mbinu za kibabe kuua upinzani zinavijenga zaidi vyama hivyo badala ya kuvibomoa, kila mtu nchini anasikia matukio hayo ya polisi kuwasumbua wapinzani na kuona wanaonewa na wananchi kuichukia serikali!
watu wa nje pia wanasikia na kuona video za matukio hayo na kuharibu taswira ya nchi na utoaji wao misaada na utalii, watalii wengi wa ulaya na marekani wanachukia nchi zenye ukandamizaji na pia matukio haya wapinzani wanayaandikia funding proposals na kupewa mabilioni kutoka nje kuja kuvuruga juhudi mfano hai ni tshirt alizogawa Zzk mji mzima Kilwa pesa hizo katoa wapi? aulizwe na Takukuru!
hapa ujanja ni kuwaruhusu wapinzani wafanye kwa amani vikao vya ndani na hata kwenye majukwaa ya siasa wasibugudhiwe sheria ya vyama vingi inawapa uhuru huo!
1. cha kufanya ni kuhakikisha wagombea wa ubunge wa upinzani hatari kwa kijani wanakosa form za ubunge kwa kukosa vigezo au wanapewa masharti kila wakileta form zirudishwe wakarekebishe vipengele hadi muda wa kurudisha form upite.
2. kesi za uchochezi ziwepo za kumwaga hata wagombea hatari wa upinzani wakose muda wa kampeni wawe wanashinda mahakamani, kesi zao zisiishe kosa moja wapewe kesi kumi na kila wiki wapewe tarehe kurudi mahakamani hadi uchaguzi upite na wengine wapewe kesi za kutakatisha pesa na uchochezi na uhaini na waambiwe sio raia!!
3.kutumia makada mitaani kuhamasisha watu kujiunga na kijani, tshirt na kofia na vitenge na vilemba vigaiwe kwa wingi hali ni ngumu wengine watumie nguo hizo kufanya mtoko! hii ni takrima muhimu! isipuuzwe wapinzani wameanza kuitumia na itawapaisha!
4. kuhakikisha miradi mingi ya maendeleo inakamilika kila mji au wilaya na kuondoa wakandarasi wazembe na kuwashitaki na kuwatupa jela maafisa wanaofisadi miradi.
5. Wakurugenzi kutumia magoli ya mkono kama last resort kwa majimbo yote tunayojua wabunge wake ni waropokaji na mawakala wa mabeberu!
6. kuendelea kupiga vichwa vya nyoka kule Dom, wakikaa hosp au mahabusu nchi inatulia miradi inaenda kwa kasi
7. kuunda kamati ya ufundi kuhakikisha wale wabunge hatari kumi hatari kwa kijani hawarudi bungeni!
hakuna haja ya mabomu ya machozi siasa ni akili tu, si mchezo unaohitaji hasira, Bia Yetu uko wapi? ushaamka na kuzimua? nakuwakilisha!