Tukiingia vitani nitavaa kombati na kwenda mstari wa mbele, sio kwasababu napenda vita la hasha, sio kwasababu ninamuunga mkono Mr dhaifu hata kidogo, sio kwasababu ninawachukia wanyaranda hapana ila kwasababu naipenda Tanzania.
Moja Tayari tutakuwa na vita ngumu sana kwani Kagame amesha-mpbilize Kenya na Rwanda sijui Burundi wako upande gani, na ukweli tatizo sio kauli ya Jk kuhusu waasi, utakuwa ni mpango wa Muda mrefu wa maadui zetu.
Kwa sasa naomba kila Mtanzania tuwe wamoja, acheni siasa na acheni mzaha, vita inahusu nchi na haihusu mtu, wakiweza kutuchapa atakayeathirka ni sisi. Usalama wa Taifa jamii uanze mara moja, kila mgeni ambaye hujui katokea wapi mripoti mara moja kitua cha polisi, bila kujali ni Mkenya, Mganda, Mnyarwanda au Mrundi. Kagame atawaingiza kwa kutumia njia mbali mbali. Kipindi cha kupima uzalendo na uzawa ni wakati wa vita.
Wamesema mengi na wanafanya mengi. I hate this. Walituchezea mchanga 1977 tukaachwa mbaya, na sasa wanataka tena kutuchezea cheusi chekundu.
Mwisho busara na uwezo wote utumike kuepusha vita , iwe ni suluhisho la mwisho, ila tusisubiri kutiwa vidole vya macho. Tayari nimeanza kufua kombati zangu na buti. Haya kama inabidi tuanze mapema kuchangia chakula na maji ya wanajeshi wetu tuambiwe mapema, tujiandae vizuri. Hatuji aadui ni wangapi ila tunao wengi, hasa mabebru wanaotaka gesi na madini.