Likizo kwa wanafunzi iwe ni lazima

Safi ulifanya VIZURI kulisimamia hili mwalimu mwenzangu.
 
ikitokea shule imefelisha wanafunzi wengi walimu wanawekwa kitimoto sasa sijui mnataka wafanye nini, na wazazi wanapenda kuwapeleka wanafunzi shule zinazofaulisha sana.
Acha tamaa mwalimu,nenda likizo kasalimie wazazi na ndugu zako,Mimi nimefundisha kwa miaka zaidi ya ishirini sijawahi kusumbuliwa kwa kuferisha,wewe uko shule gani ambayo watoto wakifeli unasumbuliwa?

Pili Umeshindwa kuendana na syllabus kwa miezi sita ijekuwa mwezi mmoja!?,wee hufai kuwa mwalimu una m
Uzembe,inabidi mamlaka zikufatilie,haiwezekani hadi juni hujaendana na Syllabus
 
Hilo halipingiki, ni miradi yao! Wanafanya hivyo wapate hela! Hata ungekuwa wewe ungefanya hivyo!
Kwa gharama ipi? Uzima na afya ya akili ya mtoto. Ikiwa mtu mzima tu anahitaji kupumzika itakuwa mtoto ambae toka asubuhi anajazwa masomo kichwani halafu unatarajia afanye hivyo mwaka mzima bila mapumziko?

Tuache kuhalalisha tamaa zetu kwa sababu za kipumbavu. Tatizo wabongo huwa tunajua magonjwa ni yale yanayoonekana tu kwa macho, kutokujua kuchoka kiakili kunaweza leta matatizo ya kisaikolojia yatakayokuwa na athari kubwa hata mbeleni.

Tulisoma enzi zetu na likizo tulikaa makwetu na mpaka leo hii tunaishi. Nini cha mno kilichoongezeka kwa sasa kiasi cha kuhitaji mtoto asipumzike?
 
Hayupo mwalimu wa kupoteza muda wake wakati wa likizo eti kisa anitolea kufaulisha watoto nimefundusha kwa sasa Nina shule 10 sijawahi kuona hii kitu tofauti na walimu kuwachangisha watoto pesa .

Kiufupi ufundishaji wakati wa likizo ni miradi ya walimu kupiga pesa ,sasa kichaka kimewaka moto,tafuteni kichaka kingine nyie walimu wa aina hii.

Jifunzeni kuwa na miradi yenu ili likizo kama hii mkasimamie miradi yenu,ualimu kazi nzuri sana isipikuwa inaharibiwa na watu wachache kama ninyi
 
Binafsi naamini kupumzika ni baada ya kufa tu! Vinginevyo maisha ni mapambano yasiyo na kupumzika Kama unavyofikiri wewe!

Shule zikifunga ufundishaji na ujifunzaji hupungua kwa asilimia kubwa si kama inavyokuwa shule zinapokuwa hazijafunga!

Ukienda mataifa yaliyoendelea wao shule zikifunga watoto huwa wapo busy kufanya project mbalimbali wanazopewa mashuleni lakini kwetu sisi ambapo ujinga ni mwingi bado tunatakiwa kupambana kuelewa yale ambayo hatukuyaelewa! Huwezi amini hii nchi kuna watu wamemaliza chuo kikuu na hawajui kusoma wala kuandika! Mfano badala ya Hakuna mtu anaandika akuna nk

Acheni watoto wasome
 
Naunga mkono hoja ni muhimu sana kupumzika. Japokuwa tufahamu tu kwamba ufundishaji wakati wa likizo haujaanza leo ni wa siku nyingi.

Miaka ya nyuma wanafunzi wa boarding kwa shule za serikali, (hasa kwa madarasa ya mtihani )walijitolea kubaki shuleni ili kijisomea wakati wa likizo. Na wwngine walisoma tuition wakiwa huko huko likizoni (nyumbani)
Ni makibaliano tu.
Siasa zisiwe nyingi tutapotezana
 
Huu ndio ukweli,wanafunzi wapumzike,darasa la 4,darasa la 6,darasa la 7,form 2 na form 4.
 
Wanafunzi kutopata muda wa likiizo ni matokeo ya mfumo wa elimu.
Ni dhahiri kwa mwaliku anayejaribu kufundisha kwa kuwaelewesha wanafunzi , hawezi kumaliza syllabus kwa muda muafaka ndio maana wanafunzi wanalazimishwa kukaa mashuleni ili waalimu wapate muda wa kumaliza topics.
Suluhisho ni specialization ianzie hata shule za msingi ili wanafunzi wawe na masomo machache ambayo watasoma kwa kuelewa sio kukariri
 
Tatizo tumewakabishi wafanyabiashara kuwa watunga sera.

Hapa swala ni kutafuta pesa na kusomesha watoto international schools.

Mawaziri wao husomesha International Schools, hawapati hizo kero
 
Elimu ni maisha!
Wewe umenena kisomi! Hata mimi nilishauri tuboreshe kwanza mazingira ndipo tupige stop tuition wakati wa likizo
 
Tutafute namna ya kufaulisha ...lkn tusiwanyime watoto likizo.
Hapo ndioo tatizo likipo! Tanzania ni moja ya nchi ambazo wanafunzi wana ufaulu wa juu sana lakini implementation ya hiyo elimu ni zero.
Wanazunzi wasome topics chache na waelewe ili wanachosoma waweze kukitumia kwa kufanya uvumbuzi kama huko first world.
 
Hapana Mkuu hao ni watoto wetu! Kama ungejua kazi ya ualimu haina maslahi ungesomea kazi nyingine au kufanya kazi nyingine yenye maslahi.
Wazazi siyo shamba lenu la kuokoteza hela,ujue hata sisi tunaitafuata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…