A
Anonymous
Guest
Nianze kwa kupongeza JamiiForums kwa kazi nzuri mnayoifanya kwa kweli mnastahili pongezi kubwa.
Mimi nina ombi moja, ninaomba nisaidieni kuuliza swali kwa Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe pamoja na Wizara yake kuwa ni lini Serikali itakuwa na mpango wa kununua Mahindi kwa huu Mwaka wa 25/26?
Watanunua ni lini kwa maana ya kuanza kwa mchakato? Kama hawatanunua wanampango gani madhubuti wa kuhakikisha Mkulima anauza Mahindi kwa bei nzuri?
Maana mpaka sasa ni Julai 2025 tunaenda Mwezi wa Nane, Bunge limevunjwa, kikao cha mwisho cha Mawaziri kishafanyika, Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) - Tanzania nao wapo kimya, tunauliza kupitia page zao pia hawajibu, hivyo tumebaki njia panda.
Wangetupa mwongozo sisi tujue na kama hawatanunua watoe vibali kwa Wafanyabiashara.