Lililokuwa taifa la kupigiwa Mfano halipo tena

Lililokuwa taifa la kupigiwa Mfano halipo tena

Kila nabii na kitabu chake. Ukitaka kujua namaanisha nini kuhusu msemo huo, basi muulize Oscar Kambona, bibi Titi Mohammed na viongozi wengine walioonja joto la jiwe la mwl Nyerere. Kidogo uniambie Mwinyi ndo hakutumia nguvu kubwa kuwaadhibu waliompinga.

Kuna kijana (jina simtaji) huko chuo kikuu fulan aliwahi kumchora raisi Mwinyi picha ya kudhalilisha, kijana akashukiwa na wanausalama ili wakamuadabishe, lkn Mwinyi akawapigia sim fasta wana usalama na kuamrisha wamuachie kijana huyo haraka iwezekanavyo aendelee na masomo yake bila kujali matusi na kejeli zake alizozionesha kwake, kwa familia yake na nafasi yake kama raisi wa nchi.

Huyu kijana angefanya hivyo enzi za Nyerere pengine leo tusingekuwa nae tena.
Kwa ufahamisho tu, ni wakati wa Mwinyi ndipo hadhi ya Tanzania kama taifa la kutolea mfano ilipoanza kushuka kwa kasi ya kutisha. Yawezekana unasumbuliwa na umri lakini hata ikulu yenyewe ilishuka hadhi ikawa kama sebule ya mashemeji na walanguzi

Ni katika wakati huo elimu haikupewa kipaumbele na ikawa kama si chochote si lolote mradi uwe na hela. Uongozi wa Mwinyi uliitwa majina mengi na hata yeye binafsi aliitwa mzee yupo yupo kila kitu kikawa rukhsa na ndio wakati ulanguzi ulipoota mizizi na kukomaa!

Ni wakati huo hadi pesa za waliokuwa wastaafu wa jumuiya ya Afrika Mashariki zilipokabidhiwa kwa serikali ili iwafikishie walengwa kuangukia mikononi mwa walafi. Wengi wa hao wastaafu walikufa wakililia mafao ambayo inadaiwa yalitumika kununulia nyumba huko ng'ambo.

Kama tunataka kutoa mifano ya viongozi walioishusha hadhi ya taifa letu, muasisi wake ni Ali Hassan Mwinyi. Hadi vivutio vya viwanja vya Ikulu kama tausi waliopendeza kukivinjari ndani ya viwanja hivyo walivyotoweka kiajabu ajabu na hadi leo haijulikani walipelekwa wapi.

Baada ya Mwinyi, uongozi wa taifa letu haukuwa tena kwa wenye sifa na uwezo, mtu yeyote yule aliyeutaka alijiona anaweza. Hali hiyo ya kushuka kwa sifa na uwezo wa kuiongoza Tanzania imeendelea hadi leo na ukishateuliwa na CCM, wewe ni Rais tu inyeshe isinyeshe!
 
Matokeo yake yamekuwa watu kulia lia yanapowakuta bila kuwa na uthubutu wa kuchukua hatua. Watu wamelazimika kuwa wenye kuangalia maslahi yao binafsi yanayowagusa wao moja kwa moja. Kwa maana jitihada za kuhoji lolote zimegeuzwa kuwa ni kujichumia majanga.
Binafsi naamini mvua ilianza kutunyeshea hapa, kwenyemaoni ya hii mistari miwili.
CCM baada ya kuwa chama cha "Ukombozi na Mapinduzi" hatua iliyofuata baada ya Mwalimu Nyerere kung'atuka ikawa ni chama cha kujijenga viongozi walioshika madaraka na kuanzisha msemo wa "huyu ni mwenzetu", hata kama uwenzetu huo ni wa kuvuruga maslahi ya nchi.

Hali hii yote uliyoielezea katika andiko la mada ni matokeo ya mambo yaliyosimamiwa na chama cha CCM. Kama mwananchi unataka kuwa kiongozi wa ngazi yoyote, ni lazima uweke akili zako pembeni (kama unazo akili), na badala yake uongozwe na zile zinazokubaliwa na chama, kama unataka kufanikiwa kuwa kiongozi.

Na inakupasa ujuwe kwamba muundo wa CCM umetapakaa kote, nchini toka kwenye shina huko mtaani wanakoishi wananchi wa kawaida. Kwa hali hiyo, CCM imeweza kuwalaza akili wananchi kama ulivyosema, na kuwa kama makondoo yanayofuata tu kila kinachosemwa na viongozi wa CCM na serikali yao.

Hali hii inawanufaisha sana CCM, ndiyo maana wanapigana juu chini kuhakikisha kwamba hali hii ya ukondoo haiwatoki wananchi.
 
Walio thubutu kumhoji Nyerere walifia jela au walikimbia nchi. Alitawala kidikteta yule mchonga meno.
Wewe unamfahamu kivyako, na unaweza kudai na kutupa matope yote unayotaka kupaka, lakini hilo halibadili chochote kuhusu aliyoyasimamia Mwalimu Nyerere ndani ya nchi hii.
Huwezi kuanza kuandika historia ya kutunga tu juu ya jambo lolote na watu wenye akili wakaamini tu bila kuhoji usahihi wa hayo unayoelezea.
 
Binafsi naamini mvua ilianza kutunyeshea hapa, kwenyemaoni ya hii mistari miwili.
CCM baada ya kuwa chama cha "Ukombozi na Mapinduzi" hatua iliyofuata baada ya Mwalimu Nyerere kung'atuka ikawa ni chama cha kujijenga viongozi walioshika madaraka na kuanzisha msemo wa "huyu ni mwenzetu", hata kama uwenzetu huo ni wa kuvuruga maslahi ya nchi.

Hali hii yote uliyoielezea katika andiko la mada ni matokeo ya mambo yaliyosimamiwa na chama cha CCM. Kama mwananchi unataka kuwa kiongozi wa ngazi yoyote, ni lazima uweke akili zako pembeni (kama unazo akili), na badala yake uongozwe na zile zinazokubaliwa na chama, kama unataka kufanikiwa kuwa kiongozi.

Na inakupasa ujuwe kwamba muundo wa CCM umetapakaa kote, nchini toka kwenye shina huko mtaani wanakoishi wananchi wa kawaida. Kwa hali hiyo, CCM imeweza kuwalaza akili wananchi kama ulivyosema, na kuwa kama makondoo yanayofuata tu kila kinachosemwa na viongozi wa CCM na serikali yao.

Hali hii inawanufaisha sana CCM, ndiyo maana wanapigana juu chini kuhakikisha kwamba hali hii ya ukondoo haiwatoki wananchi.
Msiisingizie CCM ila wale walioaminiwa na Mwl JKN ndiyo waliofanya usaliti...Wanachama wakawaida wameendelea kuwa waaminifu isipokuwa watu wachache ambao wamejimilikisha chama chetu
 
Msiisingizie CCM ila wale walioaminiwa na Mwl JKN ndiyo waliofanya usaliti...Wanachama wakawaida wameendelea kuwa waaminifu isipokuwa watu wachache ambao wamejimilikisha chama chetu
EEEeeeeHeeeee Heeee!

Mkuu 'Ame', mbona unanichekesha kiasi hiki mkuu wangu!

Kwanza kabisa kabla ya yote, nikubaliane moja kwa moja na wewe juu ya unafiki wa viongozi waliokuwa chini ya Mwalimu.
Hawa ndio waliokwamisha kila juhudi zilizojaribiwa wakati wa Mwalimu kwa njia mbalimbali. Na ni aina ya viongozi hao hao wanaoendelea kuishikilia CCM hadi leo, na usitegemee kuona matokeo tofauti.

Hata ukiwaita hawa kuwa "watu wachache", lakini ndio wanaoshikilia kila jambo linaloendeshwa na chama hiki.

Sasa mkuu 'Ame', hawa wanachama ambao unawaita wengi, mbona hawajitokezi na kukataa chama chao kutumiwa isivyo?
Kwa nini pasijitokeze na jasiri mmoja, wawili, au kundi dogo katika hao wengi wakasema sasa IMETOSHA! Hatutaki tena chama chetu kutumiwa visivyo.

Najuwa utaanza kuleta stori za Magufuli hapa, lakini huyo pamoja na utofauti wake kama kweli alikuwa nao, uongozi wake ulikuwa siyo wa kawaida (niseme hivyo kurahisisha mambo).
 
  • Thanks
Reactions: Ame

Mbona wamejitokeza mara nyingi? What have they gained zaidi ya kuwa branded negatively na hao ambao wame consolidate power na wealth?
 
Vyama vya siasa vilifutwa mwaka 1965, miaka minne baada ya uhuru na vilirejeshwa mwaka 1992, miaka mingi baada ya Nyerere kuondoka madarakani.
Nyerere alifuta vipi vyama vya upinzani wakati ni yeye ndie aliruhusu vianze kuwepo licha ya kupingwa na wengi kwenye chama chake?

Usichanganye Nyerere kuvifuta vyama vya upinzani wakati wa kupigania Uhuru na baada ya hapo, wakati wa kupigania Uhuru ilikuwa ni vyema kwake kufanya alivyofanya ili kuwaunganisha watanzania kwa muda mfupi, wawe na lengo moja, ili kufikia matarajio waliyojiwekea.

Kuruhusu vyama vya upinzani kabla ya uhuru kungekuwa ni kuvurugana wenyewe kwa wenyewe hapa ndani, hivyo mkoloni angetumia mvurugano wetu kuendelea kututawala kirahisi, mimi niko na Nyerere kwenye hilo.
 
Hizi ni petty issues,
Kwa mtazamo wangu vipo vitu vjngi vinavyoashiria kudumaa kwa fikra ikiwemo humu JF na hasa hili Jukwaa la Siasa.

Ukiachilia mbali hizo ban unazolalamikia mtu kupigwa bila kupewa haki ya kujieleza, japo hapa ningesisitiza watumiaji wa jukwaa wawe wanajikumbusha sheria na kanuni zinazotawala..

Lakini pia tatizo la kudumaa kifikra lina extend mpaka kwa watumiaji wa hili jukwaa.

Uwepo wa makundi yanayoshabikia vyama vya siasa ndio chanzo cha haya yote, hii imesababisha wengi toka pande tofauti kushindwa kuwa wakweli/wazi pale jambo baya linapotokea upande wao, huamua kulifumbia macho, wengi husubiri mpaka litokee upande wa pili ndio waseme.

Kwangu hili pia linasababisha kudumaza wengj kifikra, hatupati nafasi ya kujadili mambo kwa mapana yake kwa sababu ya mahaba na ushabiki kwa vyama tuvipendavyo.
 
Kwenye kuwajengea wananchi uthubutu uko chaka
Waliofia jela au kuikimbia nchi ni waliotaka kuulipua mlango bila kujali maisha ya waliokuwa ndani.

View attachment 2389895

Umuhimu wa kudai haki kwa amani kistaarabu lazima kuzingatiwa.

Nyerere aliwajengea wananchi wake uthubutu na Hilo si jambo dogo.
 
Tatizo kubwa ni ubaguzi wa kisiasa
Watanganyika wa kawaida ni watu wema wakarimu na hawana ubaguzi. Nenda popote, utake kuishi, biashara, utangaze dini, uoe au uolewe n.k utakaribishwa. Hii ni fursa kubwa sana mtu kutafuta maendeleo.
Ni kundi dogo sana lenye nguvu ya uhodhi lenye jeuri ya kulinda wanachotamani.
Wapo wanaopigania kuingia huko lakini wanakabiliana na shida ya mwenye nguvu mpishe.
Watu wa kawaida ni wengi sana, wana meno lakini wanaogopa kung'ata sababu kuna mishale imelengwa.
Tanzania kwetu pazuri.
 
Wakati wa Nyerere msimamo ulikuwa huu:

View attachment 2389885

Mengi ya ukiukaji haki ya leo yasingekuwa na nafasi.

Kwa msimamo huu madaraka yalikuwa Kwa watu. Walinzi was maslahi yao walikuwa watu wenyewe.

Msome Nyerere kumwelewa, mwana halisi was nchi hili. Wametuulia uthubutu was kuhoji tumekuwa kama mifugo ya mtu.
inawezekana umezaliwa baada ya nyerere na unasimuliwa tu kuwa alikuwa mwema sana, uliza watu wazima na wazee wawe wakweli wakwambie maisha yalivyokuwa. Umezaliwa umekuta watu wanakunywa chai, sukari inauzwa madukani, magazeti yapo siyo yale ya ccm tu, vyama vya siasa vipo, unaweza hata ukahoji jambo lolote juu ya sheria na katiba, ukamhoji mbunge, dc, waziri, rc hata rpc....hata ukaandika kuhoji utendaji wa rais.....kisha unaona mazingira ya sasa ni mabaya?

Acha masikhara mtoto
tunaheshimu tu mila zetu kwamba marehemu husemwa kwa mema tu, ukichanganya na unafiki wa watanzania basi inakuwa balaa. lakini tukisema ukweli, maisha ya wakati wa nyerere yakirudiwa hata nusu au robo tu miaka ya leo, nchi italipuka vibaya sana
 
Wengine tunawanyooshea vidole walioliuwa taifa kwa ubinafsi wao.

Leo hii hata ubakaji na ulawiti wa watoto unaousikia kwetu, ni matokeo ya kufa kwa uthubutu wa kuhoji.

View attachment 2390120

Tambua kwa msimamo huu wa Nyerere wenye nchi ni wananchi. Nani atalialia? Nani atakuwa Mungu mtu?

Zingatia mada mjomba kujipambanua unaishi zama zipi.
Sawa
 
Kwenye kuwajengea wananchi uthubutu uko chaka
TYL ya Nyerere ilikuwa na kina Ulimwengu na kina Kikwette. Uvccm Leo Ina kina johnthebaptist. Wengine humo ni kina nyie msioona hata umuhimu wa kuanza na: "kwa maoni yangu ...."

Nyie ni kutiririka tu kama vile mmetoka kuongea na Mungu.
 
Tanzania ya enzi za Nyerere ikiheshimika kila pembe ya dunia haipo tena. Tanzania hiyo ilikuwa na misimamo yake iliyojulikana na isiyotetereka.

Uhuru wa Tanzania hiyo haukuwa na maana yoyote bila Afrika yote kuwa huru. Uhuru wa Tanzania hiyo haukuwa na maana yoyote kama kulikuwa na ukiukwaji haki popote duniani Ukweli huo ulifahamika hivyo na kila rafiki na hata kila adui.

Kama taifa tulikuwa wamoja na nchi ilikuwa yetu sote. Nguvu ya hoja ilitamalaki na uthubutu wa kuhoji ulisisitizwa katika nyanja zote kutokea shule za misingi.

Leo baadhi ya watu kwa nafasi na ubinafsi wao wametumia nguvu kuuuwa uthubutu wa kuhoji. Yote hiyo ikiwa kwa nia ya kujimilikisha nchi wao na familia zao. Wasijue kuwa nchi wanaiuwa pia

Leo hatushindani kwa hoja. Hoja hazijibiwi kwa hoja, bali kejeli au kwa marungu. Watu wenye hoja tofauti wanatakiwa kuufyata. Tumelazimishwa kuwa taifa la makondoo.

Matokeo yake yamekuwa watu kulia lia yanapowakuta bila kuwa na uthubutu wa kuchukua hatua. Watu wamelazimika kuwa wenye kuangalia maslahi yao binafsi yanayowagusa wao moja kwa moja. Kwa maana jitihada za kuhoji lolote zimegeuzwa kuwa ni kujichumia majanga.

Uwezo wa kujenga, kutetea au kupinga hoja haupo tena. Utanzania wetu tuliojulikana nao umeparaganyika. Kila mtu imekuwa yupo yupo tu. Leo bila aibu tunajinasibu kama mashabiki wa Man U au Arsenal.

Ni muhimu kwa Kila mmoja kujihoji amefanya nini kuifikisha hii nchi hapa.

Anasema Prof Shivji:

“Pasipo mijadala au ubunifu huwezi kuendeleza fikra, na hii inakwenda moja kwa moja kuathiri usomaji na ufundishaji.”

Kwanini kuwaziba watu midomo? Kwanini hoja kupigwa marungu? Kwanini kuitana majina? Kwanini kujikita kupambana na mleta hoja badala ya kupambana na hoja? Nk, nk.

Kwanini JF hupiga wajumbe ban, kufuta au kufunga nyuzi bila kutoa sababu zikajulikana hadharani?

"Kwanini," huhitaji majibu si marungu.
🤔🤔🤔🤔
 
inawezekana umezaliwa baada ya nyerere na unasimuliwa tu kuwa alikuwa mwema sana, uliza watu wazima na wazee wawe wakweli wakwambie maisha yalivyokuwa. Umezaliwa umekuta watu wanakunywa chai, sukari inauzwa madukani, magazeti yapo siyo yale ya ccm tu, vyama vya siasa vipo, unaweza hata ukahoji jambo lolote juu ya sheria na katiba, ukamhoji mbunge, dc, waziri, rc hata rpc....hata ukaandika kuhoji utendaji wa rais.....kisha unaona mazingira ya sasa ni mabaya?

Acha masikhara mtoto
tunaheshimu tu mila zetu kwamba marehemu husemwa kwa mema tu, ukichanganya na unafiki wa watanzania basi inakuwa balaa. lakini tukisema ukweli, maisha ya wakati wa nyerere yakirudiwa hata nusu au robo tu miaka ya leo, nchi italipuka vibaya sana

Umeandika maneno matupu yasiweza kuvunja mfupa. Jikite kwenye Imani hii utwambie palipo na tatizo:

IMG_20221017_103027_006.jpg
 
Kwa ufahamisho tu, ni wakati wa Mwinyi ndipo hadhi ya Tanzania kama taifa la kutolea mfano ilipoanza kushuka kwa kasi ya kutisha. Yawezekana unasumbuliwa na umri lakini hata ikulu yenyewe ilishuka hadhi ikawa kama sebule ya mashemeji na walanguzi

Ni katika wakati huo elimu haikupewa kipaumbele na ikawa kama si chochote si lolote mradi uwe na hela. Uongozi wa Mwinyi uliitwa majina mengi na hata yeye binafsi aliitwa mzee yupo yupo kila kitu kikawa rukhsa na ndio wakati ulanguzi ulipoota mizizi na kukomaa!

Ni wakati huo hadi pesa za waliokuwa wastaafu wa jumuiya ya Afrika Mashariki zilipokabidhiwa kwa serikali ili iwafikishie walengwa kuangukia mikononi mwa walafi. Wengi wa hao wastaafu walikufa wakililia mafao ambayo inadaiwa yalitumika kununulia nyumba huko ng'ambo.

Kama tunataka kutoa mifano ya viongozi walioishusha hadhi ya taifa letu, muasisi wake ni Ali Hassan Mwinyi. Hadi vivutio vya viwanja vya Ikulu kama tausi waliopendeza kukivinjari ndani ya viwanja hivyo walivyotoweka kiajabu ajabu na hadi leo haijulikani walipelekwa wapi.

Baada ya Mwinyi, uongozi wa taifa letu haukuwa tena kwa wenye sifa na uwezo, mtu yeyote yule aliyeutaka alijiona anaweza. Hali hiyo ya kushuka kwa sifa na uwezo wa kuiongoza Tanzania imeendelea hadi leo na ukishateuliwa na CCM, wewe ni Rais tu inyeshe isinyeshe!
Sikulaumu sana kwa vile najua yote uliyoandika hapa ulihadithiwa, na aliekuhadithia aliamua kukuhadithia hivi kwa sababu zake maalum.

Alijua kwamba wewe hauna ujanja wala uwezo wa kutambua michanga anayokulisha. Siku zote mtu anapotaka kudanganya huwa anaangalia target ya yule anaetaka kumdanganya, so akiona anaetaka kudanganywa amekaa kihasara hasara bila kuonesha maarifa ya kutaka kuutafuta ukweli, basi mdanganyaji ndo huanza sasa kumwaga uongo wake na kutimiza malengo yake. Ila akiona mtu anaetaka kumdanganya yuko makini kuzuia uongo wowote basi mdanganyaji huamua kuacha kudanganya ili kukwepa aibu.

So mpaka hapo inaonesha dhahiri kuwa umemezeshwa matango pori tena yaliojaa miba. Na ujanja wa kuyacheuwa hauna. Anyway ngoja nikupe somo hapo chini.

Unasema wakati wa Mwinyi ndio ikulu ilianza kushuka thamani. Je unaweza kuweka kithibitisho chenye kuthibitisha kuwa ikulu ilikosa thamani?
Inamaana ndugu, au watu kutembelea ikulu ndo kukosa thaman!!!
Ni watu wangapi mpaka wasanii, wanamichezo nk wamekuwa wakitembelea ikulu ya white house, je kutembelewa huko kumeishusha thaman kiasi gani ikulu yao?
Inamaana ikulu ni peponi au mbinguni ambapo hapatakiwi mtu wa kawaida kutembelea mpaka wale watu wa Mungu peke yao.

Kuhusu elimu naomba uniletee fact (na sio maneno matupu) zinazoonesha kuwa wakati wa utawala wa Nyerere alimu ilipewa kipaumbele na wakati wa Mwinyi haikupewa kipaumbele.

Kuhusu majina ndo kama nilivyoandika hapo juu kwamba Mwinyi aliamini katika demokrasia na uhuru wa kutoa mawazo, ndo maana kila mtu alikuwa huru kumwita jina alilotaka, kitu ambacho kwa Nyerere ingekuwa hatari kubwa kwa waitaji wa majina hayo.

Hivi wewe haujui kama Mwinyi alipoingia aliikuta nchi iko uchi kutokana na hali mbaya ya uchumi aliouacha Nyerere. Ikiwa walimu, manesi, madokta, polisi, jeshi na watumishi wengine wa serikali ilikuwa ngumu kuwalipa mishahara kutokana na hali mbaya ya uchumi, sasa hizo hela za waastafu unazosema zingetoka wapi?

Unaposema wizi na ufisadi ulianza wakati wa Mwinyi hapo ndo nipogundua kwamba wewe umehadithiwa wala haukuwepo wakati wa Mwinyi. Sisi tuliokuwepo tunafahamu jinsi Mwinyi alipoingia tu ikulu alianza na oparation ya fagio la chuma ili kurudisha pesa zilizokuwa zimeibwa na kukwapuliwa wakati wa utawala wa Nyerere. kuna msemo unaosema kifo cha wengi harusi kwahiyo wakati watu walipokuwa wanaumia na kuteseka wakati wa uongozi wa Nyerere, kuna wajanja wachache waliokuwa wananeemeka kupitia hali hiyo. Mfano kipindi hicho kulikuwa hakuna bidhaa nzuri madukani, hakuna chakula kizuri madukani, hakuna mafuta, sukari nk. Watu tulikuwa tunalishwa unga wa yanga, sabuni za kutengenezwa na mise ya michikichi. Ila viongozi wa serikali walikuwa wanakula vizuri na baadae walikuwa wanakusanya vyakula hivyo na kwenda kuviuza kwa watu wenye pesa kimya kimya. Na kwa vile kipindi hicho kulikuwa hamna maduka basi ilikuwa rahisi watu wenye pesa kununua vitu hivyo kupitia baadhi ya viongozi hao wa serikali.

Kifupi toka tulipopata uhuru hakuna awamu ambayo ilipita bila ufisadi na wizi wa fedha za serikali. Kasome historia za kina mzee Mtei wakati wapo serikalini pamoja na magava wengine waliofanyakazi chini ya serikali ya Nyerere.

Nyerere ni baba wa taifa, alijenga misingi bora ya umoja na mshikamano, alitokomeza ukabila, ukanda nk, lkn ndio raisi alieondoka madarakani akiiacha nchi ikiwa uchi kiuchumi, huku wananchi wakiwa maskini wa kutupwa, 90% ya wananchi wakiwa hawana uwezo hata wa kula milo miwili au mmoja kwa siku. Watu walichakaa wasijue wapi watapata angalau mafuta ya kula ya kupaka mwilini, watu walikauka midomo kwa kukosa maji, walikonda na hata kuumwa vidonda vya tumbo kwa kukosa chakula maana unakuta familia ya mume, mke na watoto 4 inapokea kilo 2 tu ya unga wa yanga kwa ajili ya ugali, kilo 2 ya mchele tena mdundiko, mafuta lita 1, sukari kilo 1 afu wanaambiwa watumie week nzima ndo gari kitapita tena.

Mwinyi alipoingia aliondoa mateso yote watu wakawa wanapata huduma inavyostahili, waandishi wa habari wakaruhusiwa kuandika chochote wanachojisikia kitu ambacho kwa Nyerere ilikuwa ngumu kwa muandishi kuandika kitu kibaya against government yani mwandishi unatakiwa uandike habari za kumsifu baba wa taifa na serikali yake tu. Na ndio maana wengi hamkujua ukweli kuhusu uozo uliyokuwa ndani ya serikali yake. Mwinyi aliruhusu kukosolewa na waliokosoa hawakuuwawa, hawakukimbia nchi, hawakuteswa, hawakufungwa wala kufukuzwa chama, ila kwa wale waliothubutu kumkosoa Nyerere wengi wao hatunao tena, wengine mpaka leo wapo nje ya nchi na uraia walibadilisha kitambo sana.

Nakuonea huruma kwa kulishwa matango pori tena ukute umelishwa na mtu wa kijijini asiejua lolote wala chochote.
 
Tanzania ya enzi za Nyerere ikiheshimika kila pembe ya dunia haipo tena. Tanzania hiyo ilikuwa na misimamo yake iliyojulikana na isiyotetereka.

Uhuru wa Tanzania hiyo haukuwa na maana yoyote bila Afrika yote kuwa huru. Uhuru wa Tanzania hiyo haukuwa na maana yoyote kama kulikuwa na ukiukwaji haki popote duniani Ukweli huo ulifahamika hivyo na kila rafiki na hata kila adui.

Kama taifa tulikuwa wamoja na nchi ilikuwa yetu sote. Nguvu ya hoja ilitamalaki na uthubutu wa kuhoji ulisisitizwa katika nyanja zote kutokea shule za misingi.

Leo baadhi ya watu kwa nafasi na ubinafsi wao wametumia nguvu kuuuwa uthubutu wa kuhoji. Yote hiyo ikiwa kwa nia ya kujimilikisha nchi wao na familia zao. Wasijue kuwa nchi wanaiuwa pia

Leo hatushindani kwa hoja. Hoja hazijibiwi kwa hoja, bali kejeli au kwa marungu. Watu wenye hoja tofauti wanatakiwa kuufyata. Tumelazimishwa kuwa taifa la makondoo.

Matokeo yake yamekuwa watu kulia lia yanapowakuta bila kuwa na uthubutu wa kuchukua hatua. Watu wamelazimika kuwa wenye kuangalia maslahi yao binafsi yanayowagusa wao moja kwa moja. Kwa maana jitihada za kuhoji lolote zimegeuzwa kuwa ni kujichumia majanga.

Uwezo wa kujenga, kutetea au kupinga hoja haupo tena. Utanzania wetu tuliojulikana nao umeparaganyika. Kila mtu imekuwa yupo yupo tu. Leo bila aibu tunajinasibu kama mashabiki wa Man U au Arsenal.

Ni muhimu kwa Kila mmoja kujihoji amefanya nini kuifikisha hii nchi hapa.

Anasema Prof Shivji:

“Pasipo mijadala au ubunifu huwezi kuendeleza fikra, na hii inakwenda moja kwa moja kuathiri usomaji na ufundishaji.”

Kwanini kuwaziba watu midomo? Kwanini hoja kupigwa marungu? Kwanini kuitana majina? Kwanini kujikita kupambana na mleta hoja badala ya kupambana na hoja? Nk, nk.

Kwanini JF hupiga wajumbe ban, kufuta au kufunga nyuzi bila kutoa sababu zikajulikana hadharani?

"Kwanini," huhitaji majibu si marungu.
Kipindi cha Nyerere ulikuwepo au unaadithiwa? Nani alikuwa na ubavu wa kumhoji au kumkosoa Nyerere?

Leo kutwa watu wanashinda mitandaoni kumtukana Rais alafu unasema hakuna uhuru? Kipindi cha Nyerere sio vyama vingi avikuwepo vilipigwa marufuku kabisa
 
Ni dhambi kubwa kumuweka independent thinker Ulimwengu katika kundi moja na JK.
TYL ilikuwa tawai la chama tawala, hakuna kulikiwa hakuna shida sana ulipofurukuta ukiwa huko ndani yake. Shughuli aliipata Ulimwengu alipojaribu ku challenge akiwa nje ya mfumo hadi akafanywa Mnyarundwa[emoji16].
TYL ya Nyerere ilikuwa na kina Ulimwengu na Kikwette. Uvccm Leo Ina kina johnthebaptist. Wengine humo ni kina nyie msioona hata umuhimu wa kuanza na: "kwa maoni yangu ...."

Nyie ni kutiririka tu kama vile mmetoka kuongea na Mungu.
 
Kipindi cha Nyerere ulikuwepo au unaadithiwa? Nani alikuwa na ubavu wa kumhoji au kumkosoa Nyerere?

Leo kutwa watu wanashinda mitandaoni kumtukana Rais alafu unasema hakuna uhuru? Kipindi cha Nyerere sio vyama vingi avikuwepo vilipigwa marufuku kabisa
Huyo kijana hakuwepo, haya yote alihadithiwa na watu ambao walikuwa na malengo yao juu ya uhadithiaji huu.
Na kwa vile kijana nae ni mtu wa upande ule uliojaa itikadi fulan basi akachukua vile vile kama alivyohadithiwa na kuja kuyaandika humu.

Mtu yeyote aliemjua vizuri Nyerere hawezi kuthubutu kuandika hivi alivyoandika kijana.
 
Back
Top Bottom