwa na namna akashindwa nguvu na wakachukua uongozi wa Chama na Nchi mwaka huo kwenye Uchaguzi Mkuu. Ripoti ya maadili iliyotengenezwa na Idara ya Usalama ya Chama kumkatalia Kikwete asiwe Rais ilibadilishwa mwishoni na kutengenezwa Mpya iliyomsafisha na kuchukua usukani. Inasemwa suala hili lilisababisha kifo cha aliyekuwa Mwana usalama wa Chama Mwandamizi Marehemu Balozi Daud Mwakawago.

kundi hili limeendelea kutawala siasa za Tanzania tangu mwaka huo 2005 hadi sasa ambapo kwa sehemu kubwa chini ya Mzee wa Msoga wao ndo wamekuwa wakiwa na ushawishi mkubwa zaidi katika siasa za Nchi na Chama huku wakiamua nani awe nani.

Mazuri ya Kundi la Wanamtandao;
1. Ni kundi linaloamini kwenye soko huria. Hawaamini kwenye Serikali kuhodhi Uchumi wa Nchi hivyo kufanya ustawi mzuri wa uchumi kwa nchi.

2. Pamoja na kukumaliza ukiingilia maslahi yao ila mara nyingi hawaamini sana katika kuua watu na kuwakomoa vibaya. Wanaweza hata kukupa nusu mkate ili utulie ufanye mambo yako na usiwabughuzi kwenye kula yao.

Mabaya ya Kundi la Wanamtandao;

1. Ni Mafisadi sana sana. Wana amini katika kuhodhi njia zote za kiuchumi wao tu. Hivyo kunufaika kwanza wao na vizazi vyao. Hili linasababisha nchi kutokuwa na maendeleo ya Uhakika kwa wananchi kutokana na mgawanyo usio sawa wa rasilimali za Taifa.

2. Wanapenda kuhodhi madaraka wao tu. Wana amini ili wafanikishe madili yao ni lazima washike njia zote za kufanya maamuzi. Hili linapelekea watu wenye uwezo wanaoweza kulisaidia Taifa kusonga mbele kushindwa kupata nafasi za Uongozi.

3. Wanasababisha kukua kwa kasi sana kwa kundi la Wasio nacho kwa sababu kiuhalisia Uchumi unashikiliwa na wao. Hawawazi sana kuhusu ustawi wa kundi hili la Wasio nacho.

Mada inayofuata Nitakuelezea Kundi la Sukuma Gang. Kundi lililotengenezwa Kwa Makusudi kulikabili Kundi la Mtandao au wanaojulikana sasa Msoga Gang.

Tutakuwepo!

No Reforms No Election ✊️✌️
Polepole alisema kuwa vinara wa hilo kundi walikuwa watano na mmoja tu kafariki.Tupate Majina yao;
1. Kikwete
2. Lowassa (RIP)
3. Rostam
4. Nchimbi
5. .........
 
Walikuwa wengi sana!

1. Kikwete - The Master Mind
2. Rostam - King's Maker
3. Lowassa- The Chief Operator
4. Sitta- General Manager
5. Membe- The Shadow
6. Nchimbi- Logistics
7. Bashe- Chief Assistant to the King's Maker

Kinana alikuwa overall in-charge of Innovations and Operations

In this list watatu ndo wametangulia mbele ya Haki - Sitta, Lowassa na Membe.
 
Na very arrogant Kisha washamba
Nimewaelezea vizuri kwenye hii mada👇
 
Naangalia akili za Lowassa, Chenge, Kikwete (master mind), Rostam Aziz ambaye tuliaminishwa ni wakala wa CIA, hawa vichwani ni wa kawaida Sana, pamoja na kuwa wahitimu wa Havard.

MIkakati na mbinu zao ni za "kijamaa" Sana japo wao wanamini katika ubepari. Ndio maana Jiwe aliwahenyesha Sana japo naye ndio hivyo, kumbe hii nchi Watu wenye vichwa vizito wanaweza kuanzisha Illuminati Yao na wakapindua meza!
 
Semeni yoote, hakuna kundi litakalochukua nchi bila ridhaa ya deep state
Jakaya si mwanamtandao,ni mtu wa dola,aliutumia mtandao kisha akaubwaga punde tu baada ya kushika hatamu
2015 akaubwaga tena baada ya kuujeruhi vibaya kwa kutumia Richmond
Wanamtandao wanafurahi Sana wakiona tunaamini kuwa wamefarakana, hawa ni wamoja Hadi Kesho....
Wana kiapo kama cha Illuminat
 
Kundi la mtandao liliasisiwa na mabwanyenye wa Chadema 1993 kwa sababu wao hawakuwa na interest na nafasi ya Urais

Ningekuwa na muda ningefafanua zaidi
Wewe Acha kupotosha Hujui kitu!
Wafuatao ndio original mtandao:

Kikwete
Lowassa
Rostam
Sitta
Kinana
Anna Makinda

Halafu wasaidizi wao wakuu wakiwa :
Nchimbi
Didas Masaburi
Makongoro Mahanga
 
Wewe Acha kupotosha Hujui kitu!
Wafuatao ndio original mtandao:

Kikwete
Lowassa
Rostam
Sitta
Kinana
Anna Makinda

Halafu wasaidizi wao wakuu wakiwa :
Nchimbi
Didas Masaburi
Makongoro Mahanga
Kikwete hakuwepo kabisa kwenye kundi la mtandao walimuomba mwaka ule ule 1995

Samahani lakini 😄✔️
 
Amani iwe nanyi wanabodi

Ukiambiwa kuhusu uwepo wa kundi hili unaweza kusema hizi ni stori za Kusadikika. Ila Ukweli ulio wazi ni kwamba hizi sio stori za kusadikika, sio series za kihindi, kituruki wala kikorea.

Ili kulifahamu kundi hili unapaswa kuufahamu mfumo wa Chama cha Mapinduzi wa kumpata mgombea wao Urais tangu wakati wa Chama Kimoja.

Kwa wasiofahamu Chama cha Mapinduzi hujulikana kama Chama dola kwa sababu ndo kilikuwa Chama pekee cha siasa nchini Tanzania miaka michache baada ya Uhuru hadi mwaka 1992 tulipoingia rasmi kwenye mfumo wa vyama vingi.

Kwa sababu hiyo vyombo vya ulinzi na usalama vilikuwa na nafasi kubwa sana kwa siasa za ndani za Chama hiki. Kwa kifupi ili uwe Mgombea Urais wa CCM ilikuwa ni lazima Idara ya Usalama ya Chama watoe taarifa ya kukusafisha na kusema unafaa kuwa Rais. Ikumbukwe Idara hii ndo baadae ilikuja kujulikana kama Kamati ya Maadili ya Chama na ni bahati mbaya Idara hii imekuwa vilevile tangu wakati wa Chama kimoja hadi sasa.

Kundi la Wanamtandao ni kundi lililoundwa baada ya Nyerere kuondoka kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi. Kundi hili liliongozwa na Makada wenye ushawishi na mizizi ya vyombo vya dola ndani ya CCM.

Kundi hili liliundwa kwa mjumuiko wa Makada mbalimbali waliokuwa Watumishi wa Idara ya Usalama, Jeshi la Wananchi, Wafanyabiashara, Wanazuoni na wengineo wengi hasa kutokana na Serikali ya Awamu ya Pili kufungua milango ya Kiuchumi na kuachana na Uchumi wa Kijamaa.

Dhumuni kuu la kuundwa kwa kundi hili ndani ya CCM ilikuwa ni kukamata Uongozi wa CCM na Taifa kwa kipindi kirefu. Kundi hili lilijipanga ku dominate siasa za nchi hii kuanzia 1995 hadi kwenye uhai wote wa Taifa la Tanzania.

Kundi hili liliandaa vijana, wataalam wa masuala ya kiuchumi na ku recruit kila waliyemuona anafaa kwa maslahi mapana ya kundi lao.

Baada ya Taarifa kumfikia Mzee Nyerere wakati wa Uchaguzi wa 1995. Mzee alitoka Butiama kurudi Dar ili kusimamia show kundi hili lisikiteke Chama. Uzuri kwa kuwa ulikuwa Uchaguzi wao wa Kwanza, Kundi hili halikufanikiwa kuchukua Uongozi wa Chama na Nchi mwaka 1995.

Kosa kubwa alilolifanya Mkapa ni kupuuzia nguvu ya Kundi hili hivyo kwa kuwa walikuwa na nguvu aliendelea kuwaacha kwenye nafasi nyeti. Walikamata Idara za Fedha za Chama kwa Rostam kuwa Mweka Hazina wa Chama, Kikwete aliendelea kuwa Waziri wa Mambo ya Nje huku akiitumia nafasi hiyo vilivyo kulijenga kundi hili ndani na nje ya nchi.

Mzee wa Vijisenti aliendelea kuwa Mwanasheria wao makini, Lowassa akiwa mwanamikakati mkuu wa ndani huku Bernad Membe akijenga vizuri mahusiano ya kundi hilo na Idara ya Usalama.

Walifanikiwa kuweka watu kwenye nafasi mbalimbali za Uongozi chini ya Mkapa na pia walifanikiwa kukwapua hela nyingi sana BOT kupitia sakata la EPA ili kujijengea ushawishi wa kifedha.

Kufikia mwaka 2005 Kundi hili lilikuwa kama Kansa ambayo imeshaila nchi nzima. Kwa kuwa Nyerere alishatangulia mbele ya Haki mwaka 1999, Mkapa hakuwa na namna akashindwa nguvu na wakachukua uongozi wa Chama na Nchi mwaka huo kwenye Uchaguzi Mkuu. Ripoti ya maadili iliyotengenezwa na Idara ya Usalama ya Chama kumkatalia Kikwete asiwe Rais ilibadilishwa mwishoni na kutengenezwa Mpya iliyomsafisha na kuchukua usukani. Inasemwa suala hili lilisababisha kifo cha aliyekuwa Mwana usalama wa Chama Mwandamizi Marehemu Balozi Daud Mwakawago.

kundi hili limeendelea kutawala siasa za Tanzania tangu mwaka huo 2005 hadi sasa ambapo kwa sehemu kubwa chini ya Mzee wa Msoga wao ndo wamekuwa wakiwa na ushawishi mkubwa zaidi katika siasa za Nchi na Chama huku wakiamua nani awe nani.

Mazuri ya Kundi la Wanamtandao;
1. Ni kundi linaloamini kwenye soko huria. Hawaamini kwenye Serikali kuhodhi Uchumi wa Nchi hivyo kufanya ustawi mzuri wa uchumi kwa nchi.

2. Pamoja na kukumaliza ukiingilia maslahi yao ila mara nyingi hawaamini sana katika kuua watu na kuwakomoa vibaya. Wanaweza hata kukupa nusu mkate ili utulie ufanye mambo yako na usiwabughuzi kwenye kula yao.

Mabaya ya Kundi la Wanamtandao;

1. Ni Mafisadi sana sana. Wana amini katika kuhodhi njia zote za kiuchumi wao tu. Hivyo kunufaika kwanza wao na vizazi vyao. Hili linasababisha nchi kutokuwa na maendeleo ya Uhakika kwa wananchi kutokana na mgawanyo usio sawa wa rasilimali za Taifa.

2. Wanapenda kuhodhi madaraka wao tu. Wana amini ili wafanikishe madili yao ni lazima washike njia zote za kufanya maamuzi. Hili linapelekea watu wenye uwezo wanaoweza kulisaidia Taifa kusonga mbele kushindwa kupata nafasi za Uongozi.

3. Wanasababisha kukua kwa kasi sana kwa kundi la Wasio nacho kwa sababu kiuhalisia Uchumi unashikiliwa na wao. Hawawazi sana kuhusu ustawi wa kundi hili la Wasio nacho.

Mada inayofuata Nitakuelezea Kundi la Sukuma Gang. Kundi lililotengenezwa Kwa Makusudi kulikabili Kundi la Mtandao au wanaojulikana sasa Msoga Gang.

Tutakuwepo!

No Reforms No Election ✊️✌️
Kumbe mapambano yalianza mapema! Jakaya mwanafunzi aliyefeli BA economics akapitishwa kwa kulazimishwa na chama dola akapata marginal "Pass" anaburuza hadi maprof saa hii!
Walipofanikiwa kumtoa Nyerere haikutosha ikabidi wamtoe mkapa! JPM alipoleta shida zaidi wakamuondolea kwanza power house zake zote! Kumbukeni Katibu mkuu kiongozi wa ikulu, Kumbukeni Balozi Mahiga, Kumbukeni wote waliondoka ghafla kwa kisingizio cha korona!
Sukuma gang liliendelea kupambana hadi wakamtoa mwanamtandao maarufu Membe!! hata baada ya Magu kukata!!
JK, Rostam, Makamba, Nape,and co Mungu anawaona!!
 
JK kijana pendwa wa Nyerere.

JK kumkata Lowasa, na kumlazimisha Rostam aachane na Siasa za CCM (Kujivua Gamba) ilikuwa ni kujaribu kuuvunja mtandao.
 
Back
Top Bottom