DOKEZO Limeshafika ghorofa ya 13 na linaendelea, lakini nguzo kama njiti za kiberiti

DOKEZO Limeshafika ghorofa ya 13 na linaendelea, lakini nguzo kama njiti za kiberiti

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
kwa ninavyo jua mimi hawatofuatilia mpaka lije kudondokea watu kama kule nanihiii kwa wahindi
 
Kwenye structural engineering and design kuna mambo mengi ya kaungalia wakati wa kudesign ambayo ni kama ifuatavyo:

1. Kazi ya jengo husika ambayo hii ndiyo ina determine aina ya mzigo ambao slabs, beams na colums zitabeba. Maana mzigo husika ndio unaotumika kudesign size za colums, beams.

2. Material itakayotumika kwenye ujenzi. Mara nyingi maghorofa yanajengwa kwa kutumia zege (concrete) na steel (nende) lakini pia kuna baadhi ya maghorofa ambayo yanajengwa kwa kutumia steel columns and beams ambapo kwa Tanzania yapo machache kama lile la City Mall pembeni na DIT. Sasa size ya columns na beams zinaweza kuwa ndogo kulikana na uimara wa grade ya zege/ concrete iliyotumika pamoja na amount ya nondo/steel zilizotumika kutengeneza hizo colums au beams.

3. Weight distribution au mgawanyiko wa uzito wa mzigo kwenda kwenye beams na columns . Mara nyingi hii inakua determined na umbali uliopo kati ya beam moja na nyingine au column moja na nyingine. Umbali kati ya coumn moja na nyingine ukiwa mkubwa maana yake ni kwamba kila column itakua inabeba uzito mkubwa kuliko zile columns ambazo umbali kati ya moja na nyingine ni mdogo. Columns au beams kadri zinavyobebeshwa mzigo mkubwa ndivyo size yake inavyozidi kuwa kubwa na ndivyo grade ya zege pamoja na nondo size zinavyozidi kuwa kubwa.

Conclusion;
Siyo rahisi saana kupima na kujua kama jengo limekidhi viwango kwa kuangalia kwa macho hasa kwa kuweka picha kama alivyofanya mtoa mada unahitaji kujua combination ya vitu 3 nilivyotaja hapo juu.
 
Pumbavu, kamenitoka tu; Halafu watu wakifa ni ishu yetu sote kama nchi sio?
Tatizo hamjui haki zenu za kirai, unapolipa kodi sehemu ya hela yako inatakiwa itumike kuhakikisha kuna watu wanalipwa kulinda, mali, usalama na afya za wengine. Tusipende kujishughulisha na mambo yasiyotuhusu, wapo wataalamu wanalipwa kwaajili ya kukagua, kusimamia na kuridhia mambo ya ujenzi. Ni kweli zipo ajali na zipo namna za kushughulika nazo. Acheni umbea, msijishughulishe na mambo yasiyowahusu.
 
Picha hapo chini inajieleza, jengo lipo Kariakoo, limefika ghorofa kama 13 hivi na bado naona kuna nondo zimetokeza hapo juu kuashiria kwamba floor bado zinaendelea juu.

Sasa unaweza kuta michoro ya structural engineer imespecify mwisho ghorafa 10, lakini mwenye jengo anaamua tu kuongeza zaidi kwa tamaa ya pesa. Maana zile nguzo ni nyembamba sana na jengo lenyewe ni jembamba kama mlingoti.

Mamlaka zinazohusika zifanye ukaguzi ili lisije likaleta madhara na mwishowe tukapeperusha bendera nusu mlingoti.

View attachment 1193373
Unaweza kuwa sawa ila mimi niki zoom hiyo picha naona kuna nguzo nene fresh tu kwa ndani. Kwa macho naona kama kuna about 30cm x 30cm nguzo ndani.
 
Haya mambo hayafanywi kienyeji enyeji tu. Lazima mtu awe na permit na authorization kutoka kwa mamlaka husika; na engineer anakuwa ame approve michoro ya hilo jengo kuwa ujenzi huo ni salama. Kama hujui kitu unauliza ufahamishwe...

Mchana mwema!
Baati nzuri tupo humu tuliosimamia ujenzi pale kkoo kama Engineer...ujenzi wa matajiri wa pale ni wa ujanja ujanja...usikute hata sticker wanazotumia hapo ni feki na hata wakaguzi wakipita hapo wanapewa chao wanasepa bila hata kukagua ubora wa jengo....na inawezekana amepata kibali cha kujenga ghorofa zaidi ya 10 lakini structure desing standards za engineer na kinachofanyika ni tofauti...hivyo angalizo alilotoa mleta mada lisibezwe hata kidogo
 
Picha hapo chini inajieleza, jengo lipo Kariakoo, limefika ghorofa kama 13 hivi na bado naona kuna nondo zimetokeza hapo juu kuashiria kwamba floor bado zinaendelea juu.

Sasa unaweza kuta michoro ya structural engineer imespecify mwisho ghorafa 10, lakini mwenye jengo anaamua tu kuongeza zaidi kwa tamaa ya pesa. Maana zile nguzo ni nyembamba sana na jengo lenyewe ni jembamba kama mlingoti.

Mamlaka zinazohusika zifanye ukaguzi ili lisije likaleta madhara na mwishowe tukapeperusha bendera nusu mlingoti.

View attachment 1193373
Tunaishi kimungumungu weweee
 
Mleta mada hisia zako ziko sawa kiasi fulani, lakini nikujuze kwamba, beam ya ghorofa kwanza lazima iwe imeanzia chini kuanzia futi 6 kuendelea(inategemea na nature ya ardhi) nguzo kuwa nyemba hata kama ina uimara kiasi gani endapo itakuwa imechukua mzigo mzito lazima itacrack, beam inayosukwa huenda na nonda mm16 na ratio ya torori kwa mfuko na upana wa beam ni ft. 1½ hii huchukua ishirini na kuendelea, lakini kwenye hizo nguzo hutujajua zina upana kiasi gani maana hapo.
 
Umejuaje kama hiki alichokileta sio moja ya issue zake? Maybe hizi ndio kazi zake kwa hiyo usimjudge sana.

BTW kwa huo muonekano wa hizo nguzo ni kweli jengo linatia shaka uimara wake.

Cc Unforgetable
Nyie ndio huwa mnadanganywa na mafundi unakuta kavaranda ka hipped roof upana hakazidi hata mita 5 lakini watu wameweka nguzo 3 za uneno futi 3,huwa siwaelewi tumieni wataalamu
 
Mkuu, fanya issue zako, mambo ya watu achana nayo, unaweza ukawa na very limited facts kwenye hilo jambo
kinga ni bora kuliko tiba,acha afikishe maada kama ni sahihi ktk ujenzi huo au si sahihi..coz hatutaki kuomboleza na bendera nusu mlingoti
 
Back
Top Bottom