Nigrastratatract nerve
JF-Expert Member
- Sep 4, 2019
- 1,524
- 4,477
LINAPOKUJA SWALA LA KUTISHIA MASLAHI NA USALAMA WA MAREKANI, HUWA HAIHITAJI KUOMBA USHAURI, KUZINGATIA HAKI ZA BINADAMU WALA KUTII SHERIA ZA KIMATAIFA:
Ukiitazama nchi ya Marekani katika taswira ya macho, unaweza kudhani kwamba, ni taifa la kidemokrasia linalofuata utawala wa sheria na kulinda haki za binadamu ikiwemo kuheshimu sheria za kimataifa, mipaka ya kiutawala ya nchi nyingine, lakini kiuhalisia wa mambo, Marekani ndilo taifa linaloongoza kwa kuvunja haki za binadamu duniani kuliko taifa jingine, ni taifa linaloongoza kwa kuvunja utawala wa sheria duniani, ni taifa linaloongoza kwa kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine pasipo kuheshimu uhuru wa nchi kujitawala na kujiamulia mambo yake, na pia ni taifa linaloongoza kwa kuzua migogoro au machafuko na vita vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi mbali mbali, hususani panapokuwa na rasilimali adimu inazozihitajika kujenga uchumi wake zilizoko katika nchi husika.
Kuna baadhi ya Wanasiasa wa upinzani na Wanaharakati wanaodhani serikali ya Tanzania inapochukua hatua kali za kisheria dhidi ya wale wanaotishia amani na usalama wa nchi kwamba, kwa kufanya hivyo inakandamiza haki za binadamu, inakandamiza demokrasia na kuminya uhuru wa watu kujieleza na kutoa maoni, lakini wanachosahau ni kwamba, kwa taifa la Marekani, inapotokea mtu au kikundi cha watu kutishia usalama na maslahi ya Marekani, haijalishi ni ndani ya mipaka ya Marekani au nje ya mipaka ya Marekani, mahali popote duniani, Marekani huwa haihitaji kuomba ushauri kwa mtu wala kuheshimu sheria za kimataifa, isipokuwa huchukua hatua kali inavyoona zinafaa kwa wakati huo kutegemeana na mazingira, wakati mwingine ikibidi hata kuua.
Katika kuthibitisha kwamba, maslahi na usalama wa Marekani mahali popote duniani ni kipaumbele cha kwanza kisichohitaji kuchezewa, hapo jana tarehe 03rd January, 2020 Rais wa Marekani Donald Trump aliamuru kuuawa kwa Jenerali wa Iran Qasseem Soleiman kupitia shambulio la ndege isiyokuwa na rubani (drone) eneo la uwanja wa ndege wa Baghdad nchini Iraq. Shambulio hili la jana ni majibu kufuatia wiki iliyopita waandamanaji kuvamia na kuushambulia Ubalozi wa Marekani nchini Iraq.
Huyu alikuwa Mkuu wa kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi nchini Iran. Anadaiwa kuwa mmoja wa watu makatili kuwahi kutokea katika eneo la ukanda wa Mashariki ya kati. Alikuwa akiaminiwa sana na kiongozi wa kidini wa Iran, kutokana na kupanga na kuratibu makundi mbali mbali ya kihalifu ikiwemo kuisaidia Syria katika vita vyake na Islamic State (IS) iliyoratibiwa na Marekani kutaka kuuangusha utawala wa Rais Assad. Kuuawa kwa Jenerali huyu licha ya kwamba ni pigo kubwa kwa Iran, pia kunaweza kuchochea vita kamili kati ya Marekani na Iran ambayo tayari imeapa kulipiza kisasi, huku Marekani ikipeleka askari zaidi na 3,500 na vifaa vya kijeshi ghuba ya Uajemi nchini Iraq.
Kupitia shambulio hili la Marekani lililomuua Jenerali wa Iran huko nchini Iraq, watanzania tuanze kujifunza na kutambua kwamba, usalama wa nchi ni kipaumbele cha kwanza. Hatuwezi kufanya siasa za kidemokrasia iwapo nchi haina usalama, hatuwezi kuwa na uhuru wa kujieleza na kutoa maoni ikiwa nchi haina usalama, wala hatuwezi kuzungumzia haki za binadamu endapo taifa halina usalama. Kwa msingi huo tutambuwe kwamba, hakuna kazi ngumu na nyeti kwa nchi kama kulinda na kudumisha usalama na amani.
Kazi ya kulinda na kudumisha usalama katika nchi, si swala la mchezo mchezo. Tunapoona na kushuhudia amani iliyopo katika nchi, tusidhani wala kufikiri kwamba ni kudra ya mwenyezi Mungu. Wapo maadui wa kila aina wanaopanga kuihujumu nchi yetu kila uchao, wakiwemo watanzania wenzetu wanaokubali kutumiwa na maadui, lakini wote hao wanashindwa kutokana na mifumo ya ulinzi na usalama wa nchi kuwa imara wakati wote. Katika hali ya kawaida huwezi kutarajia kuwaona maafisa wa kibalozi wa nchi za kigeni wakihudhuria mahakamani kwenye kesi anayoshitakiwa mtanzania mweusi kwenye nchi yake. Mkiona hivyo, basi mjuwe kisu kimekata mfupa. Wanafanya kila wawezalo kumnasua mtu wao waliyekuwa wakimtumia kwa mambo maovu ikiwemo kuhatarisha usalama wa nchi yetu. Kwa kuilinganisha Tanzania na Marekani, Tanzania ndiyo nchi yenye utawala wa kisheria ambayo mtu akivunja sheria, anafikishwa mbele ya sheria, tofauti na Marekani ambayo inajichukulia sheria mkononi kuvuka mipaka na kwenda kuua raia wa nchi nyingine, halafu wajinga na wapumbavu wanaipigia makofi na kuitolea mfano wa wa kuigwa. Tangu alipouawa Jenerali wa Iran huko Iraq, Wanasiasa na Wanaharakati wa Tanzania, wamenyamaza kimya, hakuna aliyenyanyua mdomo kulaani au kukemea kilichofanywa na Mareksni kwa Jenerali Qasseem Soleiman wa Iran.
Mwisho niiombe serikali, katika swala la kulinda na kusimamia usalama wa nchi, isilegeze kamba kwa mtu yeyote atakayetishia usalama wa nchi yetu kwa namna yoyote. Isiangalie umaarufu alionao wala nafasi yake kwenye jamii. Watu wa nchi nyingine wanakimbilia kwetu kwa sababu ya usalama na amani iliyopo. Endapo tukiivuruga nchi yetu, sisi tutakimbilia wapi? Atakayejaribu au kuthubutu kuvuruga amani na usslama wa nchi yetu, basi avurugwe yeye kwanza kabla nchi haijavurugika.