Mwanafunzi wa miaka 13 hawezi mlawiti mwanafunzi mwenzake mpaka akashindwa kutembea. Hii kesi ni ya kuchunguza naomba nitoe my personal experience on such a case.
Nilipokuwa darasa la pili nilisingiziwa kubaka mapacha tuliokuwa tukisoma pamoja na kukaa dawati moja.
Nilishangaa asubuhi nafika shuleni naitwa officini na kuanza kupigwa mboko. Nilikuwa mdogo siwezi jitetea wala kujieleza.
Hii kitu ilisinumbua sna mpaka namaliza darasa la saba zile siku za mwishoni sababu tuliendelea kuwa marafiki ilinibidi nimuulize mmoja wao nini kilitokea na kwanini walinisingizia.
Yule pacha mmoja alinieleza ukweli kuwa walifanywa ivyo na mwalimu wao wa tuition ambaye navyoandika hivi sasa ni mwalimu mkuu wa iyo shule leo hii. Walidai mwalimu aliwatisha sana so hawakuweza msema. Na wazazi wao alipowaleta kwa uyo mwalimu aliwaambia lazima itakuwa ni mimi ambaye huwa nao muda wote wanapokuwa shule.
Na huyu mwalimu ndye aliyenichapa sana mbele ya shule na wazazi wa wale mapacha.
Mpaka leo huwa najiuliza hata hawa wazazi hawakuweza kutafakari uwezzekano wa mtoto mmoja kubaka watu wawili?
So back to this case, mi nashaur uchunguzi ufanyike.