Lindi hadi Mbeya kwa barabara kuna umbali gani?

Lindi hadi Mbeya kwa barabara kuna umbali gani?

Hiyo njia ya kusini si ya makorongo matupu?
Hivi we ni wa nchi hii kweli? We kusini unakuchukuliaje, kwanini unafikiri barabara ya kusini iwe ya makorongo kwa hiyo kwa hiyo akili yako ndogo. Hiyo lami huko ulipo ilijengwa na wananchi? Acheni upumbavu kusini ni Tanzania serikali inapeleka maendeleo maeneo yote.. Kwanza ujue barabara ya kwanza ya lami ilijengwa kusini, yaani Trunk Road number one, T001 imeanzia Dar mpaka Tunduma. Barabara ya lami kutoka Makambako kupitia Njome mpaka Songea iljengwa enzi za Nyerere kabla hata lami haijafika hata Dodoma (T006). sasa hivi kuna lami tena nzuri ya kisasa. Kutoka Lindi-Masasi-Mtwara tangia kipindi cha Mkapa. Lindi-Masasi-Tunduru-Songea iko muda mrefu. Songea-Njombe-Makambako-Mbeya tangia kipindi cha baba wa Taifa.Kuna lami kutoka Songea-Mbinga-Mbamba Bay(ziwa Nyasa). Njombe-Makete

Huwezi amini kusini hata stand zao za wilaya ni za kisasa hazipo hata huko kwenu, kwa mfano wilaya ya Nanyumbu iliyoko mkoa wa Mtwara ina stand ya Kisasa eneo linaitwa Mangaka. Stand ya wilaya ya Tunduru ni ya kisasa ni wilaya chache sana ktk nchi hii inazo. Lami imefika mpaka wilaya ya Newala ambayo iko mkoa wa Mtwara, lami imefika Ruangwa ambayo iko mkoa wa Lindi.
Nyie endeleeni tu kukenua meno kama Ngedere na ujinga wenu wa kutojua nchi yenu. Katembee uijue nchi siyo unakaa nyuma ya keyboard unaandika kwa hisia tena kuwawazia wenzako mambo mabaya. Kusini mbona kuchele. Sema watu wa kusini wastaarabu sana hawana tabia za kujisifu km watu wa kanda za kaskazini(hasa wachaga) na kanda ya ziwa (hasa wasukuma). Watu wengine kweli mna upungufu wa akili, anayejenga barabara ni serikali halafu mtu anakuja hapa eti kwetu kuna lami, kuna sehemu nchi hii wanakijiji wameshawahi kuchangia kujenga lami? Serikali yetu inajenga miundo mbinu kwa uwiano mzuri.
 
Naomba kuuliza kwa mwenye kujua. Ukitoka Lindi Hadi Mbeya Kwa barabara. Umbali ukoje kulinganisha na Dar Hadi Mbeya.

Hali ya barabara pia ikoje?
Mzee Baba Jipange njia iko Vzuri sana nimetoka kupita hiyo njia Kuanzia Mbagala, Kibiti, Ikwiriri, unaingia Lindi Kijiji cha Mkwaya ukifika Mnazi Mmoja unaingia zako Kulia uelekeo wa Namungo FC na Mtama, Unaipita Masasi, Tunduru, Songea, Madaba, Makambako - unaingia uelekeo wa Mbeya.
Barabara ni Lami mwanzo mwisho. Lkn Mind You ile barabara ina Malori yanayosombelea Makaa ya Mawe kutoka Liganga kuelekea Bandari ya Mtwara yaani kila baada ya Km 3 au 5 mbele unapishana na Lori yaaani mengi mnooo. Barabara ya kutoka Songea kuja Makambako imechakaa, ni nyembamba na ina kona ukiwa kipande hicho mwambie dereva awe mtulivu. All in all utainjoy mandhari nzuri mnooo.
Kama unatumia Basi usilazimishe gari ya moja kwa moja. Chukua gari ya Dar -Songea via Lindi, then pale Songea Ingia La Charls kula maisha siku iishe. Siku ya pili panda gari Songea Mbeya kwa rahaaaa zoote unaingia Green City.
 
Kwahiyo Kwa urefu WA kilomita Mbeya to Dar ni fupi kulinganisha na Mbeya to Lindi??
kabisa tena zaidi ya mara 2, Dar-Lindi ni Km 470 tu. Ukitoka Dar Lindi unafika saa 6 mchana km umeanzia safari yako Mbagala au Temeke. sasa hata akili ya kawaida ukitoka Dar unapita mkoa moja tu wa Pwani mkoa unaofuata ni wa Lindi, umbali utoke wapi.
 
Hujaelewa kabisa sijataja Dar kabisa..
Nauliza Lindi to Mbeya sio Lindi to Dar
 
Sitaki kuja Dar ...nataka barabara za kusini kutoka Lindi Hadi Mbeya..
Sijawahi kupita hizo barabara za kusini mwisho wangu Dar Mtwara na ningeweza kugugo ila nimetumia makadirio tu.
 
Naomba kuuliza kwa mwenye kujua. Ukitoka Lindi Hadi Mbeya Kwa barabara. Umbali ukoje kulinganisha na Dar Hadi Mbeya.

Hali ya barabara pia ikoje?
1683277376603.png

15 hr 37 min (1,050.2 km) via Mtwara–Mbamba Bay Rd and B4
 
Hujaelewa kabisa sijataja Dar kabisa..
Nauliza Lindi to Mbeya sio Lindi to Dar
Ok sorry, Lindi-Mbeya ni Km 1068, nauli sh. 61,000/= Barabara ni nzuri ni lami ila kuna kona nyingi kutokea Tunduru-Namtumbo-Songea na kutoka Madaba(Songea)-Njombe. Ukitoka Njombe-Makambako-Wang'ing'ombe-Mbarali-Mbeya ni tambarare tu unaenjoy safari kutalii nchi yako.
 
View attachment 2610732

15 hr 37 min (1,050.2 km) via Mtwara–Mbamba Bay Rd and B4
we umejichanganya, Mtwara-Mbamba Bay ndiyo route gani hiyo. Mbona km umechanganya maharage na unga? Ukitoka Lindi unapitia njia zifuatazo: Lindi-Tunduru(Km337)-Songea(Km 265)-Njombe(Km 235)-Makambako(Km 60)-Mbeya(Km 185). Hii ndiyo route yenyewe
 
Naomba kuuliza kwa mwenye kujua. Ukitoka Lindi Hadi Mbeya Kwa barabara. Umbali ukoje kulinganisha na Dar Hadi Mbeya.

Hali ya barabara pia ikoje?
Umenikumbusha basi la Teeteeco enzi hizo Lindi/Mbeya na Lindi/Dar es Salaam.
 
we umejichanganya, Mtwara-Mbamba Bay ndiyo route gani hiyo. Mbona km umechanganya maharage na unga? Ukitoka Lindi unapitia njia zifuatazo: Lindi-Tunduru(Km337)-Songea(Km 265)-Njombe(Km 235)-Makambako(Km 60)-Mbeya(Km 185). Hii ndiyo route yenyewe
Kwani ramani inasemaje hapo, wewe unaona hiyo barabara imekwenda Mbambabay?
 
we umejichanganya, Mtwara-Mbamba Bay ndiyo route gani hiyo. Mbona km umechanganya maharage na unga? Ukitoka Lindi unapitia njia zifuatazo: Lindi-Tunduru(Km337)-Songea(Km 265)-Njombe(Km 235)-Makambako(Km 60)-Mbeya(Km 185). Hii ndiyo route yenyewe
Fafanua ueleweke
Lindi-Tunduru(Km337)-Songea(Km 265)-Njombe(Km 235)-Makambako(Km 60)-Mbeya(Km 185)
 
Fafanua ueleweke
Lindi-Tunduru(Km337)-Songea(Km 265)-Njombe(Km 235)-Makambako(Km 60)-Mbeya(Km 185)
Nieleweke nini, ni barabara ninayoifahamu vizuri napitia mara nyingi. Hizo ni KM yaani umbali kutoka mji moja kwenda mwingine km nilivyoonesha
 
Kwahiyo Kwa urefu WA kilomita Mbeya to Dar ni fupi kulinganisha na Mbeya to Lindi??
Unataka kusemaje??sasa safari ya mbeya dar,,,,na mbeya lindi kwa Akili yako ipi ni safari ndefu??
 
Unataka kusemaje??sasa safari ya mbeya dar,,,,na mbeya lindi kwa Akili yako ipi ni safari ndefu??
Kwa akili yangu?
Nimeanzisha thread kuuliza wanaojua..
Wapi umeona nimesema Kwa akili yangu?
 
Back
Top Bottom