Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Kuna kufikiri ambako nakuona hakupo sawa ndani ya CCM, kuanzia raisi Samia kama mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, Spika wa Bunge, mawaziri, wakuu wa mikoa nk, yaani uongozi wote wa nchi ulio chini ya chama tawala cha CCM.
Hivi ni lini watarudiwa na akili na kutambua kwamba kuwa na upinzani imara wa kisiasa nchini ndio chachu itakayoleta kasi ya maendeleo ya nchi? Sio jambo la kujivunia pale ambapo unaona wazi upinzani nchini unakufa na hata unachangia na kufurahia kuudumaza! Ni ujinga wa kiwango cha juu kabisa. Ni uhaini kwa nchi.
Inasikitisha sana kwamba viongozi wa CCM karibu wote, isipokuwa wachache kama mbunge Mpina, ndio wanajitambua. Hivi ina maana wengine wote hawana uwezo wa kufikiri na kutambua kwamba ili nchi iendelee kwa kasi tunahitaji watu wenye kutoa mawazo tofauti au mbadala na kuyaweka mezani ili tupime wazo lipi linafaa na tuchague hilo?
Tanzania tunawezaje kuwa na akili ya kukataza monopoly katika biashara na kuweka sheria za kuzuia hilo ili kuchochea ushindani wa kibiashara kwa faida ya wananchi, lakini tukaona ni sawa kuwa na monopoly katika siasa na jambo nzuri kwa taifa?
Kwa jinsi alivyoanza, nilikuwa na matumaini kwamba angalau Raisi Samia ana uwezo wa wa kutambua kuwa monopoly ya kiasiasa ya CCM haitatupeleka popote katika azma yetu ya kutaka kuendelea kwa haraka, lakini sasa hata yeye naona kama ni wale wale wasio na uwezo wa kuliona hili katika mapana yanayostahili.
Na mbaya zaidi, kuna taasisi ambazo zinapaswa kulea chama tawala na wapinzani nchini, kama Polisi na TISS, nazo zimekumbwa na kirusi hiki cha kuona CCM inapaswa kuwa na monopoly ya kisiasa nchini! Na kila mtu anajua CCM wanafanya kila mbinu kukiambukiza kirusi hiki ndani ya JWTZ, kama ilivyofanyika nchini Zimbabwe.
Ningependa sana nikutane na Raisi Samia uso kwa uso, nimuulize hili swali, kwamba hivi hata wewe Raisi Samia unaona kwamba CCM kuwa na monopoly ya kisiasa nchini ndio kutatuletea maamuzi ya busara na ufanisi katika kuiletea Tanzania maendeleo ya kiuchumi na kijamii? Nimuulize aseme kama kweli anaona hili ni sawa na sio tatizo. Na kama akijibu ndio, basi itabidi nimpe pole yeye na watu wake ndani ya CCM anayoiongoza, na kusema wazi hamstahili kuongoza nchi hii.