Lipi ni bora, kuwa muhuni yani nitoke nje ya ndoa au kuachana na huyu mwanamke?

Mbona

Mbona tulikubaliana humu kuwa mwanamke huwa hapewi nafasi ya pili?
Ndo nashangaa sasa mkuu, au kwenye kikao hakuwepo?

kuna jamaa mmoja ameshauri ukiona umeshindwa kabisa na unataka kumueka ndani single mom upime kwanza DNA ya maiti ya marehem mme wake pamoja na mtoto ...


Mana unaweza ukaambiwa baba amekufa kumbe anapumua mgodini huko....
 
Kwanza pole sana,. take easy, move on. kunguru hafugiki ujue hilo na uzur alshakwambia akirudia ufany chcht so uamuzi upo mikononi mwako mkuu.
 
Muhimu sasa hivi atulie na afanye mambo ambayo sahihi ambayo yatamletea amani ili aweze kusahau kwa haraka.

Kama anapenda kula nyama choma sana ahudhurie migahawa a- enjoy. Kama mpira anaangalia ndani aende kuangalia kwenye mabanda.

Kama mpenzi wa movie alipie kifurushi chake Netflix atizame movie maisha yaendelee.
 
Hoja nzito, Uzi ufungwe !!
 
Fanya hivyo tu, maana jela hapo ipo nje nje.
 
Barikiwa
 
Asante sana kiongozi
 
Ogopa sana mtu mwenye kisasi.
Mtu ambae anafanya kosa badala ya kukiri na kuomba msamaha yeye anasema mbona wewe ulifanya hiki na kile, kwanini hukuniambia au kuuliza...

Kua makini msije fikia hatua ya kufukiana na magunia ya mikaa.
Kama mmeshindwana achaneni kwa amani, watoto mtawalea tu, ni bora muwalee nyote wawili mkiwa hai mmetengana kuliko walelewe na watu baki mkiwa wafu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…