Polisi wa Wilaya ya Kilwa Mkoa wa Lindi wamemkamata Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo ndugu Zitto Kabwe Pamoja na baadhi ya viongozi wengine wakati wakiwa wanaendesha kikao cha ndani cha kukaribisha Madiwani wapya.
---
Kwa mujibu wa Chama cha ACT Wazalendo kupitia mtandao wa Twitter, Kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe na Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Sulemani Bungara (Bwege) wamekamatwa
Chama hicho kimeeleza kuwa Polisi wamewasili kwenye mkutano wao wa ndani Wilayani Kilwa ambapo shughuli za kuwapokea Madiwani 8 wa CUF zilikuwa zinaendelea
Aidha, kimebainisha kuwa kitatoa taarifa zaidi baadaye kwani sasa Viongozi wa chama hicho mkoni humo pamoja na Wanachama wanaelekea Kituoni
======
UPDATES:
LINDI: MKUU WA WILAYA AAMURU VIONGOZI 8 WA ACT-WAZALENDO WAKAMATWE, BWEGE AUGUA MAHABUSU
Mbunge wa Kilwa Kusini, Said Bungara (Bwege) amezidiwa ghafla akiwa mahabusu katika Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Kilwa na kukimbizwa Hospitali ya Kilwa Masoko kwa matibabu
Bwege, Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe na viongozi wengine6 wa ACT Wazalendo walikamatwa na Polisi leo asubuhi wakiwa katika mkutano wa ndani wa chama Wilayani Kilwa
Maelezo ya awali ya Polisi yamewataka Viongozi hao kuwa na Wadhamini 8, kila mdhamini atamdhamini Kiongozi mmoja ila kwa mujibu wa ACT, Viongozi wa Kituo kwa sasa wameondoka wakidai kuwa na kikao na Mkuu wa Wilaya
Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai amesema aliagiza Polisi wawakamate Viongozi kwa sababu wamefanya maandamano bila kibali na kulikuwa na fujo kwa umma ikiwemo milio ya honi
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai amesema aliagiza Polisi wawakamate Viongozi 8 ACT WAZALENDO akiwemo Kiongozi Mkuu Zitto Kabwe na Mbunge wa Kilwa Kusini Selemani Bungara (Bwege) kwa sababu wamefanya maandamano bila kibali. “kulikuwa na fujo kwa umma, milio ya honi nk”