Kwa ufahamisho tu, ni wakati wa Mwinyi ndipo hadhi ya Tanzania kama taifa la kutolea mfano ilipoanza kushuka kwa kasi ya kutisha. Yawezekana unasumbuliwa na umri lakini hata ikulu yenyewe ilishuka hadhi ikawa kama sebule ya mashemeji na walanguzi
Ni katika wakati huo elimu haikupewa kipaumbele na ikawa kama si chochote si lolote mradi uwe na hela. Uongozi wa Mwinyi uliitwa majina mengi na hata yeye binafsi aliitwa mzee yupo yupo kila kitu kikawa rukhsa na ndio wakati ulanguzi ulipoota mizizi na kukomaa!
Ni wakati huo hadi pesa za waliokuwa wastaafu wa jumuiya ya Afrika Mashariki zilipokabidhiwa kwa serikali ili iwafikishie walengwa kuangukia mikononi mwa walafi. Wengi wa hao wastaafu walikufa wakililia mafao ambayo inadaiwa yalitumika kununulia nyumba huko ng'ambo.
Kama tunataka kutoa mifano ya viongozi walioishusha hadhi ya taifa letu, muasisi wake ni Ali Hassan Mwinyi. Hadi vivutio vya viwanja vya Ikulu kama tausi waliopendeza kukivinjari ndani ya viwanja hivyo walivyotoweka kiajabu ajabu na hadi leo haijulikani walipelekwa wapi.
Baada ya Mwinyi, uongozi wa taifa letu haukuwa tena kwa wenye sifa na uwezo, mtu yeyote yule aliyeutaka alijiona anaweza. Hali hiyo ya kushuka kwa sifa na uwezo wa kuiongoza Tanzania imeendelea hadi leo na ukishateuliwa na CCM, wewe ni Rais tu inyeshe isinyeshe!
Sikulaumu sana kwa vile najua yote uliyoandika hapa ulihadithiwa, na aliekuhadithia aliamua kukuhadithia hivi kwa sababu zake maalum.
Alijua kwamba wewe hauna ujanja wala uwezo wa kutambua michanga anayokulisha. Siku zote mtu anapotaka kudanganya huwa anaangalia target ya yule anaetaka kumdanganya, so akiona anaetaka kudanganywa amekaa kihasara hasara bila kuonesha maarifa ya kutaka kuutafuta ukweli, basi mdanganyaji ndo huanza sasa kumwaga uongo wake na kutimiza malengo yake. Ila akiona mtu anaetaka kumdanganya yuko makini kuzuia uongo wowote basi mdanganyaji huamua kuacha kudanganya ili kukwepa aibu.
So mpaka hapo inaonesha dhahiri kuwa umemezeshwa matango pori tena yaliojaa miba. Na ujanja wa kuyacheuwa hauna. Anyway ngoja nikupe somo hapo chini.
Unasema wakati wa Mwinyi ndio ikulu ilianza kushuka thamani. Je unaweza kuweka kithibitisho chenye kuthibitisha kuwa ikulu ilikosa thamani?
Inamaana ndugu, au watu kutembelea ikulu ndo kukosa thaman!!!
Ni watu wangapi mpaka wasanii, wanamichezo nk wamekuwa wakitembelea ikulu ya white house, je kutembelewa huko kumeishusha thaman kiasi gani ikulu yao?
Inamaana ikulu ni peponi au mbinguni ambapo hapatakiwi mtu wa kawaida kutembelea mpaka wale watu wa Mungu peke yao.
Kuhusu elimu naomba uniletee fact (na sio maneno matupu) zinazoonesha kuwa wakati wa utawala wa Nyerere alimu ilipewa kipaumbele na wakati wa Mwinyi haikupewa kipaumbele.
Kuhusu majina ndo kama nilivyoandika hapo juu kwamba Mwinyi aliamini katika demokrasia na uhuru wa kutoa mawazo, ndo maana kila mtu alikuwa huru kumwita jina alilotaka, kitu ambacho kwa Nyerere ingekuwa hatari kubwa kwa waitaji wa majina hayo.
Hivi wewe haujui kama Mwinyi alipoingia aliikuta nchi iko uchi kutokana na hali mbaya ya uchumi aliouacha Nyerere. Ikiwa walimu, manesi, madokta, polisi, jeshi na watumishi wengine wa serikali ilikuwa ngumu kuwalipa mishahara kutokana na hali mbaya ya uchumi, sasa hizo hela za waastafu unazosema zingetoka wapi?
Unaposema wizi na ufisadi ulianza wakati wa Mwinyi hapo ndo nipogundua kwamba wewe umehadithiwa wala haukuwepo wakati wa Mwinyi. Sisi tuliokuwepo tunafahamu jinsi Mwinyi alipoingia tu ikulu alianza na oparation ya fagio la chuma ili kurudisha pesa zilizokuwa zimeibwa na kukwapuliwa wakati wa utawala wa Nyerere. kuna msemo unaosema kifo cha wengi harusi kwahiyo wakati watu walipokuwa wanaumia na kuteseka wakati wa uongozi wa Nyerere, kuna wajanja wachache waliokuwa wananeemeka kupitia hali hiyo. Mfano kipindi hicho kulikuwa hakuna bidhaa nzuri madukani, hakuna chakula kizuri madukani, hakuna mafuta, sukari nk. Watu tulikuwa tunalishwa unga wa yanga, sabuni za kutengenezwa na mise ya michikichi. Ila viongozi wa serikali walikuwa wanakula vizuri na baadae walikuwa wanakusanya vyakula hivyo na kwenda kuviuza kwa watu wenye pesa kimya kimya. Na kwa vile kipindi hicho kulikuwa hamna maduka basi ilikuwa rahisi watu wenye pesa kununua vitu hivyo kupitia baadhi ya viongozi hao wa serikali.
Kifupi toka tulipopata uhuru hakuna awamu ambayo ilipita bila ufisadi na wizi wa fedha za serikali. Kasome historia za kina mzee Mtei wakati wapo serikalini pamoja na magava wengine waliofanyakazi chini ya serikali ya Nyerere.
Nyerere ni baba wa taifa, alijenga misingi bora ya umoja na mshikamano, alitokomeza ukabila, ukanda nk, lkn ndio raisi alieondoka madarakani akiiacha nchi ikiwa uchi kiuchumi, huku wananchi wakiwa maskini wa kutupwa, 90% ya wananchi wakiwa hawana uwezo hata wa kula milo miwili au mmoja kwa siku. Watu walichakaa wasijue wapi watapata angalau mafuta ya kula ya kupaka mwilini, watu walikauka midomo kwa kukosa maji, walikonda na hata kuumwa vidonda vya tumbo kwa kukosa chakula maana unakuta familia ya mume, mke na watoto 4 inapokea kilo 2 tu ya unga wa yanga kwa ajili ya ugali, kilo 2 ya mchele tena mdundiko, mafuta lita 1, sukari kilo 1 afu wanaambiwa watumie week nzima ndo gari kitapita tena.
Mwinyi alipoingia aliondoa mateso yote watu wakawa wanapata huduma inavyostahili, waandishi wa habari wakaruhusiwa kuandika chochote wanachojisikia kitu ambacho kwa Nyerere ilikuwa ngumu kwa muandishi kuandika kitu kibaya against government yani mwandishi unatakiwa uandike habari za kumsifu baba wa taifa na serikali yake tu. Na ndio maana wengi hamkujua ukweli kuhusu uozo uliyokuwa ndani ya serikali yake. Mwinyi aliruhusu kukosolewa na waliokosoa hawakuuwawa, hawakukimbia nchi, hawakuteswa, hawakufungwa wala kufukuzwa chama, ila kwa wale waliothubutu kumkosoa Nyerere wengi wao hatunao tena, wengine mpaka leo wapo nje ya nchi na uraia walibadilisha kitambo sana.
Nakuonea huruma kwa kulishwa matango pori tena ukute umelishwa na mtu wa kijijini asiejua lolote wala chochote.