A
Hata bila NFRA bei ya mtaani ni nzuri na kama una mahindi mengi vusha Nje ya NchiNianze kwa kupongeza JamiiForums kwa kazi nzuri mnayoifanya kwa kweli mnastahili pongezi kubwa.
Mimi nina ombi moja, ninaomba nisaidieni kuuliza swali kwa Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe pamoja na Wizara yake kuwa ni lini Serikali itakuwa na mpango wa kununua Mahindi kwa huu Mwaka wa 25/26?
Watanunua ni lini kwa maana ya kuanza kwa mchakato? Kama hawatanunua wanampango gani madhubuti wa kuhakikisha Mkulima anauza Mahindi kwa bei nzuri?
Maana mpaka sasa ni Julai 2025 tunaenda Mwezi wa Nane, Bunge limevunjwa, kikao cha mwisho cha Mawaziri kishafanyika, Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) - Tanzania nao wapo kimya, tunauliza kupitia page zao pia hawajibu, hivyo tumebaki njia panda.
Wangetupa mwongozo sisi tujue na kama hawatanunua watoe vibali kwa Wafanyabiashara.
Soko ndio linaamua ,kulalamikia Wakenya ni nonsense Kwa sababu wao wanajua Kwa kupeleka Kwa nini na nyie wakulima msifanye scouting ya soko?Asante saana kwa huu uzi mkuu.
It's so unfortunate- wanasiasa kama kawaida yao wanatanguliza maslahi yao ya kisiasa. Nani anakuwa nani na ujinga mwingi.
Sisi wakulima tumesahaulika. Kwa viongozi mliopo humu mnapaswa kuelewa jinsi mnavuopigania maslahi ya familia zenu kwenye huu uchaguzi ndivyo hivyo sisi wakulima tunapigania maslahi ya familia zetu pia.
Kwanini msiweke utaratibu mzuri wa bei za mazao! Serikali nyingi duniani mfanyabiashara/mjasiriamali/ mkulima mzawa anapewa kipaumbele kuliko mtu yeyote.
Watu tuna Tani kibao za maharage lakini tunazifungia ndani kwasababu ya bei isiyokuwa-controlled na serikali. Kwa taarifa yenu wakenya wamejazana wanayanunua maharage kwa bei ya kutupwa na athari mtaiona baada ya miezi michache.
Mtaanza kutafuta mchawi wa bei ya bidhaa za kilimo kupanda. Huwezi kuskia haya yakiongelewa kila mwanasiasa sasa hivi kinachoangaliwa ni namna ya kushinda na kulisha familia zao
Kamawakulima wenyewe hamjitambui na hamtaki kuunana kuwa voting power kwenye siasa nani akujali?
Nasikia zoezi la ununuzi limesha anza Ruvuma kwenye vituo vitano,baadhi ni Songea manispaa,Namtumbo,Mbinga,Soko ndio linaamua ,kulalamikia Wakenya ni nonsense Kwa sababu wao wanajua Kwa kupeleka Kwa nini na nyie wakulima msifanye scouting ya soko?
Mwisho wakulima wa India na Nchi zingine Huwa wakulima wanakiwasha Hadi Serikali inasarenda.
Ndio maana Mimi nilimsikia mwanasiasa hazunhumzii mambo ya wakulima kwangu huyo ni trash asiniletee habari za Katiba Mpya ambazo Hazina Msaada shambani.