View attachment 1148981Tumeshuhudia Linel Messi kwa muda mrefu akisota na timu yake ya Taifa kuipa mafanikio tangu kombe la Dunia 2006 hadi mwaka jana 2018.
Tofauti na mafanikio makubwa aliyoiletea klabu yake ya Barcelona
Pamoja na kuwa na mastaa wengi, Argentina bado imeendelea kuwa kichwa cha mwenda wazimu kwa kuondolewa mapema kwenye mashindano muhimu kuanzia makombe yote ya Dunia Messi aliyoshiriki (ukiondoa ile ya Brazil ya mwaka 2014 ambako Argentina ilifika fainali), kwenye Copa America nk
Argentina inachokosa kikubwa ni uongozi
Kwenye uongozi kinachohitajika ni
- Inspiration - aweze kuwatia hamasa wenzake hata wakati wa hali ngumu
- Kujengewa wachezaji positive and winning mentality
- Communication - aweze kuwa medium/njia laini na rahisi ya mawasiliano- kusiwepo na gap ya mawasiliano yenye kusababisha mahusiano mabaya, magomvi na kutoaminiana kwenye timu
- Unification au kujenga timu kila mtu ajione ni sehemu ya timu na peke yake hakuna mafanikio
- Uzalendo - kwamba mafanikio ni lazima kwa ajili ya familia, marafiki, ndugu, nchi na awe tayari kujitoa mhanga kwa ajili ya hiyo
Hizo sifa zote Messi hana
- Messi is not a good communicator
- Ukimya wake unapitiliza na mara nyingi hana muda wa kuwatia ari na hamasa wenzake
TOFAUTI NAYE
Cristiano Ronaldo hizi sifa anazo na ndizo zilizomletea kupata mafanikio kwenye timu yake ya Taifa na wenzake wanampenda sana
Makosa makubwa timu nyingi za mpira zinafdanya ni kwa vile mchezaji ni mzuri uwanjani basi na wampee na unahodha wa timu wakati sifa za uongozi hana
Karibuni kama mna maoni, michango ijikite kwenye sifa za uongozi na sio uchezaji wa hao wawili