DOKEZO Limeshafika ghorofa ya 13 na linaendelea, lakini nguzo kama njiti za kiberiti

DOKEZO Limeshafika ghorofa ya 13 na linaendelea, lakini nguzo kama njiti za kiberiti

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Haya mambo hayafanywi kienyeji enyeji tu. Lazima mtu awe na permit na authorization kutoka kwa mamlaka husika; na engineer anakuwa ame approve michoro ya hilo jengo kuwa ujenzi huo ni salama. Kama hujui kitu unauliza ufahamishwe...

Mchana mwema!
Lile lililoanguka posta kwani halikuwa na michoro? Ilikuwepo ila shida ni pale jengo linapojengwa zaidi ya idadi iliyokuwa specified kwenye michoro
 
Unaweza ukawa na hoja lakini Strength haipimwi kwa unene Wa beam! ingefaa ukaweka structure ikoje ili tuichambue!

Note: Jengo linaweza kuwa na column/beam nyembamba lakini zikawa ni nyingi ili kufanya load distribution kuwa safe!.

Kwahiyo ipendeze sasa kuangalia structure kwanza kabla ya kulaumu
Wapi nimelaumu? Mimi nimetia angalizo ili wahusika wakajiridhishe tu, sidhani kamankuna tatizo hapo, maana wanalipwa mishahara kwa kazi hiyo anyway..
 
Umejuaje kama hiki alichokileta sio moja ya issue zake? Maybe hizi ndio kazi zake kwa hiyo usimjudge sana.

BTW kwa huo muonekano wa hizo nguzo ni kweli jengo linatia shaka uimara wake.

Cc Unforgetable
Unforgetable anaonekana sana kwenye comment zako mkuu nini kilicho nyuma ya pazia ama ni kama mahondaw na smart
 
Engineer Tetramelyz
Haya mambo hayafanywi kienyeji enyeji tu. Lazima mtu awe na permit na authorization kutoka kwa mamlaka husika; na engineer anakuwa ame approve michoro ya hilo jengo kuwa ujenzi huo ni salama. Kama hujui kitu unauliza ufahamishwe...

Mchana mwema!
 
Nikikuambia mimi ndie niliyelichora na niliweka ghorofa 10 tu na sikupewa taarifa ya amendment utasemaje? Hahahah..., sisemi hivyo ila nasema tu, what if.
Mkuu, weka wazi mambo, peleka kwa relevant bodies hiyo observation yako watayashughulikia professionally and legally, ukileta hayo mambo huku tutayashughulikia kienyeji kama nilivyofanya
 
Bwana mmoja anaitwa Raza alijenga ghorofa 2 pale indira ghandi street-CBD kwa kibali cha kujenga mwisho floor 9 na lingine 10. Yeye akajenga moja floor 15 na nyingine floor 16. Kilichotokea unakumbuka na nadhani hatosahau maisha yake yote yaliobaki.
Sidhani kama wanaweza kujenga jengo LA gharama kubwa kama hilo kwa wataalam wa kuokota jalalani
 
Sijajua ana mpango wa kutumia materials gani kwenye finishing,kama atatumia tofali kama ukuta kama ilivyoanza hapo ghorofa ya kwanza kwa jengo lote nitakuwa na mashaka,lakini kama atabadili kwa baadhi ya floors kwenda juu atatumia materials nyepesi sioni kama kutakuwa na tatizo...
 
Back
Top Bottom