Haya mambo mawili(mojawapo)huenda ndio ambayo Mama leo atayaweka hadharani japo yote mawili yatafanywa kwa njia ya kuzuga tu.
Mchakato wa katiba mpya hata ukianza upya utakuwa ni wa kutaka kutuliza shinikizo lililopo na kuwatuliza wanaotupa misaada but they wil never be serious.
Kingine ni uwezekano wa kutangaza adhima yake ya kushirikisha wapinzani feki kwenye serikali ya mseto katika wakati watakaokuwa wameupanga ikiwa ni pamoja na kufanya mabadiliko ya katiba kuruhusu uundwaji wa serikali ya mseto na wanafuika watakuwa ni ACT na vyama vingine vidogo vidogo.
Haya hata kama hayatangazwa leo hii, ila mjue yako njiani na siku yoyote yatatangazwa rasimi kwanini ni mahitaji ya wakati, na kwa mazingira tuliyonayo, hayakwepeki, hivyo ni swala la muda tu.
Watalazimika kutekeleza mojawapo ya mambo hayo mawili hata kama hawapendi kama walivyolazimika kukubali kuanzisha kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.