DOKEZO Limeshafika ghorofa ya 13 na linaendelea, lakini nguzo kama njiti za kiberiti

DOKEZO Limeshafika ghorofa ya 13 na linaendelea, lakini nguzo kama njiti za kiberiti

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Tatizo hamjui haki zenu za kirai, unapolipa kodi sehemu ya hela yako inatakiwa itumike kuhakikisha kuna watu wanalipwa kulinda, mali, usalama na afya za wengine. Tusipende kujishughulisha na mambo yasiyotuhusu, wapo wataalamu wanalipwa kwaajili ya kukagua, kusimamia na kuridhia mambo ya ujenzi. Ni kweli zipo ajali na zipo namna za kushughulika nazo. Acheni umbea, msijishughulishe na mambo yasiyowahusu.
Mkuu mie sijakuelewa, umechukizwa na jamaa kusema au nini kinatatiza hapo? Naona ni sahihi kabisa jamaa kutoa onyo, tunaona madudu mangapi kwenye miundombinu inapigwa tikitaka juu kwa juu yakitokea ya kutokea unakua msiba wa taifa. Komaa hapo hapo mtoa taarifa. Ujumbe utafika tu.
 
Mkuu, fanya issue zako, mambo ya watu achana nayo, unaweza ukawa na very limited facts kwenye hilo jambo
Mtoa mada kaandika point sana. Madhara aliyoeleza yaliwahi kutokea siku za nyuma na kumbukumbu bado zipo.
Yeye hajalalamika mtu kujenga mjengo wake isipokuwa namna lilivyojengwa ndiyo katia shaka.
Haya ya kusema afuate ishu zake na wakati mazingira anayoishi kuna sehemu panatia shaka ni ubinafsi uliopitiliza.
 
Mleta mada hisia zako ziko sawa kiasi fulani, lakini nikujuze kwamba, beam ya ghorofa kwanza lazima iwe imeanzia chini kuanzia futi 6 kuendelea(inategemea na nature ya ardhi) nguzo kuwa nyemba hata kama ina uimara kiasi gani endapo itakuwa imechukua mzigo mzito lazima itacrack, beam inayosukwa huenda na nonda mm16 na ratio ya torori kwa mfuko na upana wa beam ni ft. 1½ hii huchukua ishirini na kuendelea, lakini kwenye hizo nguzo hutujajua zina upana kiasi gani maana hapo.
Sawa, ngoja wahusika wakajiridhishe na hayo.
 
Mimi siko hapa kulaumu mtu au kusema huyu anamakosa, point is, ujenzi unatia shaka, wahusika wakajiridhishe.
Majengo yanapojengwa huwa kuna wahusika kutoka katika authorities wanapita kufanya ukaguzi ili kuhakikisha usalama kwa wafanyakazi na kile kinachofanyika site kinakubalika. Sidhani kama mpaka hilo jengo linafika hatua hiyo wahusika hawajafika kukagua
 
Majengo yanapojengwa huwa kuna wahusika kutoka katika authorities wanapita kufanya ukaguzi ili kuhakikisha usalama kwa wafanyakazi na kile kinachofanyika site kinakubalika. Sidhani kama mpaka hilo jengo linafika hatua hiyo wahusika hawajafika kukagua
Kwani kila anaekagua ni lazima.awe mwadilifu
 
Baati nzuri tupo humu tuliosimamia ujenzi pale kkoo kama Engineer...ujenzi wa matajiri wa pale ni wa ujanja ujanja...usikute hata sticker wanazotumia hapo ni feki na hata wakaguzi wakipita hapo wanapewa chao wanasepa bila hata kukagua ubora wa jengo....na inawezekana amepata kibali cha kujenga ghorofa zaidi ya 10 lakini structure desing standards za engineer na kinachofanyika ni tofauti...hivyo angalizo alilotoa mleta mada lisibezwe hata kidogo
Kwenye ujanja ujanja hapo sawa. Ila swala la kusema kuwa nguzo ni nyembamba so zinaweza kufail performance sidhani kama ni judgment nzuri.
 
Haya mambo hayafanywi kienyeji enyeji tu. Lazima mtu awe na permit na authorization kutoka kwa mamlaka husika; na engineer anakuwa ame approve michoro ya hilo jengo kuwa ujenzi huo ni salama. Kama hujui kitu unauliza ufahamishwe...

Mchana mwema!
Hayapaswi kufanywa kienyeji.., ila reality kuna developers sio waaminifu na wana-cut corners sio Africa tu hata UK England yaliwakuta kipindi kile jengo kuungua moto, halmashauri ilifanya uzembe wa kutumia materials zenye walakini...
 
Kwa muonekano wa hzo nguzo ilitakiwa mwisho wa ghorofa 7 tu [emoji41][emoji41][emoji41][emoji41][emoji41][emoji41][emoji41][emoji41][emoji41][emoji41][emoji41][emoji41][emoji41]
 
Sidhani kama wanaweza kujenga jengo LA gharama kubwa kama hilo kwa wataalam wa kuokota jalalani
Kuna jengo mitaa ya kati lilidondoka na kuua watu, lilikuwa limefika ghorofa 15, kifusi chake kilimwagwa Jangwani wakati wanalifukua. Ilikuja kugundulika baadae kuwa mmiliki alipewa kibali cha ghorofa 10.
Ukijiuliza kama naye alikuwa anawekeza pesa bila kujua madhara ndipo unajua kuwa ujinga wa Watz sio vijijini tu bali ni kuanzia wasiokuwa na pesa na wenye nazo, wasiokuwa na elimu na waliosoma, wenye madaraka na makapuku.
Dhambi mbaya kabisa na inayotumaliza ni pale unapoona kitu batili kinatokea alafu unakaa pembeni na kusema 'hayanihusu'.
Mkuu FRANCIS DA DON umefanya vizuri kuleta huu mjadala hapa ili kama kuna wenye hoja za kitaalamu waziweke na kuclear doubt, huwezi jua labda ni utaalamu wa kisasa.
 
Picha hapo chini inajieleza, jengo lipo Kariakoo, limefika ghorofa kama 13 hivi na bado naona kuna nondo zimetokeza hapo juu kuashiria kwamba floor bado zinaendelea juu.

Sasa unaweza kuta michoro ya structural engineer imespecify mwisho ghorafa 10, lakini mwenye jengo anaamua tu kuongeza zaidi kwa tamaa ya pesa. Maana zile nguzo ni nyembamba sana na jengo lenyewe ni jembamba kama mlingoti.

Mamlaka zinazohusika zifanye ukaguzi ili lisije likaleta madhara na mwishowe tukapeperusha bendera nusu mlingoti.

View attachment 1193373
Siwezi kubeza uzi wako,,


Ila cha kusikitisha likitokea la kutokea

Hao hao wanaopinga, wata delete hizo commentz zao

[emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom