Nawasalimu katika jina la Jamhuri ya Tanganyika huru. Nilikuwa mapumziko ya likizo ndefu nimerejea tena jukwaani na hii ndio mada yangu ya kwanza.
Kwa sheria na kanuni za Kazi duniani kote kila mfanyakazi anastahili mapumziko ya likizo ya mwezi mmoja katika miezi 12 ya mwaka.
Hili ni takwa la kisheria ndio maana hata marais hustahili hii likizo na uma hutaarifiwa rasmi kuhusu mapumziko ya rais. Kuna baadhi ya watumishi hasa wanaopenda sana kutumia mitandao ya kijamii, hupenda kutoa taarifa kwa kila wafanyacho ikiwepo mapumzikoni likizoni.
Kama kipindi Hicho cha likizo hawajasafiri kwenda popote, kijijini ama nje ya nchi kulingana na ukwasi ni ngumu kuona mitupio na selfie za kutosha.
Lakini kama wametoka nje mbali na eneo la Kazi kuselfika na kutupia mapichapicha ni jambo lisilo epukika na kwakuwa siku hizi camera tunatembea nazo lazima ushawishike. Kuna kipindi wakati wa mapumziko ya likizo Hayati mwendazake alitupia mapichapicha akiwa kapumzika kwenye miamba na majabali.. Nadhani alikuwa anayapenda sana mawe ndio maana hata akajiita jiwe!
Likizo ni wakati wa kupumzisha mwili na akili lakini pia ni wakata wa ku 'refresh mind' kwa bata za hapa na pale.. Ni katika kipindi hiki lazima tu utashawishika kutupia matukio mitandaoni..! Hasa kwa wale addicted.
Ukiwa mapumziko ya likizo na ukajikataa kabisa kutoonekana popote hasa kama wewe ni mpenda sifa ni uthubutu wa hali ya juu mno na lazima jamii inayokujua vena ikushangae sana na kutengeneza mijadala mingi
Anaway likizo ya kisheria ni wiki nne! Zikiisha hizi hujarudi kibaruani ni aidha kati ya haya mawili
1. Kuzidisha tetesi
2. Breaking news
Bado tunahesabu siku.. Tuupe muda wakati.
Good morning Tanganyika.β€