Opuk Jater
Senior Member
- Dec 25, 2018
- 145
- 131
HILI NDILO JIBU LINALOTAKIWA....Kwenye structural engineering and design kuna mambo mengi ya kaungalia wakati wa kudesign ambayo ni kama ifuatavyo:
1. Kazi ya jengo husika ambayo hii ndiyo ina determine aina ya mzigo ambao slabs, beams na colums zitabeba. Maana mzigo husika ndio unaotumika kudesign size za colums, beams.
2. Material itakayotumika kwenye ujenzi. Mara nyingi maghorofa yanajengwa kwa kutumia zege (concrete) na steel (nende) lakini pia kuna baadhi ya maghorofa ambayo yanajengwa kwa kutumia steel columns and beams ambapo kwa Tanzania yapo machache kama lile la City Mall pembeni na DIT. Sasa size ya columns na beams zinaweza kuwa ndogo kulikana na uimara wa grade ya zege/ concrete iliyotumika pamoja na amount ya nondo/steel zilizotumika kutengeneza hizo colums au beams.
3. Weight distribution au mgawanyiko wa uzito wa mzigo kwenda kwenye beams na columns . Mara nyingi hii inakua determined na umbali uliopo kati ya beam moja na nyingine au column moja na nyingine. Umbali kati ya coumn moja na nyingine ukiwa mkubwa maana yake ni kwamba kila column itakua inabeba uzito mkubwa kuliko zile columns ambazo umbali kati ya moja na nyingine ni mdogo. Columns au beams kadri zinavyobebeshwa mzigo mkubwa ndivyo size yake inavyozidi kuwa kubwa na ndivyo grade ya zege pamoja na nondo size zinavyozidi kuwa kubwa.
Conclusion;
Siyo rahisi saana kupima na kujua kama jengo limekidhi viwango kwa kuangalia kwa macho hasa kwa kuweka picha kama alivyofanya mtoa mada unahitaji kujua combination ya vitu 3 nilivyotaja hapo juu.