Lindi: 13 wafariki katika ajali kati ya Coaster na Lori

Lindi: 13 wafariki katika ajali kati ya Coaster na Lori

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1713796407128.png

Watu 13 wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa kufuatia ajali ya basi dogo la abiria aina ya Toyota Hiace lililokuwa likitokea Somanga kuelekea Kilwa Mkoani Lindi kugongana uso kwa uso na lori la mafuta leo April 22,2024 katika Kijiji cha Somanga.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi, John Imori amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo katika barabara kuu ya Lindi - Kibiti ambapo amesema chanzo cha ajali ni Dereva wa lori kuhama upande wake na kuingia upande wa Hiace na kugongana uso kwa uso.

Majeruhi sita wanapatiwa matibabu katika Kituo cha Afya cha Tingi huku miili ya waliofariki ikihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi.

Kamanda Imori amesema Mashuhuda wamesema Dereva wa lori amelewa na walimuona akiwa anayumba na kumgonga Mwendesha baiskeli kabla ya ajali hyo ya gari, hivyo atafanyiwa vipimo na ikibainika alikunywa pombe kupita kiasi atachukuliwa hatua “Dereva wa lori na wa Hiace wote tumewakamata kwa mahojiano”
 

Watu 13 wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa kufuatia ajali ya basi dogo la abiria aina ya Toyota Hiace lililokuwa likitokea Somanga kuelekea Kilwa Mkoani Lindi kugongana uso kwa uso na lori la mafuta leo April 22,2024 katika Kijiji cha Somanga...
Ukichunguza kwa umakini Sana utagundua kwamba Kiini hasa cha mkasa huu ni uduni wa miundombinu ya barabara hapa Tanzania. Barabara ni nyembamba sana, 'lanes' za kupita magari hazijatenganishwa kwa matuta, kingo au magingi
 
Watu 13 wamefariki dunia na wengine wamejeruhiwa kufuatia ajali ya basi dogo la abiria aina ya Coaster iliyokuwa ikitokea Somanga kuelekea Kilwa Kivinje kugongana uso kwa uso na lori la mafuta.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi, John Imori amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akisema taratibu zingine za kubaini chanzo cha ajali zinaendelea.

20240422_184027.jpg
 
Sio kwa ubaya ila nauliza dereva wa hiace kaponaje hapo ilihali ilikuwa ni head to head collission? Naona hapo mwisho wanasema amekamatwa kwa ajili ya mahojiano. HOW?
 
Umeambiwa DEREVA wa Lori alikua chakari.
Umeelewa lakini mantiki ya point yangu ya kwenye comment hiyo uliyonukuu??
Hata kama dereva angekuwa kipofu, endapo kama barabara hiyo ingejengwa kwa kuzingatia hayo masuala niliyoeleza wala ajali hiyo isingeweza kutokea, ingezuilika.

Tuta, Ukingo au gingi kubwa kati kati ya barabara vingeweza kuzuia magari yanayopishana kuweza kukaribiana na kugongana uso kwa uso. Tuta au gingi lingekuwa kizuizi 'barrier' cha kulizuia gari la upande mmoja wa barabara kuvuka na kwenda kulivamia gari linalopita upande wa pili wa barabara hivyo kuzuia ajali kutokea.
 
Huko kuhama kwa hilo gari kubwa yawezekn kukwepa mashimo,

Hiyo barabara ni mbovu sana (mashimo makubwa yakutosba

R.I.P.


TUTENGENEZEEN NJIA YA KUSINI JAMAN
 
hivyo atafanyiwa vipimo na ikibainika alikunywa pombe kupita kiasi atachukuliwa hatua
Atafanyiwa vipimo pombe zikiwa zimekwisha kichwani ili kufuta ushahidi, ilitakiwa huyo kamanda aseme kipimo tayari maana wanakuwa navyo mfukoni
 
Back
Top Bottom