Lipi ni chaguo (Option) sahihi kuhusu ujenzi wa nyumba ya Ghorofa moja

Wanatisha watu tu. Ghorofa nyingi za kawaida ni 120-250m tu. Sasa huku mtaani watu wana nyumba za chini 50-70m zaidi ya tano utashindwa kujenga ghorofa ukiamua? Mimi binafsi sina mzuka na ghorofa ila mwenzangu humwambii kitu.
Ina maana Chawa Mwijaku katuongopea kuhusu gharama za ujenzi wa ghorofa lake, 1.3B??
 
Dadavua kidgo mkuuu. Tupe maarifa.
Katika ujenzi kuna kitu kinaitwa estimation yaani makadirio ya ujenzi haya. Yamegawanyika katika makundi mawili
1. Engineering estimate
2. Actual estimate.
Hii engineering estimate ni makadirio ya awali ya ujumla na yanakuwa kwa mfumo wa SQM pia kama hayo ya actual ila utofauti ni kuwa engineering estimate, inaweza kupungua au kuongezeka kidogo sana.

Kwa wastani mara nyingi hii huwa ni makadirio ya general kwahio unapima jengo lako lina SQM ngapi unazidisha alafu unazidisha na bei ya SQM moja ya soko in general ( hii hutumika hasa kwa wanaojenga gorofa kwa kutumia wakandarasi au wataalamu). Ambapo nafkir kwa sasa SQM moja Ina anzia kwny laki 5 mpk 6 na nusu ( hapa ni general mpk finishing).

Ukishapata hii engineering estimate mara nyingi inakuaga juu kidogo kwa actual estimate.( Hii inakusaidia kuandaa bajeti yako sahihi).
Ukishaamua kujenga na bajeti iko tiyar unamtafuta mtaalamu anakuandalia sasa actual estimate kulingana na uhalisia kwa kipindi na mahali husika.
 
Mkuu, msisitizo wako ni mzuri. Ila umeamua kutisha watu kwa kiasi chake. Laini 6 za nondo za 16mm hazina ulazima wowote kwenye ujenzi wa structural members za nyumba ya ghorofa 1.

NB: Beans โœ–๏ธ = Beams โœ”๏ธ
 
Though inategemea na ukubwa wa ghorofa lakini hii Urongo
Yes hapo kadanganya sana fikiria slab ya mita 6 kwa 7 hii nyumba simple tu room moja chini,sebule,dining,jiko,public toilet juu room 2 zote master na balcon haiwezi tumia M15 imezidi sana ni M10 ila hapa dah!
 
Ndugu yangu,mimi hii ni ndoto yangu kujenga ghorofa, nimefanya utafiti wa kina miaka kama 6 hivi nafanya utafiti. Kwanza elewa tunatishana sana kuhusu ghorofa.. ..
Ghorofa moja ya makazi kama hiyo ambayo unamanisha haina haja ya kuweka mawe na kumwaga zege(Germany concrete).. hii niliambiwa na mtaalamu kabisa na anajenga sana hizi ghorofa na nimefika site zake mara kadhaa, pili matumizi ya nondo wanadanganya sana,watu wengi hawaelewi, nondo zinazoweza kutumika zinaweza kuwa mm12, mm10, mm16 na mm 8, ila wengi utasikia lazima mm16 kwenye nguzo..uongo. Unaweza tumia mm12 ila kwenye kusuka wataweka nondo 6, ukitumia mm16 wataweka nondo 4, slab ni mm12 zinatumika, mm10 utatumia kama rings. Ila pia kuna muda wanaangalia na ardhi ikoje ndo watoe budget, kama eneo tambalale halina maji maji ardhi kama ya siyo mfinyanzi hapo unaweza jikaza tu, cha msingi kaa na mtaalam mpe wazo lako mchore ramani na makadirio yote. Siyo hivyo wanavyosema walimwengu japo pesa inatembea kidogo.
 
Bongo watu wengi waongo hasa aliyefanya Jambo flani
Kuna mtu humu alisema ghorofa bila mil 300 haiwezi kujenga. Sikutaka kuingia deep kumueleza ukweli maana tungeanza kubishana tu bila kujua kwa nini namkatalia
 
A
Asante sana Kiongozi! mpaka sasa mchoro wangu umeshapitishwa na Manispaa, sasa najilusanya kuanza hilo jambo.

Umenitia moyo sana kiongozi. Asante.
 
Shida inaanzia pale mtu anapotaka kujenga kitu chenye muonekano wa gharama kuuubwa lakini (here is thecatch) bila ya kutumia hiyo gharama kubwa๐Ÿค”.

Naamini inawezekana ila ni kwa gharama gani tujiulize.

Ukifuatilia comment utagundua hata sina nilijualo kuhusu ujenzi wa ghorofa, ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Gharama zinategemeana na eneo na aina ya mchoro pia, mfano anayejenga Morogoro,Tanga au Pwani ni tofauti na anayejenga Dar es salaam mfano, me nimejenga Pwani,mlandizi roli moja dogo la mawe yale yameandikwa M3 pembeni ni laki 3, wakati Dar itakuwa bei kubwa zaidi ya hiyo,, mchanga roli kama hilo ni elf 80,kokoto laki320, hata kifusi cha udongo elf 50. Tofali za inch 6 wanauza 1200 moja mpk site. Za inch 5 ni 900 mpaka site, so unaona tofauti hapo, cement na nondo kwa pwani na Dar ndo zinafanana bei..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ