Lile fupa lililowashinda marais wanaume 4, rais mwanamke 1 aligegeda kama mlenda!. Miswada 3 ya ukombozi mpya wa taifa letu yatua bungeni asubuhi hii

P, umeanza Uswahili lini ?je atalikojoza lini?
 
Uchawa wote huu ndugu yangu,lakini hawakupi hata uDC
 
Kufanikiwa kwa hili na likapita, basi tuanze kukusanya maua ya kumpatia mama Samia.

Lakini suala la Kura halihusiani na mauaπŸ˜ƒ
 
Furaha ya kila mtanzania ni kuona mapungufu yaliyopo yanaondolewa, sasa hatuwezi kushangilia kama Paskal kama hatujaona content
 
Kama CCM wasingemtisha mzee Kikwete dakika za mwisho, leo hii tungeshakuwa na Katiba bora kabisa ambayo imeshirikisha watanzania wote.

Ni kwanzo mzuri kwake kwenye suala hili kama kweli sheria hizo zina nia njema kwa Taifa letu.
Sasa aliye mtisha kasha fariki na kabla ya kufa eti kaandika kitabu cha kuomba msamaha watanzania dah!! Hii nchi ni tabu tupu
 
Kabla hujaona kontenti tayari unashangilia?
 
yaani ushabiki wa kisiasa wa namna hii nchi za watu wenye akili huwezi kuukuta kabisa, kwasababu ni unafiki fulani hivi, hivi nchi hii itakombolewa kwa ushabiki as if sisi wote ni watoto hapa nchini? paschal hivi huwa unakuwa na shida gani mbona huwa hueleweki wakati tunaamini shule ulienda?
 
Samia amewashinda hao wengine maswala mengi tuu ya msingi kuanzia swala la Ngorongoro Hadi maswala ya uchumi na Demokrasia.

Binafsi Huwa napenda zaidi maswala ya uchumi.Kwa miaka 3 ya Samia tunazungumzia Bajeti ya kutoka Trilioni 30, 2020/2021 Hadi Trilioni 47, 2024/2025 Ongezeko la Trilioni 17 ndani ya miaka 3.

Samia sio wa level za Tanzania na watu dizaini yake Huwa wanapatikana mara chache sana Duniani.
 
Hayo bajeti imesaidia nini nchi zaidi ya umeme kukatika kila siku na madawa hospitalini hakuna.
 
Hayo bajeti imesaidia nini nchi zaidi ya umeme kukatika kila siku na madawa hospitalini hakuna.
Unauliza imesaidia nini? πŸ˜‚πŸ˜‚ Unaishi Ulaya au?

Kwani hujui kwamba next year bwawa la umeme linaanza Kuzalisha umeme?

Kwani hujui kwamba Vipande vyote vya SGR vina wakandarasi? Ameweka wakandarasi 5 na aliwakuta 3 tuu.

Kwani hujui kwamba Tanzania ndio Nchi pekee yenye miradi Mingi mikubwa SubSahara Afrika?

Kiufupi nikitaka kutaja Kila kitu humu tutajaza seva.Sekta zoooote za Uchumi zinakimbia sana na Kuna miradi mikubwa asikwambie mtu.

Itoshe kwako kusoma namba hizi hapa πŸ‘‡

View: https://twitter.com/BusInsiderSSA/status/1722603308429508863?t=Me6WKLHxoYSMmROW9He_6A&s=19
 
Pascal, nashauri tusianze kutoa maua mapema, kuwa na sheria nzuri za uchaguzi ni kitu kingine na utekelezaji wa sheria hizo ni kitu kingine. Hapo kwenye utekelezaji ndipo kimbembe kilipo.
 
Unawahi kununua nepi kisa mkeo na ujauzito wa mwezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…