Linda Lusingu: Muingereza mwenye asili ya Tanzania ashinda udiwani London

Fisiemu wanatamani wamrudishe wampe cheo!
manake wana tabia ya kupenda vitu vinavyong'aa
 
Umewaza kama mimi, huku viongozi husubiri mtu aliyefanikiwa kisha wachukulie pointi za mezani hapo. Nakumbuka kuna yule Mzanzibari aliyeshinda tuzo ya Nobel ya uandishi watu walivyohangaika kuona watadandia vipi ile nyota.
Kuna yule mchezaji kwenye kombe la dunia, mwenye asili ya Tanga, bungeni aliongelewa sana...
 
..Ni Mtanzania.

..Hata kwenye hotuba yake ya ushindi amemshukuru Mama.

..Pia amekitaja Chama cha Mapinduzi, kuwa ndicho kilichomlea.

Ok. My worry is we don't recognise dual citizenship. And those with it, fall victims
 
Wabongo kama wachina tu, wanapenda sana kusifiwa...huyo ni Muingereza period!

Yaleyale ya Obama watu kusema ana asili ya bongo kisa sijui bibi yake wa kifikia alitokea Rorya sijui wapi huko kwa Wajaluo wa TZ
Ninaifahamu hii familia, baba yao alikua Mchungaji wa Jehovah Witness na kanisa likimpeleka Uingereza miaka mingi. Mama wa hawa watoto ni Mganda na kwao Kiingereza ndiyo lugha rasmi.

Huyu dada amehitimu Oxford University.
 
Ok. My worry is we don't recognise dual citizenship. And those with it, fall victims

..Nilikuwa natania tu.

..Dual citizenship ni jambo ambalo linawaogopesha Watz.

..Nadhani serikali imeamua kutoa Special Status ambayo itawatambua Watz waliochukua uraia wa nchi nyingine.

..Binafsi napinga Dual citizenship, lakini naunga mkono Special Status.
 
Ni sababu ya Royal Tour; amshukuru rais samia kwa kutengeneza video hiyo.
 
Aisee mama anaendelea kuupiga mwingi, kazi iendelee
 
kumbe hata waingereza hawakuipenda lockdown! sisi watz tulipenda lockdown?
 
Tukipata mafanikio nchi za nje mnatuita Watanzania, tukiikosoa serikali yetu mnatuita vibaraka wa mabeberu. Tukitaka uraia pacha mnatuita wasaliti, tukipata nafasi za uongozi ughaibuni mnatuita Watanzania. Wanafiki nyinyi! Kwani hamjui Linda lusingu kapata nafasi hiyo tayari alishakuwa raia wa UK?[emoji847]
 
TUME ya UCHAGUZI ya kule inaonyesha ina Watu weledi sana ingekuwa hapa Mwingereza ndio kagombea asingepata kura hata ya mkewe
Sisi waafrika ni wabaguzi sana kuliko ubaguzi wenyewe,halafu tunakimbilia kulia wazungu ni wabaguzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…