Lionel Messi arejea timu ya taifa Argentina

Lionel Messi arejea timu ya taifa Argentina

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Mchezaji bora wa dunia wa soka,Lionel Messi ametangaza kurejea kwenye timu ya taifa ya Argentina. Messi ameandika kuwa timu ya taifa ya nchi yake ina matatizo mengi yanayopaswa kurekebishwa uwanjani.

Messi aka Andunje amewashukuru wananchi wote wa Argentina na wote waliomtaka arudi timu ya taifa. Messi amesisitiza kuwa anaipenda nchi yake. Atakuwa chini ya kocha mpya wa timu ya Taifa,Bauza. Here he is again!
 
Bora angekaa tu pembeni anarejesha gundu lake kwenye timu ya taifa
 
Namshangaa mtanzania mwenzangu anaesema "anajidhslilisha" hivi wananchi wako wakikuomba utumikie taifa lako unakuwa unajidhalilisha? Au ni ufinyu wa akili hadi mtu unasema hivyo na mtu anaposema ana "Gundu" hivi unamwitaje mtu anagundu anaefanya vizuri sokoni(kimapato),uwanjani na kupata tuzo kibao kuwa ana Gundu,au ni kutojua maana ya neno Gundu? Mwisho wa siku kila mchezaji ana maamuzi yake binafsi na akiombwa anauwezo wa kukubali ama kukataa pia.
 
Katika mambo nisiyoyapenda ni kwa Mtoto wa Kiume kutokuwa na msimamo... Sasa anataka kusema kwamba hapo awali alikurupuka au alikuwa anataka atest watu watajisikiaje akiacha soka kwenye timu yake ya taifa. Sipendi kutokuwa na msimamo kwa kweli.
 
King of failure!!! Nesi katika ubora wa hopeless!
 
kwani chochote utakaachoombwa lazima ukubali??? kombe ameshindwa kubeba FULLSTOP.
Alieweka huo utaratibu kwamb usipobeba kombe fullstop ni nan?au ni ww ambae hata danadana matatizo
 
hana jipya labda argentina ingekuwa barca angebeba kombe, lakini tofauti na barca hana kitu
 
Haters hawakupendezewa mfalme kurejea timu ya taifa, hahahaa kuna watu wa ajabu humu jf!!!!!

Acha niendelee kuzisoma post zenu zisizokua na maana yeyote..huo unaitwa "wivu wa kike" dume zima linaongea upuuzi.


Mleta post waabeja sana nkoi,
 
Good news, kustaafu kwake hakujamvunjia heshima, amerejea na heshima inaendelea kama kawa. Leo ni furaha iliyoje kwa mashabiki duniani!
 
Akiendelea kukosa makombe safari hii sijui atafanyaje tena. Maskini Messi wa watu. Na kizazi golden cha Argentina ndio kinapita hivyo. Afadhali ya mwenzake Ronaldo keshaondoa gundu tayari!
 
Huyu jamaa zimwi la Ronaldo linamsumbua sana.
Huyu jamaa zimwi la Ronaldo linamsumbua sana.

Kinachomuuma Messi ni kuwa ameona mwenzake Ronaldo amebeba taji LA Euro cup akiwa NA timu ya taifa ya Ureno wakati yeye hana taji lolote la maana akiwa na timu ya Argentina! Hilo ndilo limemlazimisha arudi timu ya taifa ili abahatishe kombe la dunia 2018! Angekubali tu kuwa R7 ni habari nyingine!
 
Matapishi hayalambwi!

Haka kakwepa kodi inabidi kalambe tu matapishi maana hakuna jinsi nyingine ya kujaribu kusafisha taswira mbele ya jamii! Si unajua kalishafungwa hata kama ni kifungo cha nje! kifungo ni kifungo bila kujali aina ya kifungo!
 
Back
Top Bottom