Picha hapo chini inajieleza, jengo lipo Kariakoo, limefika ghorofa kama 13 hivi na bado naona kuna nondo zimetokeza hapo juu kuashiria kwamba floor bado zinaendelea juu.
Sasa unaweza kuta michoro ya structural engineer imespecify mwisho ghorafa 10, lakini mwenye jengo anaamua tu kuongeza zaidi kwa tamaa ya pesa. Maana zile nguzo ni nyembamba sana na jengo lenyewe ni jembamba kama mlingoti.
Pia wanasema jengo moja hadi jingine inabidi paachwe nafasi walau ya kupumulia, sasa hilo jengo ni kama linataka kugusa hili lingine, kwa ukaribu huu, hata moja moto ukiwaka lazima la pili lishike moto.
Mamlaka zinazohusika zifanye ukaguzi ili lisije likaleta madhara na mwishowe tukapeperusha bendera nusu mlingoti.
View attachment 1193373
Kwa ufupi ni kuwa nguzo/columns za jengo zinzaweza kubadilika urefu ila upana ukabaki vile vile floor zinazofuata.
Mfano:-
Ground -3rd floor (300x600)
3rd floor- 7th floor (300x450)
7th - 10th floor (300x300)
Usanifu wa majengo pia hutegemea aina ya matumizi ya jengo,hivyo mzigo utakaosafirishwa kupitia beams baadae columns/nguzo ni lazima ukidhi ubora wa zege,kiasi na aina ya nondo,size za beams na columns/nguzo.
Kwa ufupi ni kuwa kuonekana kwa wembemba wa nguzo upande wa mbele (cx view) hakumaanishi nguzo zile ni nyembamba,pengine ungelipiga picha ubavuni mwa jengo ili tuone kama upande wa (cy view) uko vile vile?.
Hata hivyo ukubwa wa nguzo hutegemea:-
1.uzito.
2.urefu wa floor to floor.
3.ukubwa wa balcony/cantilever (kuna wakati clients hawapendi beams zichomoze/zionekana nje ya jengo)
4.Aina ya/na ubora wa Nondo.
5.Matumizi ya Jengo (mfano: Parking, Ukumbi,Kanisa n.k)
Mbali na hivyo zipo aina mbili za majengo:-
1.Framed structures (non dead walls)
2.Load bearing structures (dead walls)
Hivyo usanifu wa 2. Hapo juu husaidia kuta kubeba mizigo directly kutoka kwenye beams,hivyo kupunguza mzigo kwenye columns/nguzo.
Yawezekana,lakini sina hakika kuwa Jengo hilo ni mojawapo ya Partial-framed/load bearing structure.
Cha kufanya/kukagua ni:-
Tabia ya udongo.
Matumizi ya Jengo.
Material inayotumika,hasa Nondo,kokoto, mchanga na tofari.
Ubora wa zege iliyokwisha fanyika awali.(rebound hammer/cube tests kama zipo).
Michoro hasa beams,columns,balcony details,foundations bases/raft.
Kiwango cha maji yanayotumika kumwagilia au ni aina gani ya umwagiliaji inatumika kushibisha zege.