Uchaguzi 2020 Lipumba: Mgombea Ubunge Temeke (CUF) alipata kura sifuri kwenye kituo ambacho yeye na familia yake walienda kupiga kura

Akizungumza na vyombo vya habari tofauti tofauti, akiwa anatoa msimamo wa chama chake kuhusu uchaguzi mkuu uliofanyika 28/10/2020 alisema wizi uliofanyika ni hatari zaidi ya korona.

Nanukuu
"Mgombea wa chama chetu jimbo la Temeke akiwa yeye na familia yake ya watu saba, kwenye kituo alichopigia kura na familia yake amepata kura sifuri, hawana aibu watu hawa ni hatari zaidi ya korona"

Aisee sijajua inawezekana vipi mgombea akose hata kura aliyojipigia mwenyewe [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

#Ukweli utabaki pale pale atakayesema uchaguzi huu ulikua huru na haki aende mirembe.

Video hii hapa chini
Your browser is not able to display this video.
 
Kuanzia sasa nakuita Pro. Lipumba mwanzo nilikuwa nakuona huna utofauti na wale wa Majalalani
 
Haha haha πŸ€“πŸ€“πŸ€“πŸ€“πŸ€“πŸ€“πŸ€£πŸ€£πŸ€£. Chezea chama kubwa wewe. Nyie si ndiyo kimbelembele? Tulikuwa tunawahadhaaa tu. Pole zako
 
Akae kwa kutulia, dawa imuingie..
 
Once a traitor ...... aendeleee kushangaa amevuna alichokipanda
 
Safi sana
 
πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ Itakuwa kura zao ziliharibika

Ila prof amevuna na yeye karai πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Huwezi sema kuna haki kama hujawahi kukutana na ukiukaji haki....

Hatimaye yamemkuta Lipumba huko
 
Mimi nikiingia Peponi nikakutana na Wa-CCM itanibidi nitoke tena nje niangalie mlangoni vizuri kumeandikwaje, isije ikawa nimejichanganya.
 
Anashangaa kura saba hazipo, akashangae uchaguzi Marekani ambapo kumepatikana kura za watu ambao walishafariki dunia.
 
Hahahaha kuiba nako kunahitaji akili sana na ujue mahesabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…