Nyerere alifuta vipi vyama vya upinzani wakati ni 👉 yeye ndie aliruhusu vianze kuwepo'| licha ya kupingwa na wengi kwenye chama chake?
Usichanganye Nyerere kuvifuta vyama vya upinzani wakati wa kupigania Uhuru na baada ya hapo, wakati wa kupigania Uhuru ilikuwa ni vyema kwake kufanya alivyofanya ili kuwaunganisha watanzania kwa muda mfupi, wawe na lengo moja, ili kufikia matarajio waliyojiwekea.
Kuruhusu vyama vya upinzani kabla ya uhuru kungekuwa ni kuvurugana wenyewe kwa wenyewe hapa ndani, hivyo mkoloni angetumia mvurugano wetu kuendelea kututawala kirahisi, mimi niko na Nyerere kwenye hilo.
Nyerere aliruhusu au alishauri viruhusiwe?
Tena walioshauri ni wengi sio Nyerere peke yake.
Yani raisi wa nchi awe Mwinyi afu ruhusa atoe Nyerere?
Unataka kutuambia kwamba Nyerere alikuwa na cheo cha ayatollah Khomen wa Iran ambae maamuzi yake ndio ya mwisho mbele ya raisi?
Kama alikuwa na cheo cha ayatollah mbona alishindwa kutumia cheo hicho kurudisha azimio la Arusha na badala yake akawa analalamika tu kwenye vyombo vya habari kama tunavyoweza kulalamika mimi na wewe hapa JF bila kuwa na uwezo wa kumfanya lolote tunaemlalamikia?
Kama alikuwa na cheo hicho mbona alishindwa kumzuia Kambona na wengine waliokimbia utawala wake wasirudi nchini kama alivyowazuia kabla hajatoka kwenye uraisi?
Mbona alishindwa kuzuia mfumo wa biashara huria aliokuwa anaupinga wakati na kuukataza enzi za utawala wake na badala yake akawa analalamika tu kwenye vyombo vya habari kama kawaida yake?
Ukweli ni kwamba watu wengi (sio wote) wamekuwa wakipindisha ukweli wa baadhi ya mambo kwa lengo la kumpa sifa mtu ambae sifa hizo hazimstahili ili yule ambae zinamstahili aonekane hakuna la maana lolote alilofanya au analofanya.
Ni kawaida kukuta watu hao wakichukua mazuri ya Mwinyi kumpa Nyerere au Mkapa, na kuchukua baadhi ya mabaya ya hao niliwataja kumpa Mwinyi.
Mwinyi ataendelea kuwa baba wa demokrasia ya nchi yetu maana katika utawala wake ndio watu walikuwa huru kuikosoa serikali yake na yeye mwenyewe bila mkosoaji yeyote kufungwa, kukimbia nchi, kufukuzwa chama, kuuwawa nk.
Nyerere angekuwa anapenda demokrasia asingewahenyesha waliokuwa wanampinga.
Angewasikiliza na kuwavumilia.
Mengine ni propaganda tu kama zilivyo propaganda zingine.
By the way namheshimu Nyerere kama baba wa taifa letu, alieleta umoja na mshikamano kati yetu, alietokomeza ukabila na ukanda, aliepiga vita ukoloni kupitia nchi zilizopata uhuru baada yetu.
Nndio maana avatar yangu inaongozwa na picha yake kitambo sana.