Lijue kundi la Wanamtandao. Kundi linalosemwa kuiongoza Tanzania tangu 1995 hadi sasa

Amani iwe nanyi wanabodi

Ukiambiwa kuhusu uwepo wa kundi hili unaweza kusema hizi ni stori za Kusadikika. Ila Ukweli ulio wazi ni kwamba hizi sio stori za kusadikika, sio series za kihindi, kituruki wala kikorea.

Ili kulifahamu kundi hili unapaswa kuufahamu mfumo wa Chama cha Mapinduzi wa kumpata mgombea wao Urais tangu wakati wa Chama Kimoja.

Kwa wasiofahamu Chama cha Mapinduzi hujulikana kama Chama dola kwa sababu ndo kilikuwa Chama pekee cha siasa nchini Tanzania miaka michache baada ya Uhuru hadi mwaka 1992 tulipoingia rasmi kwenye mfumo wa vyama vingi.

Kwa sababu hiyo vyombo vya ulinzi na usalama vilikuwa na nafasi kubwa sana kwa siasa za ndani za Chama hiki. Kwa kifupi ili uwe Mgombea Urais wa CCM ilikuwa ni lazima Idara ya Usalama ya Chama watoe taarifa ya kukusafisha na kusema unafaa kuwa Rais. Ikumbukwe Idara hii ndo baadae ilikuja kujulikana kama Kamati ya Maadili ya Chama na ni bahati mbaya Idara hii imekuwa vilevile tangu wakati wa Chama kimoja hadi sasa.

Kundi la Wanamtandao ni kundi lililoundwa baada ya Nyerere kuondoka kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi. Kundi hili liliongozwa na Makada wenye ushawishi na mizizi ya vyombo vya dola ndani ya CCM.

Kundi hili liliundwa kwa mjumuiko wa Makada mbalimbali waliokuwa Watumishi wa Idara ya Usalama, Jeshi la Wananchi, Wafanyabiashara, Wanazuoni na wengineo wengi hasa kutokana na Serikali ya Awamu ya Pili kufungua milango ya Kiuchumi na kuachana na Uchumi wa Kijamaa.

Dhumuni kuu la kuundwa kwa kundi hili ndani ya CCM ilikuwa ni kukamata Uongozi wa CCM na Taifa kwa kipindi kirefu. Kundi hili lilijipanga ku dominate siasa za nchi hii kuanzia 1995 hadi kwenye uhai wote wa Taifa la Tanzania.

Kundi hili liliandaa vijana, wataalam wa masuala ya kiuchumi na ku recruit kila waliyemuona anafaa kwa maslahi mapana ya kundi lao.

Baada ya Taarifa kumfikia Mzee Nyerere wakati wa Uchaguzi wa 1995. Mzee alitoka Butiama kurudi Dar ili kusimamia show kundi hili lisikiteke Chama. Uzuri kwa kuwa ulikuwa Uchaguzi wao wa Kwanza, Kundi hili halikufanikiwa kuchukua Uongozi wa Chama na Nchi mwaka 1995.

Kosa kubwa alilolifanya Mkapa ni kupuuzia nguvu ya Kundi hili hivyo kwa kuwa walikuwa na nguvu aliendelea kuwaacha kwenye nafasi nyeti. Walikamata Idara za Fedha za Chama kwa Rostam kuwa Mweka Hazina wa Chama, Kikwete aliendelea kuwa Waziri wa Mambo ya Nje huku akiitumia nafasi hiyo vilivyo kulijenga kundi hili ndani na nje ya nchi.

Mzee wa Vijisenti aliendelea kuwa Mwanasheria wao makini, Lowassa akiwa mwanamikakati mkuu wa ndani huku Bernad Membe akijenga vizuri mahusiano ya kundi hilo na Idara ya Usalama.

Walifanikiwa kuweka watu kwenye nafasi mbalimbali za Uongozi chini ya Mkapa na pia walifanikiwa kukwapua hela nyingi sana BOT kupitia sakata la EPA ili kujijengea ushawishi wa kifedha.

Kufikia mwaka 2005 Kundi hili lilikuwa kama Kansa ambayo imeshaila nchi nzima. Kwa kuwa Nyerere alishatangulia mbele ya Haki mwaka 1999, Mkapa hakuwa na namna akashindwa nguvu na wakachukua uongozi wa Chama na Nchi mwaka huo kwenye Uchaguzi Mkuu. Ripoti ya maadili iliyotengenezwa na Idara ya Usalama ya Chama kumkatalia Kikwete asiwe Rais ilibadilishwa mwishoni na kutengenezwa Mpya iliyomsafisha na kuchukua usukani. Inasemwa suala hili lilisababisha kifo cha aliyekuwa Mwana usalama wa Chama Mwandamizi Marehemu Balozi Daud Mwakawago.

kundi hili limeendelea kutawala siasa za Tanzania tangu mwaka huo 2005 hadi sasa ambapo kwa sehemu kubwa chini ya Mzee wa Msoga wao ndo wamekuwa wakiwa na ushawishi mkubwa zaidi katika siasa za Nchi na Chama huku wakiamua nani awe nani.

Mazuri ya Kundi la Wanamtandao;
1. Ni kundi linaloamini kwenye soko huria. Hawaamini kwenye Serikali kuhodhi Uchumi wa Nchi hivyo kufanya ustawi mzuri wa uchumi kwa nchi.

2. Pamoja na kukumaliza ukiingilia maslahi yao ila mara nyingi hawaamini sana katika kuua watu na kuwakomoa vibaya. Wanaweza hata kukupa nusu mkate ili utulie ufanye mambo yako na usiwabughuzi kwenye kula yao.

Mabaya ya Kundi la Wanamtandao;

1. Ni Mafisadi sana sana. Wana amini katika kuhodhi njia zote za kiuchumi wao tu. Hivyo kunufaika kwanza wao na vizazi vyao. Hili linasababisha nchi kutokuwa na maendeleo ya Uhakika kwa wananchi kutokana na mgawanyo usio sawa wa rasilimali za Taifa.

2. Wanapenda kuhodhi madaraka wao tu. Wana amini ili wafanikishe madili yao ni lazima washike njia zote za kufanya maamuzi. Hili linapelekea watu wenye uwezo wanaoweza kulisaidia Taifa kusonga mbele kushindwa kupata nafasi za Uongozi.

3. Wanasababisha kukua kwa kasi sana kwa kundi la Wasio nacho kwa sababu kiuhalisia Uchumi unashikiliwa na wao. Hawawazi sana kuhusu ustawi wa kundi hili la Wasio nacho.

Mada inayofuata Nitakuelezea Kundi la Sukuma Gang. Kundi lililotengenezwa Kwa Makusudi kulikabili Kundi la Mtandao au wanaojulikana sasa Msoga Gang.

Tutakuwepo!

No Reforms No Election ✊️✌️
S

Lord, ASANTE SANA KWA SOMO HILI.
 
Kundi la mtandao liliasisiwa na mabwanyenye wa Chadema 1993 kwa sababu wao hawakuwa na interest na nafasi ya Urais

Ningekuwa na muda ningefafanua zaidi
Wee hua unajitokezaga kama vile kichwa cha mb'oo kinavyojitokeza kama boxer imetoboka!!! Hueleweki unasimamiaga nn!!
 
Ni porojo zao tu.
Mwalimu alimpenda JK tangu JK akiwa mwanafunzi chuo kikuu DSM
Na ata wapashaji habari hawasemi mwalimu alimchukia Jk hapana. Wanasema alimpenda na pia inasemwa mwalimu alikua anafahamiana vzr tu na baba yake jk, baba yake jk akihudmu ktk chama na ata kuwa mkuu wa wilaya. Alikua ana urafiki na mwalimu kwani pia kuna mambo alikua akinsaidia mwalimu 'ya kiswahili'..inasemekana ivyo. Lakini hao hao wapashaji wanakwenda mbali na kusema jk hamkubali mwalimu na huwa hampi heshima kubwa kama wanasiasa wengine wanavyompatia mwalimu heshima kubwa.
 
Hao wanaosema JK hamkubali JKN ni maneno yao tu, unajua mzee wa Msoga amekuwa punching bag nzuri ya kuondolea frustrations zao. Hii ni kwa sababu ya easy going nature yake, na pia ni mtu aliyebarikiwa kuwa juu kwenye mambo mengi tu tangu ujana wake. Alipokuwa kijana nyota yake ya uongozi na likabiliry ilikuwa juu sana kuliko peers wake.

Kuhusu kumkubali JKN, JK kafanya kazi na JKN kwa miaka mingi sana, na last time wamefanya kazi wote ni pake JK alipokuwa waziri wa mambo ya nje ktk serikali ya BWM huku JKN akiwa msuluhishi wa mgogoro wa Burundi.

Speech kibao nimemsikia JK akimpa kongole JKN.

JKN alikuwa na reservations zake kwa Lowasa na si JK
 
Kundi la mtandao liliasisiwa na mabwanyenye wa Chadema 1993 kwa sababu wao hawakuwa na interest na nafasi ya Urais

Ningekuwa na muda ningefafanua zaidi
Acha kupotosha historia! Wafuatao ndio waasisi wa mtandao :
Jakaya Kikwete
Rostam Aziz
Edward Lowassa
Samuel Sitta
Anna Makinda
Hao wengine walikuja kusajiliwa baadae; ndio wakina Emmanuel NCHIMBI, Bernard Membe, Masaburi, Makongoro Mahanga etc
Sasa nani bwanyenye wa Chadema kati ya hao? Acha hizo we chawa!
 
Kikwete aliingizwa baada ya Nyerere kusema Lowassa hawezi kuwa Rais wa JMT 😂😂😂

Hili swala liko wazi Kikwete hakuwa mwanamtandao ndio sababu 2008 aliachana na Lowassa na 2010 akamtosa Sitta
 
Kikwete aliwatosa Lowassa na Sitta because they were a threat to his ambitions ; they were eclipsing him as far as national popularity was concerned.
Bunge under Sitta was not getting directives from the executive and Lowassa was running the government single-handedly!
Kikwete felt that his power was being threatened hence his actions against Sitta ana Lowassa!!
Hiyo haikumfanya sio mwanamtanfao!’ Moreover Sitta was replaced by another mwanamtandao Anna Makinda!!
 
Kikwete aliwatosa Lowassa ma Sitta because they were a threat to his ambitions ; they were eclipsing him as far as national popularity was concerned.
Bunge under Sitta was not getting directives from the executive and Lowassa was running the government single-handedly!
Kikwete felt that his power was being threatened hence his actions against Sitta ana Lowassa!!
Hiyo haikumfanya sio mwanamtanfao!’ Moreover Sitta was replaced by another mwanamtandao Anna Makinda!!
Kwenye mazishi ya Mkapa kule Lupaso Mzee Kikwete alielezea vizuri sana hili jambo na kwamba Nyerere alishapanga baada ya Mkapa atafuata yeye kwa sababu wote ni Vijana wake 😄😄😄🙏
 
Amani iwe nanyi wanabodi

Ukiambiwa kuhusu uwepo wa kundi hili unaweza kusema hizi ni stori za Kusadikika. Ila Ukweli ulio wazi ni kwamba hizi sio stori za kusadikika, sio series za kihindi, kituruki wala kikorea.

Ili kulifahamu kundi hili unapaswa kuufahamu mfumo wa Chama cha Mapinduzi wa kumpata mgombea wao Urais tangu wakati wa Chama Kimoja.

Kwa wasiofahamu Chama cha Mapinduzi hujulikana kama Chama dola kwa sababu ndo kilikuwa Chama pekee cha siasa nchini Tanzania miaka michache baada ya Uhuru hadi mwaka 1992 tulipoingia rasmi kwenye mfumo wa vyama vingi.

Kwa sababu hiyo vyombo vya ulinzi na usalama vilikuwa na nafasi kubwa sana kwa siasa za ndani za Chama hiki. Kwa kifupi ili uwe Mgombea Urais wa CCM ilikuwa ni lazima Idara ya Usalama ya Chama watoe taarifa ya kukusafisha na kusema unafaa kuwa Rais. Ikumbukwe Idara hii ndo baadae ilikuja kujulikana kama Kamati ya Maadili ya Chama na ni bahati mbaya Idara hii imekuwa vilevile tangu wakati wa Chama kimoja hadi sasa.

Kundi la Wanamtandao ni kundi lililoundwa baada ya Nyerere kuondoka kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi. Kundi hili liliongozwa na Makada wenye ushawishi na mizizi ya vyombo vya dola ndani ya CCM.

Kundi hili liliundwa kwa mjumuiko wa Makada mbalimbali waliokuwa Watumishi wa Idara ya Usalama, Jeshi la Wananchi, Wafanyabiashara, Wanazuoni na wengineo wengi hasa kutokana na Serikali ya Awamu ya Pili kufungua milango ya Kiuchumi na kuachana na Uchumi wa Kijamaa.

Dhumuni kuu la kuundwa kwa kundi hili ndani ya CCM ilikuwa ni kukamata Uongozi wa CCM na Taifa kwa kipindi kirefu. Kundi hili lilijipanga ku dominate siasa za nchi hii kuanzia 1995 hadi kwenye uhai wote wa Taifa la Tanzania.

Kundi hili liliandaa vijana, wataalam wa masuala ya kiuchumi na ku recruit kila waliyemuona anafaa kwa maslahi mapana ya kundi lao.

Baada ya Taarifa kumfikia Mzee Nyerere wakati wa Uchaguzi wa 1995. Mzee alitoka Butiama kurudi Dar ili kusimamia show kundi hili lisikiteke Chama. Uzuri kwa kuwa ulikuwa Uchaguzi wao wa Kwanza, Kundi hili halikufanikiwa kuchukua Uongozi wa Chama na Nchi mwaka 1995.

Kosa kubwa alilolifanya Mkapa ni kupuuzia nguvu ya Kundi hili hivyo kwa kuwa walikuwa na nguvu aliendelea kuwaacha kwenye nafasi nyeti. Walikamata Idara za Fedha za Chama kwa Rostam kuwa Mweka Hazina wa Chama, Kikwete aliendelea kuwa Waziri wa Mambo ya Nje huku akiitumia nafasi hiyo vilivyo kulijenga kundi hili ndani na nje ya nchi.

Mzee wa Vijisenti aliendelea kuwa Mwanasheria wao makini, Lowassa akiwa mwanamikakati mkuu wa ndani huku Bernad Membe akijenga vizuri mahusiano ya kundi hilo na Idara ya Usalama.

Walifanikiwa kuweka watu kwenye nafasi mbalimbali za Uongozi chini ya Mkapa na pia walifanikiwa kukwapua hela nyingi sana BOT kupitia sakata la EPA ili kujijengea ushawishi wa kifedha.

Kufikia mwaka 2005 Kundi hili lilikuwa kama Kansa ambayo imeshaila nchi nzima. Kwa kuwa Nyerere alishatangulia mbele ya Haki mwaka 1999, Mkapa hakuwa na namna akashindwa nguvu na wakachukua uongozi wa Chama na Nchi mwaka huo kwenye Uchaguzi Mkuu. Ripoti ya maadili iliyotengenezwa na Idara ya Usalama ya Chama kumkatalia Kikwete asiwe Rais ilibadilishwa mwishoni na kutengenezwa Mpya iliyomsafisha na kuchukua usukani. Inasemwa suala hili lilisababisha kifo cha aliyekuwa Mwana usalama wa Chama Mwandamizi Marehemu Balozi Daud Mwakawago.

kundi hili limeendelea kutawala siasa za Tanzania tangu mwaka huo 2005 hadi sasa ambapo kwa sehemu kubwa chini ya Mzee wa Msoga wao ndo wamekuwa wakiwa na ushawishi mkubwa zaidi katika siasa za Nchi na Chama huku wakiamua nani awe nani.

Mazuri ya Kundi la Wanamtandao;
1. Ni kundi linaloamini kwenye soko huria. Hawaamini kwenye Serikali kuhodhi Uchumi wa Nchi hivyo kufanya ustawi mzuri wa uchumi kwa nchi.

2. Pamoja na kukumaliza ukiingilia maslahi yao ila mara nyingi hawaamini sana katika kuua watu na kuwakomoa vibaya. Wanaweza hata kukupa nusu mkate ili utulie ufanye mambo yako na usiwabughuzi kwenye kula yao.

Mabaya ya Kundi la Wanamtandao;

1. Ni Mafisadi sana sana. Wana amini katika kuhodhi njia zote za kiuchumi wao tu. Hivyo kunufaika kwanza wao na vizazi vyao. Hili linasababisha nchi kutokuwa na maendeleo ya Uhakika kwa wananchi kutokana na mgawanyo usio sawa wa rasilimali za Taifa.

2. Wanapenda kuhodhi madaraka wao tu. Wana amini ili wafanikishe madili yao ni lazima washike njia zote za kufanya maamuzi. Hili linapelekea watu wenye uwezo wanaoweza kulisaidia Taifa kusonga mbele kushindwa kupata nafasi za Uongozi.

3. Wanasababisha kukua kwa kasi sana kwa kundi la Wasio nacho kwa sababu kiuhalisia Uchumi unashikiliwa na wao. Hawawazi sana kuhusu ustawi wa kundi hili la Wasio nacho.

Mada inayofuata Nitakuelezea Kundi la Sukuma Gang. Kundi lililotengenezwa Kwa Makusudi kulikabili Kundi la Mtandao au wanaojulikana sasa Msoga Gang.

Tutakuwepo!

No Reforms No Election ✊️✌️
Sio kweli kwamba CCM ndio Ilikuwa chama pekee Cha siasa baada ya uhuru na hata kabla
 
Uelewa wako wa kusoma na kuelewa, jilaumu kwa hilo. Hakuna palipoandikwa kama hivyo ulivyo eleza wewe.

Sasa sijui kama sababu ya kuifufua hii mada iliyoandikwa vizuri lilikuwa ni hilo tu la wewe kutoelewa kilichoandikwa.

Hata hivyo, umefanya vizuri sana kuuleta mbele tena mjadala huu. ambao unaonyesha mkuu 'Lord' kajitahidi sana kuupa tafakuri makini.

Sijui kama kuna historia ya namna hii popote inayoweza kuelezea mtiririko wa mabadiliko ndani ya CCM kama alivyofanya mkuu 'Lord' hapa.

Kwa hili nampongeza sana.
Ila sijui alipatwa na udhuru gani kiasi kwamba siku nyingi baada ya hapo hajaonekana tena ndani ya JF; na ile ahadi yake ya Sukuma Gang, imebaki bila kutekelezwa.
Wanaua kila wasiomtaka
Mkuu 'Erythro., unajuwa alipo 'Lord'?

Maelezo yake kuhusu "Mtandao" nayapa heshima yake.

Mtandao ulitarajiwa kusambaratika baada ya mvurugano kati ya vinara wake, Kikwete na Lowassa. Hii ponapona yake na kutufikisha hapa tulipo leo, katika hali ya kutisha kabisa, nako kunahitaji maelezo ya kujitosheleza zaidi kama haya aliyofanya 'Lord'.

Lililo wazi, ni kwamba huu 'Mtandao" wa sasa ni aidha uendelee kuwa madarakani kwa kuendelea kumwaga damu au ni shurti usambaratike kabisa kwa kufurumshwa na waTanzania wanaokataa kuvurugwa kwa taifa lao.

Binafsi sioni njia itakayowabakisha salama.
 
Hata wao wanajua wamefika kikomo
 
Soma hapo nilipowekea mishale
 
Attachments

  • Screenshot_20260719-041905.jpg
    Screenshot_20260719-041905.jpg
    234.3 KB · Views: 7
Back
Top Bottom