Akitokea mwekezaji akaanzisha mfumo mzuri wa kimtandao wa kupangisha nyumba, vyumba, warehouses nk.
Kuwe na vigezo vya kuwabaini wenye nyumba kama takwa la kujisajili.
Huu mfumo utatengenezwa kimaeneo, kwamba nikiwa singida na ninahitaji chumba arusha niwe na uwezo wa kuangalia nyumba ama vyumba vinavyopatikana katika wilaya, kata, na mitaa husika na occupancy status.
Mfumo uwe na database ya wateja wote, waliokwisha pangisha nyumba vyumba, na wale wakorofi, wenye kadhia mbalimbali wawe reported na kuwe na list ya wapangaji wakorofi wote wasiolipa na matukio mengine yasiyofaa, hii itawapa fursa wapangishaji kujua tabia ya mpangaji wake mpya kwasababu kutakuwa na records za nyumba zote alizopanga, na wenye nyumba lazima waache reviews za wapangaji wao pale wanapo hama. Unaweza kuhisi itakuwaje kama mwenye nyumba kamchafua mpangaji wake kwa maksudi ili asipokelewe sehemu zingine atakazo kwenda kuomba kupanga, jibu ni kesi yoyote ya mpangaji na mpangishaji lazima iwe reported na inapothibitika mwenye nia ovu ni mpangaji basi profile yake inaweza kuwekewa nyota ndogo kuonesha yeye ni mpangaji msumbufu au asielipa kwa wakati.
Hili project inaweza kusimamiwa na serikali na itapata makusanyo mengi sana ya kodi.
Hapa madalali (kamfukoo jitegemeee)