Hakuna nilipokazania suala la kunyongwa au kumponda awaye yote aliyeridhia watu kunyongwa kwa mujibu wa sheria.
Sina tatizo na Mzee Mwinyi kama binadamu ila Nina tatizo na wewe kutaka kumpaka rangi kupitiliza kuwa ni mwingi wa huruma kuliko wengine.
Kwenye upaka rangi wako:
1. Ulipotosha kwa kudai kulihifadhi jina la mchora mapicha kuwa alidakwa na wana usalama ila Mwinyi kwa wingi wa huruma akawataka kumwachia. Wakati ukijua ni uongo taslimu.
2. Umeendelea mbele tena hapa kuonyesha kuwa kuchora mapicha ya matusi ambako nakubaliana nawe kuwa hakukubaliki Mwinyi pia hakukuvumilia.
3. Kulinganisha hoja zako kwenye #1 na #2 hapo haijulikani Mfano wako wa kumpembejea Mwinyi kupitiliza hivi kwenye kadhia hiyo ulikuwa una maana wapi.
4. Mifano ya unyongaji niliyokupa ilikuwa kukuitisha kupunguza mzuka na mtu kwa jina huruma.
Naendelea kukumbusha msingi wa hoja ni uthubutu wa kuhoji huondoa miungu watu na kuimarisha taifa na huo Nyerere hajuchoka kuusemea.
Wewe ndio wale wanaonyooshea watu kidole kimoja huku vinne vikimwangalia mnyooshaji.
Unasema kuwa mimi nampaka rangi Mwinyi kupitiliza, lkn unajifanya hauoni kuwa na ww unampa Nyerere sifa ambazo hazimstahili.
Unapozungumzia swala la uhuru wa kutoa hoja na uthubutu wa kuhoja, Nyerere hutakiwi kumuweka kama kioo cha misingi hiyo maana katika utawala wake alipingana nayo. Nimekutolea mifano iliyo hai na kuna wadau mbali mbali waliokuwepo kipindi cha Nyerere wamekufahamisha humu kupitia uzi huu, lkn kama hiyo haitoshi nikakukumbusha kuwa hata Lisu mwenyewe aliwahi kuongelea kuhusu jinsi Nyerere alivyoendesha nchi ki propaganda propaganda (uongo uongo) ili aje kusifiwa hata kwa yale ambayo hakustahili kusifiwa (kama hivi unavyofanya).
Fikiria mtu aliefuta vyama vyama vya upinzani, lkn kama hiyo haitoshi akaanza kupambana hata na wale waliojaribu kutoa mawazo yao mbadala tena bila kuvunja sheria.
Nyerere aliingiza nchi katika sera za kijamaa huku akiona kabisa misingi ya sera hiyo ilikuwa inaliangamiza taifa letu, na ukizingatia nchi yetu ilikuwa bado changa kwa kuiingiza katika sera hizo.
Watu walioona mbali kuhusu athari za sera hiyo walijaribu kumshauri, lkn matokeo yake waliishiwa kukebehiwa, kudharauliwa, kupuuzwa na wengine kupewa kesi zisizokuwa na kichwa wala miguu ili yey apate nafasi ya kufanya kile alichofikiri kufanya mwenyewe.
Na usifikiri hakuna waandishi pia ambao walikuwa wanajua athari zile za sera na siasa zake za kijamaa, lkn hakuna hata mmoja kati yao aliekuwa na uwezo wa kuthubutu kuandika chochote kutoa maoni yake kama jinsi watu walivyoanza kuruhusiwa kutoa maoni yao chini ya serikali ya mzee Mwinyi na hadi leo utaratibu huo wa kutoa mawazo umekuwa ukiendelea nk. Nyerere aliwezana na watu kama kina mzee Kawawa ambae yeye siku zote alikuwa mzee wa 'NDIO' hakuwai kuwaza kumpinga Nyerere kwa lolote wala chochote.
Jiulize... Je Lisu aliongea maneno yale kwa vile alimchukia Nyerere, au aliongea kwa vile alitaka watu waone jinsi mzee alivyoiendesha nchi kwa mkono wa chuma, tofauti na jinsi watu wamekuwa wakiaminishwa kupitia propaganda mbali mbali kwamba Nyerere alioongoza nchi hii kwa misingi ya kweli na uhuru.
Jiulize hivi kati ya wewe na Lisu ni nani aliemuelewa Nyerere vizuri?
Ni nani alieonja joto la jiwe la uongozi wake?
Ukiona mtu aina ya Tundu Lisu kaja kuzungumzia mabaya ya baba wa taifa hadharani tena aliefariki zaidi ya miaka 15 iliyopita, basi unatakiwa uyatafakari sana yale yaliosemwa dhidi yake, maana Tundu asingekurupuka tu bila kuwa na fact ya kile anachokisema.
Nyerere alipata uthubutu wa kuongea baada ya kutoka madarakani, na vilevile baada ya kuona raisi aliepo hakuwa mtu wa kupambana na wanaomsema, wanaomshauri au wanaompinga.
Ingekuwa Mwinyi ana akili kama za yule kichaa aliemfunga Kaunda kule Zambia, basi Nyerere angenyuti pembeni kusikilizia kama walivyosikilizia wengine wakati wa utawala wake.
Ila alipogundua kuwa Mwinyi ni raisi mwenye sera na misimamo tofauti na ya kwake, ndo na yeye akapata moral wa kukosoa kosoa hata pale ambapo hapakustahili kukosolewa.
Narudia tena Nyerere ni baba wa taifa letu, na mengi tu mazuri ameyafanya kwenye nchi yetu.
Lakini sifa ya kuheshimu maoni ya watu, kuheshimu uhuru wa kutoa mawazo, maoni nk hakuwa nayo.
Hiyo sifa muasisi ni Mwinyi na wengine waliofatia wakairithi.