Linapokuja suala la kulinda maslahi ya nchi Marekani haina msamaha. Watanzania jifunzeni kwa Marekani

Hivi marekani wanapiga risasi Na kubambikiza kesi RAIA wao wanaowakosoa? Hapa yanalindwa zaidi maslahi ya ccm sio taifa.maslahi ya taifa Ni pamoja Na kuheshimu haki za RAIA wako ikiwemo Na wapinzani wako kisiasa.
 
Huzijui vizuri siasa za USA. Nakushauri kasome vizuri Realism theory ujue maana ya power politics na mambo ya real pilitik halafu urudi hapa tujadili
Mkuu unapotosha, kinachoendelea marekani kila MTU anakiona, hatujasikia wapinzani wakipigwa risasi kisa kumpinga trump.acha blahblah
 
Mkuu kuhusu waliokwenda kufanya fujo Ubalozi wa Afrika Kusini, vipi A. Kusini ikifanya kama Marekani?
Waliungwa mkono na serikali? Au umesahau kuwa ni Serikali yetu ndio iliyokwenda kuwatoa pale? Sasa hao SA watakuwa wana retaliate kwa nani?
 
Waliratibiwa na chama kilicho "sacrifice a lot"😂😂😂😂. Nauli na posho ya kuandamana walipewa.
 
Huku kwetu labda maslahi ya kutetea matumbo ya wanasiasa.
LINAPOKUJA SWALA LA KUTISHIA MASLAHI NA USALAMA WA MAREKANI, HUWA HAIHITAJI KUOMBA USHAURI, KUZINGATIA HAKI ZA BINADAMU WALA KUTII SHERIA ZA KIMATAIFA:

Ukiitazama nchi ya Marekani katika taswira ya macho, unaweza kudhani kwamba, ni taifa la kidemokrasia linalofuata utawala wa sheria na kulinda haki za binadamu ikiwemo kuheshimu sheria za kimataifa, mipaka ya kiutawala ya nchi nyingine, lakini kiuhalisia wa mambo, Marekani ndilo taifa linaloongoza kwa kuvunja haki za binadamu duniani kuliko taifa jingine, ni taifa linaloongoza kwa kuvunja utawala wa sheria duniani, ni taifa linaloongoza kwa kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine pasipo kuheshimu uhuru wa nchi kujitawala na kujiamulia mambo yake, na pia ni taifa linaloongoza kwa kuzua migogoro au machafuko na vita vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi mbali mbali, hususani panapokuwa na rasilimali adimu inazozihitajika kujenga uchumi wake zilizoko katika nchi husika.

Kuna baadhi ya Watanzania wapumbavu na wajinga wakiwemo Wanasiasa wa upinzani na Wanaharakati wanaodhani serikali ya Tanzania inapochukua hatua kali za kisheria dhidi ya wale wanaotishia amani na usalama wa nchi kwamba, kwa kufanya hivyo inakandamiza haki za binadamu, inakandamiza demokrasia na kuminya uhuru wa watu kujieleza na kutoa maoni, lakini wanachosahau ni kwamba, kwa taifa la Marekani, inapotokea mtu au kikundi cha watu kutishia usalama na maslahi ya Marekani, haijalishi ni ndani ya mipaka ya Marekani au nje ya mipaka ya Marekani, mahali popote duniani, Marekani huwa haihitaji kuomba ushauri kwa mtu wala kuheshimu sheria za kimataifa, isipokuwa huchukua hatua kali inavyoona zinafaa kwa wakati huo kutegemeana na mazingira, wakati mwingine ikibidi hata kuua.

Katika kuthibitisha kwamba, maslahi na usalama wa Marekani mahali popote duniani ni kipaumbele cha kwanza kisichohitaji kuchezewa, hapo jana tarehe 03rd January, 2020 Rais wa Marekani Donald Trump aliamuru kuuawa kwa Jenerali wa Iran Qasseem Soleiman kupitia shambulio la ndege isiyokuwa na rubani (drone) eneo la uwanja wa ndege wa Baghdad nchini Iraq. Shambulio hili la jana ni majibu kufuatia wiki iliyopita waandamanaji kuvamia na kuushambulia Ubalozi wa Marekani nchini Iraq.

Huyu alikuwa Mkuu wa kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi nchini Iran. Anadaiwa kuwa mmoja wa watu makatili kuwahi kutokea katika eneo la ukanda wa Mashariki ya kati. Alikuwa akiaminiwa sana na kiongozi wa kidini wa Iran, kutokana na kupanga na kuratibu makundi mbali mbali ya kihalifu ikiwemo kuisaidia Syria katika vita vyake na Islamic State (IS) iliyoratibiwa na Marekani kutaka kuuangusha utawala wa Rais Assad. Kuuawa kwa Jenerali huyu licha ya kwamba ni pigo kubwa kwa Iran, pia kunaweza kuchochea vita kamili kati ya Marekani na Iran ambayo tayari imeapa kulipiza kisasi, huku Marekani ikipeleka askari zaidi na 3,500 na vifaa vya kijeshi ghuba ya Uajemi nchini Iraq.

Kupitia shambulio hili la Marekani lililomuua Jenerali wa Iran huko nchini Iraq, watanzania tuanze kujifunza na kutambua kwamba, usalama wa nchi ni kipaumbele cha kwanza. Hatuwezi kufanya siasa za kidemokrasia iwapo nchi haina usalama, hatuwezi kuwa na uhuru wa kujieleza na kutoa maoni ikiwa nchi haina usalama, wala hatuwezi kuzungumzia haki za binadamu endapo taifa halina usalama. Kwa msingi huo tutambuwe kwamba, hakuna kazi ngumu na nyeti kwa nchi kama kulinda na kudumisha usalama na amani.

Kazi ya kulinda na kudumisha usalama katika nchi, si swala la mchezo mchezo. Tunapoona na kushuhudia amani iliyopo katika nchi, tusidhani wala kufikiri kwamba ni kudra ya mwenyezi Mungu. Wapo maadui wa kila aina wanaopanga kuihujumu nchi yetu kila uchao, wakiwemo watanzania wenzetu wanaokubali kutumiwa na maadui, lakini wote hao wanashindwa kutokana na mifumo ya ulinzi na usalama wa nchi kuwa imara wakati wote. Katika hali ya kawaida huwezi kutarajia kuwaona maafisa wa kibalozi wa nchi za kigeni wakihudhuria mahakamani kwenye kesi anayoshitakiwa mtanzania mweusi kwenye nchi yake. Mkiona hivyo, basi mjuwe kisu kimekata mfupa. Wanafanya kila wawezalo kumnasua mtu wao waliyekuwa wakimtumia kwa mambo maovu ikiwemo kuhatarisha usalama wa nchi yetu. Kwa kuilinganisha Tanzania na Marekani, Tanzania ndiyo nchi yenye utawala wa kisheria ambayo mtu akivunja sheria, anafikishwa mbele ya sheria, tofauti na Marekani ambayo inajichukulia sheria mkononi kuvuka mipaka na kwenda kuua raia wa nchi nyingine, halafu wajinga na wapumbavu wanaipigia makofi na kuitolea mfano wa wa kuigwa. Tangu alipouawa Jenerali wa Iran huko Iraq, Wanasiasa na Wanaharakati wa Tanzania, wamenyamaza kimya, hakuna aliyenyanyua mdomo kulaani au kukemea kilichofanywa na Mareksni kwa Jenerali Qasseem Soleiman wa Iran.

Mwisho niiombe serikali, katika swala la kulinda na kusimamia usalama wa nchi, isilegeze kamba kwa mtu yeyote atakayetishia usalama wa nchi yetu kwa namna yoyote. Isiangalie umaarufu alionao wala nafasi yake kwenye jamii. Watu wa nchi nyingine wanakimbilia kwetu kwa sababu ya usalama na amani iliyopo. Endapo tukiivuruga nchi yetu, sisi tutakimbilia wapi? Atakayejaribu au kuthubutu kuvuruga amani na usslama wa nchi yetu, basi avurugwe yeye kwanza kabla nchi haijavurugika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Marekani haiwauwi raia wake wanaokosoa Rais au utawala wa nchi.
Trump kapelekwa bunge la Congress na wamemuimperch lakini hajawafunga wala kupiga risasi kina Nance Peros na wabungr wa Congress.
Wako huru kisheria kumkosoa anatakiwa kujitetea.
The man is not above the law!!
Hiyo ni USA katiba inafanya kazi!!
The guy anajaribu kuleta justification za kipuuzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hoja haiendani na hali halisi. Kulinda maslahi ya nchi kunaanzia ndani.
Kwa mfumo wa USA mwaka wa kwanza wa utawala wa Magufuli angesha ondolewa madarakani na pengine kushtakiwa kabisa.
Tukiorodhesha hapa mambo ambayo yangesababisha kumuondoa tutajaza saver bure maana ni mengi mno!
Sisi hatuna maadui wa nchi, kwa lipi hasa? Tunao wahalifu wa makosa ya jinai ambao wanastahili kushtakiwa kwa mujibu wa sheria na kwa makosa yao halisi sio KUWABAMBIKIA makosa mengine yasiyo dhamana kuwakomoa.
Nchi ikifikia mahali pa kukomoa RAIA wake basi utawala huo haufai kabisa ni sawa na mchawi anayekula nyama wanawe.
Uzalendo ni kumtoa magufuli madarakani

Hapo ndo ntaamini TISS ni elites

La sivyo ni waganga njaa tu kama watu wengine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndiyo akili za baadhi ya nchi za Africa zinapoishia, zinajua adui wa maendeleo yako ni yule anakukusoa nchini mwako (eti hasa wapinzani). Wakati mpinzani wako anakupa challenge ya hapa kuna tatizo, kwa hiyo nilitatue kivipi,, Sasa kwa nchi zetu mtu yeyote anaye kukusoa ni kwamba hapa tunakosea, tunamuona kama adui wa nchi, maendeleo na adui wako...
Ndiyo vinatokea vitu kama kutekana, kesi kubambikiwa, kukamwatwa bila kusahau kushambulia kwa njia tofauti______bullet

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii dunia ipo hivi kutokana na akili za watu mbali mbali kuungana sasa wewe unapoleta story za kwamba akili yako pekee ndo kila kitu unawadharau wapinzani unakua mtu wa ajabu sana

Serikali nyingi za kiafrika ni za kifisadi wanafanya yote haya kulinda madudu yao huko ndani na uozo uchafu na matakataka mengine

Wanasahau in this world you can kill every thing but you cant kill an idea

Osama kauliwa kwani ugaidi umeisha terrorism is an idea

The same as opposition utamuua baba swalehe leo lakini hutoua upinzani

Upinzani utatoka milangoni mwako hawa watu wajue wanayoyafanya ni mambo mabaya mnooo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
LINAPOKUJA SWALA LA KUTISHIA MASLAHI NA USALAMA WA MAREKANI, HUWA HAIHITAJI KUOMBA USHAURI, KUZINGATIA HAKI ZA BINADAMU WALA KUTII SHERIA ZA KIMATAIFA:

Ukiitazama nchi ya Marekani katika taswira ya macho, unaweza kudhani kwamba, ni taifa la kidemokrasia linalofuata utawala wa sheria na kulinda haki za binadamu ikiwemo kuheshimu sheria za kimataifa, mipaka ya kiutawala ya nchi nyingine, lakini kiuhalisia wa mambo, Marekani ndilo taifa linaloongoza kwa kuvunja haki za binadamu duniani kuliko taifa jingine, ni taifa linaloongoza kwa kuvunja utawala wa sheria duniani, ni taifa linaloongoza kwa kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine pasipo kuheshimu uhuru wa nchi kujitawala na kujiamulia mambo yake, na pia ni taifa linaloongoza kwa kuzua migogoro au machafuko na vita vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi mbali mbali, hususani panapokuwa na rasilimali adimu inazozihitajika kujenga uchumi wake zilizoko katika nchi husika.

Kuna baadhi ya Watanzania wapumbavu na wajinga wakiwemo Wanasiasa wa upinzani na Wanaharakati wanaodhani serikali ya Tanzania inapochukua hatua kali za kisheria dhidi ya wale wanaotishia amani na usalama wa nchi kwamba, kwa kufanya hivyo inakandamiza haki za binadamu, inakandamiza demokrasia na kuminya uhuru wa watu kujieleza na kutoa maoni, lakini wanachosahau ni kwamba, kwa taifa la Marekani, inapotokea mtu au kikundi cha watu kutishia usalama na maslahi ya Marekani, haijalishi ni ndani ya mipaka ya Marekani au nje ya mipaka ya Marekani, mahali popote duniani, Marekani huwa haihitaji kuomba ushauri kwa mtu wala kuheshimu sheria za kimataifa, isipokuwa huchukua hatua kali inavyoona zinafaa kwa wakati huo kutegemeana na mazingira, wakati mwingine ikibidi hata kuua.

Katika kuthibitisha kwamba, maslahi na usalama wa Marekani mahali popote duniani ni kipaumbele cha kwanza kisichohitaji kuchezewa, hapo jana tarehe 03rd January, 2020 Rais wa Marekani Donald Trump aliamuru kuuawa kwa Jenerali wa Iran Qasseem Soleiman kupitia shambulio la ndege isiyokuwa na rubani (drone) eneo la uwanja wa ndege wa Baghdad nchini Iraq. Shambulio hili la jana ni majibu kufuatia wiki iliyopita waandamanaji kuvamia na kuushambulia Ubalozi wa Marekani nchini Iraq.

Huyu alikuwa Mkuu wa kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi nchini Iran. Anadaiwa kuwa mmoja wa watu makatili kuwahi kutokea katika eneo la ukanda wa Mashariki ya kati. Alikuwa akiaminiwa sana na kiongozi wa kidini wa Iran, kutokana na kupanga na kuratibu makundi mbali mbali ya kihalifu ikiwemo kuisaidia Syria katika vita vyake na Islamic State (IS) iliyoratibiwa na Marekani kutaka kuuangusha utawala wa Rais Assad. Kuuawa kwa Jenerali huyu licha ya kwamba ni pigo kubwa kwa Iran, pia kunaweza kuchochea vita kamili kati ya Marekani na Iran ambayo tayari imeapa kulipiza kisasi, huku Marekani ikipeleka askari zaidi na 3,500 na vifaa vya kijeshi ghuba ya Uajemi nchini Iraq.

Kupitia shambulio hili la Marekani lililomuua Jenerali wa Iran huko nchini Iraq, watanzania tuanze kujifunza na kutambua kwamba, usalama wa nchi ni kipaumbele cha kwanza. Hatuwezi kufanya siasa za kidemokrasia iwapo nchi haina usalama, hatuwezi kuwa na uhuru wa kujieleza na kutoa maoni ikiwa nchi haina usalama, wala hatuwezi kuzungumzia haki za binadamu endapo taifa halina usalama. Kwa msingi huo tutambuwe kwamba, hakuna kazi ngumu na nyeti kwa nchi kama kulinda na kudumisha usalama na amani.

Kazi ya kulinda na kudumisha usalama katika nchi, si swala la mchezo mchezo. Tunapoona na kushuhudia amani iliyopo katika nchi, tusidhani wala kufikiri kwamba ni kudra ya mwenyezi Mungu. Wapo maadui wa kila aina wanaopanga kuihujumu nchi yetu kila uchao, wakiwemo watanzania wenzetu wanaokubali kutumiwa na maadui, lakini wote hao wanashindwa kutokana na mifumo ya ulinzi na usalama wa nchi kuwa imara wakati wote. Katika hali ya kawaida huwezi kutarajia kuwaona maafisa wa kibalozi wa nchi za kigeni wakihudhuria mahakamani kwenye kesi anayoshitakiwa mtanzania mweusi kwenye nchi yake. Mkiona hivyo, basi mjuwe kisu kimekata mfupa. Wanafanya kila wawezalo kumnasua mtu wao waliyekuwa wakimtumia kwa mambo maovu ikiwemo kuhatarisha usalama wa nchi yetu. Kwa kuilinganisha Tanzania na Marekani, Tanzania ndiyo nchi yenye utawala wa kisheria ambayo mtu akivunja sheria, anafikishwa mbele ya sheria, tofauti na Marekani ambayo inajichukulia sheria mkononi kuvuka mipaka na kwenda kuua raia wa nchi nyingine, halafu wajinga na wapumbavu wanaipigia makofi na kuitolea mfano wa wa kuigwa. Tangu alipouawa Jenerali wa Iran huko Iraq, Wanasiasa na Wanaharakati wa Tanzania, wamenyamaza kimya, hakuna aliyenyanyua mdomo kulaani au kukemea kilichofanywa na Mareksni kwa Jenerali Qasseem Soleiman wa Iran.

Mwisho niiombe serikali, katika swala la kulinda na kusimamia usalama wa nchi, isilegeze kamba kwa mtu yeyote atakayetishia usalama wa nchi yetu kwa namna yoyote. Isiangalie umaarufu alionao wala nafasi yake kwenye jamii. Watu wa nchi nyingine wanakimbilia kwetu kwa sababu ya usalama na amani iliyopo. Endapo tukiivuruga nchi yetu, sisi tutakimbilia wapi? Atakayejaribu au kuthubutu kuvuruga amani na usslama wa nchi yetu, basi avurugwe yeye kwanza kabla nchi haijavurugika.
Unajua kuandika lakini hujui kutoa maoni .
Unazungumzia kiongozi wa kiislamu aliyeuawa na zaidi ukasema ni kiongoz katili kuwahi kutokea katika ukanda mwa mashariki ya mbali ...(na unaona alijaribu kufanya mauaji na kupanga mbinu za kuuwa wanajeshi wa marekani ) huyo mtu kwa ni asiuwawe kwa maslah ya nchi .

Hebu njoo hapa Tz akina nani unataka wauwawe kwa maslahi mapana ya nchi kwa kuwatarisha usalama ambao Rais anawatangaza ..Manake Marekani wanatangaza kabisa kuwa kundi flani ,mtu flani au taifa flani ni adui yetu ...Rais wetu alishawahi kuwatangaza wapi hao watu hadi tuseme hao n maadui namba moja kwa MASLAH mapana ya nchi..tofauti na kusema mabeberu na hajawahi kutaja hata nchi moja...
Mada yako umeileta bila kimihemko mno..unataka tuamini mtu yoyote anaempinga Rais wetu anahatarisha usalama wa nchi ..kwangu mimi Navyojua mtu anaehatarisha usalama wa nchi hawezi kupelekwa mahakamani ili akakae mahabusu .
 
Muulize snowden hata hvy hakuna mtanzania aliyetekwa au kuuliwa kisiasa sema mkikamatwa mnasema mmetekwa hafu kuuliwa raia yanayoua ni majambazi na si serikali pimbi wewe
Kwa marekani lile suala LA lissu kupigwa risasi vyombo vya dola vingewajibika.wenzetu hawakubali viongozi wao wadhuriwe wawe Wa upinzani au serikali.
 
Ushahidi wa hao watanzania wanaotumiwa na maadui zetu tafadhali.In case kama upo!
LINAPOKUJA SWALA LA KUTISHIA MASLAHI NA USALAMA WA MAREKANI, HUWA HAIHITAJI KUOMBA USHAURI, KUZINGATIA HAKI ZA BINADAMU WALA KUTII SHERIA ZA KIMATAIFA:

Ukiitazama nchi ya Marekani katika taswira ya macho, unaweza kudhani kwamba, ni taifa la kidemokrasia linalofuata utawala wa sheria na kulinda haki za binadamu ikiwemo kuheshimu sheria za kimataifa, mipaka ya kiutawala ya nchi nyingine, lakini kiuhalisia wa mambo, Marekani ndilo taifa linaloongoza kwa kuvunja haki za binadamu duniani kuliko taifa jingine, ni taifa linaloongoza kwa kuvunja utawala wa sheria duniani, ni taifa linaloongoza kwa kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine pasipo kuheshimu uhuru wa nchi kujitawala na kujiamulia mambo yake, na pia ni taifa linaloongoza kwa kuzua migogoro au machafuko na vita vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi mbali mbali, hususani panapokuwa na rasilimali adimu inazozihitajika kujenga uchumi wake zilizoko katika nchi husika.

Kuna baadhi ya Watanzania wapumbavu na wajinga wakiwemo Wanasiasa wa upinzani na Wanaharakati wanaodhani serikali ya Tanzania inapochukua hatua kali za kisheria dhidi ya wale wanaotishia amani na usalama wa nchi kwamba, kwa kufanya hivyo inakandamiza haki za binadamu, inakandamiza demokrasia na kuminya uhuru wa watu kujieleza na kutoa maoni, lakini wanachosahau ni kwamba, kwa taifa la Marekani, inapotokea mtu au kikundi cha watu kutishia usalama na maslahi ya Marekani, haijalishi ni ndani ya mipaka ya Marekani au nje ya mipaka ya Marekani, mahali popote duniani, Marekani huwa haihitaji kuomba ushauri kwa mtu wala kuheshimu sheria za kimataifa, isipokuwa huchukua hatua kali inavyoona zinafaa kwa wakati huo kutegemeana na mazingira, wakati mwingine ikibidi hata kuua.

Katika kuthibitisha kwamba, maslahi na usalama wa Marekani mahali popote duniani ni kipaumbele cha kwanza kisichohitaji kuchezewa, hapo jana tarehe 03rd January, 2020 Rais wa Marekani Donald Trump aliamuru kuuawa kwa Jenerali wa Iran Qasseem Soleiman kupitia shambulio la ndege isiyokuwa na rubani (drone) eneo la uwanja wa ndege wa Baghdad nchini Iraq. Shambulio hili la jana ni majibu kufuatia wiki iliyopita waandamanaji kuvamia na kuushambulia Ubalozi wa Marekani nchini Iraq.

Huyu alikuwa Mkuu wa kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi nchini Iran. Anadaiwa kuwa mmoja wa watu makatili kuwahi kutokea katika eneo la ukanda wa Mashariki ya kati. Alikuwa akiaminiwa sana na kiongozi wa kidini wa Iran, kutokana na kupanga na kuratibu makundi mbali mbali ya kihalifu ikiwemo kuisaidia Syria katika vita vyake na Islamic State (IS) iliyoratibiwa na Marekani kutaka kuuangusha utawala wa Rais Assad. Kuuawa kwa Jenerali huyu licha ya kwamba ni pigo kubwa kwa Iran, pia kunaweza kuchochea vita kamili kati ya Marekani na Iran ambayo tayari imeapa kulipiza kisasi, huku Marekani ikipeleka askari zaidi na 3,500 na vifaa vya kijeshi ghuba ya Uajemi nchini Iraq.

Kupitia shambulio hili la Marekani lililomuua Jenerali wa Iran huko nchini Iraq, watanzania tuanze kujifunza na kutambua kwamba, usalama wa nchi ni kipaumbele cha kwanza. Hatuwezi kufanya siasa za kidemokrasia iwapo nchi haina usalama, hatuwezi kuwa na uhuru wa kujieleza na kutoa maoni ikiwa nchi haina usalama, wala hatuwezi kuzungumzia haki za binadamu endapo taifa halina usalama. Kwa msingi huo tutambuwe kwamba, hakuna kazi ngumu na nyeti kwa nchi kama kulinda na kudumisha usalama na amani.

Kazi ya kulinda na kudumisha usalama katika nchi, si swala la mchezo mchezo. Tunapoona na kushuhudia amani iliyopo katika nchi, tusidhani wala kufikiri kwamba ni kudra ya mwenyezi Mungu. Wapo maadui wa kila aina wanaopanga kuihujumu nchi yetu kila uchao, wakiwemo watanzania wenzetu wanaokubali kutumiwa na maadui, lakini wote hao wanashindwa kutokana na mifumo ya ulinzi na usalama wa nchi kuwa imara wakati wote. Katika hali ya kawaida huwezi kutarajia kuwaona maafisa wa kibalozi wa nchi za kigeni wakihudhuria mahakamani kwenye kesi anayoshitakiwa mtanzania mweusi kwenye nchi yake. Mkiona hivyo, basi mjuwe kisu kimekata mfupa. Wanafanya kila wawezalo kumnasua mtu wao waliyekuwa wakimtumia kwa mambo maovu ikiwemo kuhatarisha usalama wa nchi yetu. Kwa kuilinganisha Tanzania na Marekani, Tanzania ndiyo nchi yenye utawala wa kisheria ambayo mtu akivunja sheria, anafikishwa mbele ya sheria, tofauti na Marekani ambayo inajichukulia sheria mkononi kuvuka mipaka na kwenda kuua raia wa nchi nyingine, halafu wajinga na wapumbavu wanaipigia makofi na kuitolea mfano wa wa kuigwa. Tangu alipouawa Jenerali wa Iran huko Iraq, Wanasiasa na Wanaharakati wa Tanzania, wamenyamaza kimya, hakuna aliyenyanyua mdomo kulaani au kukemea kilichofanywa na Mareksni kwa Jenerali Qasseem Soleiman wa Iran.

Mwisho niiombe serikali, katika swala la kulinda na kusimamia usalama wa nchi, isilegeze kamba kwa mtu yeyote atakayetishia usalama wa nchi yetu kwa namna yoyote. Isiangalie umaarufu alionao wala nafasi yake kwenye jamii. Watu wa nchi nyingine wanakimbilia kwetu kwa sababu ya usalama na amani iliyopo. Endapo tukiivuruga nchi yetu, sisi tutakimbilia wapi? Atakayejaribu au kuthubutu kuvuruga amani na usslama wa nchi yetu, basi avurugwe yeye kwanza kabla nchi haijavurugika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Matendo yanayoitwa ya kujilinda yanategemea kiwango cha fikra na ustaarabu wa wahusika.
Kuna ambao mawazo na nguvu zao zinaishia mtu na mtu, familia, kaya, kabila, taifa hadi kimataifa.
Maendeleo na kustaarabika kwa jamii hupanua fikra na wigo wa kuelekeza vitendo na nguvu za kujilinda.
Ulinzi una uhusiano wa moja kwa moja na kujihakikishia umiliki wa madaraka na mali (utajiri).
 
Wana siasa wa upinzani wana panga na kuratibu mauwaji ya nani humu Tanzania ukifananisha na huyo Generali Soleiman wa Iran? Pili mtu uliyemwita katili na kamanda anaye ratibu magenge dhidi ya maslahi ya Marekani huko mashariki ya Kati Marekani ilitakiwa iombe ridhaaa ya nani ili kumuangamiza? Roma mkatoriki ni tishio kwa amani? Ben Saa nane ni tishio kwa amani? Hao Wana siasa wa upinzani wanaopishana kisutu kila siku ndio waliomuuwa Akwilina? Mwisho nakukumbusha tu amani ni zao la HAKI.
 
mleta mada akili ndogo sana nakuonea huruma unakula buku 7 bure hapo lumumba wakutafutie kazi nyingine japo ya kufagia barabara za laki kariakoo.
 
Back
Top Bottom