LGE2024 Lindi: Msimamizi wa Uchaguzi kwenye Manispaa asisitiza wagombea kufanya kampeni za kistaarabu

LGE2024 Lindi: Msimamizi wa Uchaguzi kwenye Manispaa asisitiza wagombea kufanya kampeni za kistaarabu

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Mbona maelekezo yameanza kuwa mengi na hata kampeni hazijaanza?

Msimamizi wa uchaguzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, Juma Mnwele amevihimiza vyama vya siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 kuhakikisha kampeni zao zinafanyika kwa kistaarabu na kwa kufuata muda uliowekwa ambao ni Novemba 20 na kumalizika Novemba 26, 2024.
1731932000305.png

Akizungumza na Mashujaa FM, Mnwele alibainisha kuwa uchaguzi huo unajumuisha wagombea 3,115 wanaowania nafasi mbalimbali kutoka vyama saba vya siasa, ambavyo ni ACT Wazalendo, CCM, CUF, CHAUMA, CHADEMA, TLP, na NCCR-Mageuzi.

Pitia Pia: CHADEMA na ACT Wazalendo nendeni mahakamani mkausimamishe Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Mnwele amesisitiza umuhimu wa kufuata muongozo wa kampeni, akiwataka wagombea kujikita katika kunadi sera zao kwa hekima na kuepuka lugha za matusi au kampeni za kumvunjia heshima mtu binafsi.

Wananchi wa Manispaa ya Lindi, kwa upande wao, wameeleza matarajio yao ya kupata viongozi waadilifu, wenye maono ya kuwaunganisha, kusikiliza kero zao, na kuzitafutia suluhisho kwa maslahi ya jamii.
 
Back
Top Bottom