Limekaaje suala la madalali kulipwa kodi ya mwezi mmoja?

Limekaaje suala la madalali kulipwa kodi ya mwezi mmoja?

Chance ndoto

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2017
Posts
4,363
Reaction score
10,265
Habari za muda huu wakuu? Heri ya mwaka mpya pia.

Leo nimekuja kuuliza na kutafuta majibu ya juu ya suala la madalali wa nyumba kulipwa kodi ya nyumba ya mwezi.

Hili suala limekaaje hii ni baada ya kuona mijadala kadha wa kadha kupitia mitandao ya kijamii tofauti.

Je, kwanini kodi ya mwezi?

Inasimamia kitu gani?
 
- Na wenye nyumba wanavyopendana na madali sasa.

- Kuna nyumba ukienda hupewi chumba/nyumba mpaka uje na dalali.

- Mwenye nyumba unakuta kashaset anapangisha chumba 70000 dalali anakuja anamwambia mzee usitoe chumba hichi nakuletea kichwa cha laki moja, mwenye nyumba hapo ni full shangwe na kumwona dalali ndio mtu.
 
Hivi kodi ya mwezi mmoja anatoa mwenyewe nyumba pia? Au mwenye nyumba yeye hatoi?
 
Achana na udalali, kuna suala ya wenye nyumba kuchukua kodi kuanzia miezi mitatu, sita hadi mwaka. Wakati unakuta mshahara mtu analipwa on monthly basis, sasa unajiuliza kama nalipwa kwa mwezi mwezi ninapata wapi hela ya kulipa miezi sita?

Na serikali iko kimya kabisa
 
Dalali anakwambia ana nyumba ukimfuata anakwambia tumpitie mwenzangu,mkifika huko nako mnaambiwa mkampitie mwingine....nyumba ina msururu wa madalali wanne! Hapo lazima wapandishe Kodi ili ile hela ya mwezi iwakimu wote wanne.
 
Habari za muda huu wakuu? Heri ya mwaka mpya pia.

Leo nimekuja kuuliza na kutafuta majibu ya juu ya suala la madalali wa nyumba kulipwa kodi ya nyumba ya mwezi.

Hili suala limekaaje hii ni baada ya kuona mijadala kadha wa kadha kupitia mitandao ya kijamii tofauti.

Je, kwanini kodi ya mwezi?

Inasimamia kitu gani?
Bila yeye hicho chumba ungepata?
 
Habari za muda huu wakuu? Heri ya mwaka mpya pia.

Leo nimekuja kuuliza na kutafuta majibu ya juu ya suala la madalali wa nyumba kulipwa kodi ya nyumba ya mwezi.

Hili suala limekaaje hii ni baada ya kuona mijadala kadha wa kadha kupitia mitandao ya kijamii tofauti.

Je, kwanini kodi ya mwezi?

Inasimamia kitu gani?

Hawa madalali wangesajiriwa na serikali kwa maana ya kuwa identified kbs na nathani TRA sehemu inayo deal na property Tax hawa wanatakiwa wawe chini yao ama la wawe chini ya NHC kitengo cha real estate, muwakamue kodi msikimbilie kwenye maduka tu.
 
Back
Top Bottom