Lijue kundi la Wanamtandao. Kundi linalosemwa kuiongoza Tanzania tangu 1995 hadi sasa

Lijue kundi la Wanamtandao. Kundi linalosemwa kuiongoza Tanzania tangu 1995 hadi sasa

Ila kiuhalisia ni bora hawa kuliko Sukuma Gang, wale jamaa ni makatili sana
Ukiingilia masrahi wa nchi/ watu maskini, hawana msamaha na wewe. Watakula tu. Ukiwa mjenga nchi wa masrahi ya nchi, unakua mtu wao.
 
Walikuwa wengi sana!

1. Kikwete - The Master Mind
2. Rostam - King's Maker
3. Lowassa- The Chief Operator
4. Sitta- General Manager
5. Membe- The Shadow
6. Nchimbi- Logistics
7. Bashe- Chief Assistant to the King's Maker

Kinana alikuwa overall in-charge of Innovations and Operations

In this list watatu ndo wametangulia mbele ya Haki - Sitta, Lowassa na Membe.
Sitta mtoe hapo
 
Yes Lissu hajawai kua na Conection na wa Mjini Lissu ni alivyotokea Magu hakua na Conection na watoto wa mjini hata. Sijui Lissu na Magu Walipishana wapi sijui nani aliwachonganisha but wangeungana wale Magu na Lissu basi biashara ilikua inaishia hapo
Shida ilianza pale Lisu alipoungana na Acasia kuleta hofu kwa wananchi na alipokubali kua wakili wa hayo makampuni ambayo Magu alikua anarekebisha mikataba nayo
 
Amani iwe nanyi wanabodi

Ukiambiwa kuhusu uwepo wa kundi hili unaweza kusema hizi ni stori za Kusadikika. Ila Ukweli ulio wazi ni kwamba hizi sio stori za kusadikika, sio series za kihindi, kituruki wala kikorea.

Ili kulifahamu kundi hili unapaswa kuufahamu mfumo wa Chama cha Mapinduzi wa kumpata mgombea wao Urais tangu wakati wa Chama Kimoja.

Kwa wasiofahamu Chama cha Mapinduzi hujulikana kama Chama dola kwa sababu ndo kilikuwa Chama pekee cha siasa nchini Tanzania miaka michache baada ya Uhuru hadi mwaka 1992 tulipoingia rasmi kwenye mfumo wa vyama vingi.

Kwa sababu hiyo vyombo vya ulinzi na usalama vilikuwa na nafasi kubwa sana kwa siasa za ndani za Chama hiki. Kwa kifupi ili uwe Mgombea Urais wa CCM ilikuwa ni lazima Idara ya Usalama ya Chama watoe taarifa ya kukusafisha na kusema unafaa kuwa Rais. Ikumbukwe Idara hii ndo baadae ilikuja kujulikana kama Kamati ya Maadili ya Chama na ni bahati mbaya Idara hii imekuwa vilevile tangu wakati wa Chama kimoja hadi sasa.

Kundi la Wanamtandao ni kundi lililoundwa baada ya Nyerere kuondoka kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi. Kundi hili liliongozwa na Makada wenye ushawishi na mizizi ya vyombo vya dola ndani ya CCM.


Kundi hili liliundwa kwa mjumuiko wa Makada mbalimbali waliokuwa Watumishi wa Idara ya Usalama, Jeshi la Wananchi, Wafanyabiashara, Wanazuoni na wengineo wengi hasa kutokana na Serikali ya Awamu ya Pili kufungua milango ya Kiuchumi na kuachana na Uchumi wa Kijamaa.

Dhumuni kuu la kuundwa kwa kundi hili ndani ya CCM ilikuwa ni kukamata Uongozi wa CCM na Taifa kwa kipindi kirefu. Kundi hili lilijipanga ku dominate siasa za nchi hii kuanzia 1995 hadi kwenye uhai wote wa Taifa la Tanzania.

Kundi hili liliandaa vijana, wataalam wa masuala ya kiuchumi na ku recruit kila waliyemuona anafaa kwa maslahi mapana ya kundi lao.

Baada ya Taarifa kumfikia Mzee Nyerere wakati wa Uchaguzi wa 1995. Mzee alitoka Butiama kurudi Dar ili kusimamia show kundi hili lisikiteke Chama. Uzuri kwa kuwa ulikuwa Uchaguzi wao wa Kwanza, Kundi hili halikufanikiwa kuchukua Uongozi wa Chama na Nchi mwaka 1995.

Kosa kubwa alilolifanya Mkapa ni kupuuzia nguvu ya Kundi hili hivyo kwa kuwa walikuwa na nguvu aliendelea kuwaacha kwenye nafasi nyeti. Walikamata Idara za Fedha za Chama kwa Rostam kuwa Mweka Hazina wa Chama, Kikwete aliendelea kuwa Waziri wa Mambo ya Nje huku akiitumia nafasi hiyo vilivyo kulijenga kundi hili ndani na nje ya nchi.

Mzee wa Vijisenti aliendelea kuwa Mwanasheria wao makini, Lowassa akiwa mwanamikakati mkuu wa ndani huku Bernad Membe akijenga vizuri mahusiano ya kundi hilo na Idara ya Usalama.

Walifanikiwa kuweka watu kwenye nafasi mbalimbali za Uongozi chini ya Mkapa na pia walifanikiwa kukwapua hela nyingi sana BOT kupitia sakata la EPA ili kujijengea ushawishi wa kifedha.

Kufikia mwaka 2005 Kundi hili lilikuwa kama Kansa ambayo imeshaila nchi nzima. Kwa kuwa Nyerere alishatangulia mbele ya Haki mwaka 1999, Mkapa hakuwa na namna akashindwa nguvu na wakachukua uongozi wa Chama na Nchi mwaka huo kwenye Uchaguzi Mkuu. Ripoti ya maadili iliyotengenezwa na Idara ya Usalama ya Chama kumkatalia Kikwete asiwe Rais ilibadilishwa mwishoni na kutengenezwa Mpya iliyomsafisha na kuchukua usukani. Inasemwa suala hili lilisababisha kifo cha aliyekuwa Mwana usalama wa Chama Mwandamizi Marehemu Balozi Daud Mwakawago.

kundi hili limeendelea kutawala siasa za Tanzania tangu mwaka huo 2005 hadi sasa ambapo kwa sehemu kubwa chini ya Mzee wa Msoga wao ndo wamekuwa wakiwa na ushawishi mkubwa zaidi katika siasa za Nchi na Chama huku wakiamua nani awe nani.

Mazuri ya Kundi la Wanamtandao;
1. Ni kundi linaloamini kwenye soko huria. Hawaamini kwenye Serikali kuhodhi Uchumi wa Nchi hivyo kufanya ustawi mzuri wa uchumi kwa nchi.

2. Pamoja na kukumaliza ukiingilia maslahi yao ila mara nyingi hawaamini sana katika kuua watu na kuwakomoa vibaya. Wanaweza hata kukupa nusu mkate ili utulie ufanye mambo yako na usiwabughuzi kwenye kula yao.

Mabaya ya Kundi la Wanamtandao;

1. Ni Mafisadi sana sana. Wana amini katika kuhodhi njia zote za kiuchumi wao tu. Hivyo kunufaika kwanza wao na vizazi vyao. Hili linasababisha nchi kutokuwa na maendeleo ya Uhakika kwa wananchi kutokana na mgawanyo usio sawa wa rasilimali za Taifa.

2. Wanapenda kuhodhi madaraka wao tu. Wana amini ili wafanikishe madili yao ni lazima washike njia zote za kufanya maamuzi. Hili linapelekea watu wenye uwezo wanaoweza kulisaidia Taifa kusonga mbele kushindwa kupata nafasi za Uongozi.

3. Wanasababisha kukua kwa kasi sana kwa kundi la Wasio nacho kwa sababu kiuhalisia Uchumi unashikiliwa na wao. Hawawazi sana kuhusu ustawi wa kundi hili la Wasio nacho.

Mada inayofuata Nitakuelezea Kundi la Sukuma Gang. Kundi lililotengenezwa Kwa Makusudi kulikabili Kundi la Mtandao au wanaojulikana sasa Msoga Gang.

Tutakuwepo!

No Reforms No Election ✊️✌️
Kumbe ndio maana mtoto wa Mkulima alisikika akisema wenye Chama wameamua 😂🤣 !
 
Shida ilianza pale Lisu alipoungana na Acasia kuleta hofu kwa wananchi na alipokubali kua wakili wa hayo makampuni ambayo Magu alikua anarekebisha mikataba nayo
Lissu hajawahi kuungana na makampuni yeyote yale. Lissu alionya na kushauri ipasavyo kuhusu hatua sahihi zilizopaswa kuchukuliwa.

Wajamaa walidharau ushauri wa Lissu matokeo yake Nchi imelipa na inaendelea kulipa Matrilioni ya Pesa za Walipa kodi hadi leo kwa kupuuza ushauri wake.

Lissu alikuwa sahihi.
 
MIAKA SIO MINGI NAHISI HII NCHI ITAKUJA KUGAWANYIKA VIPANDE VINNE KAMA SIO VITATU, KUTOKANA NA MKANGANYIKO WA MAMBO MENGI YANAYO ENDELEA NCHINI HIVI SASA.

MFANO MUUNGANO WAKITAPELI, UFISADI KUPINDUKIA, UONGOZI MBAYA KUPUUZA MAONI YA WANANCHI, RUSHWA KUKITHIRI, UWAJIBIKAJI ZERO SERIKALINI,

Naona kabisa hivi ni vitu vinavyo weza kutudikisha kwenye mpasuko hatari mfano.👇

Sukuma gang watakuwa na nchi yao itakayo jumuisha mikoa yote ya lake zone ikiwemo Kigoma,Singida,Tabora,Mara,Shinyanga,Geita,Kagera na Mwanza yenyewe kama makao makuu ya serikali hio 😂🔥

Nchi ya pili itakuwa Zanzibar. Itakuwa nchi kamili hakuna kivuli cha muungano tena.

Nchi ya tatu itakuwa mikoa yote ya pwani ya bahari ya hindi na majirani zake ikiwemo Morogoro, pwani,Tanga,Lindi,Mtwara, Dodoma, na Dar es salaam.

Nchi ya nne ni mikoa yote ya nyanda za juu kusini. Tukianza na Ruvuma,Njombe,Iringa,Rukwa,Katavi,Songwe na Mbeya kama makao makuu ya nchi hiyo. 🤣🔥

Nchi ya tano itakuwa upande wa kaskazini mwa Tz yaani Manyara,Arusha,Kilamnjaro tayari Tayari nchi hio imekamilika. 🤔

Kwa maana hiyo Tanganyika na Tz zitakuwa zimefia hapo 😭 sababu ya ulafi na kiburi cha CCM.

Ni ndoto nilikuwa naota jamani msije mkanifokea hapa. 🥺
Inabidi ukamatwe kwa kusambaza mawazo ya kihaini. Full stop.
 
Lissu hajawahi kuungana na makampuni yeyote yale. Lissu alionya na kushauri ipasavyo kuhusu hatua sahihi zilizopaswa kuchukuliwa.

Wajamaa walidharau ushauri wa Lissu matokeo yake Nchi imelipa na inaendelea kulipa Matrilioni ya Pesa za Walipa kodi hadi leo kwa kupuuza ushauri wake.

Lissu alikuwa sahihi.
Tafuta ukweli utafahamu zaidi.
 
Walikuwa wengi sana!

1. Kikwete - The Master Mind
2. Rostam - King's Maker
3. Lowassa- The Chief Operator
4. Sitta- General Manager
5. Membe- The Shadow
6. Nchimbi- Logistics
7. Bashe- Chief Assistant to the King's Maker

Kinana alikuwa overall in-charge of Innovations and Operations

In this list watatu ndo wametangulia mbele ya Haki - Sitta, Lowassa na Membe.
Kuna Mtandao Daraja la I: - walianzia Saigon Kariakoo
Mtandao Daraja la II;- waliingia KK kati ya 2007 na 2017
Mtandao Daraja la III; - hawa ni vijana wa kazi wa Mtandao Daraja la I
baadhi yao utawaona kwenye hizi picha
CCM ina wenyewe
1754520951798.png

1754521042014.png
 
Alikuwa ni mwana mtandao ila naye aliutaka Uwaziri Mkuu kwa udi na uvumba awamu ya Nne !
Huyo hajui kuwa zile hekaheka ilikuwa na grievances za sitta baada ya mtandao kumuahidi uwaziri mkuu na kumtosa ndio yakawa yale yaliyokuwa mpk EL kutoswa uwaziri mkuu.
 
Back
Top Bottom