Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,734
- 5,750
Kwani kuwa mgombea ndio huwezi kufanya makosa?Yaani hata mgombea mwenyewe asijue jinsi ya kupiga kura?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani kuwa mgombea ndio huwezi kufanya makosa?Yaani hata mgombea mwenyewe asijue jinsi ya kupiga kura?
Lipumba alifanya makosa kufikiria kuwa shetani anaweza kufanya urafiki wa kudumu na baadhi ya watu.
Kazi kubwa ya shetani ni kukuangamiza. Anaweza kukupa vivutio, lakini ni lazima vitakuwa vivutio vya muda mfupi.
Sent using Jamii Forums mobile app
Maajabu ya uchaguzi yanaendelea, Lipumba akiwa anaongea na vyombo vya habari ameshangazwa na kitendo cha mgombea ubunge jimbo la Temeke kupitia chama anachokiongoza cha CUF, Zainab Mndolwa kuambulia kura sifuri kwenye kituo ambacho yeye na wana-familia saba walienda kupiga kura.
Lipumba amesema hiyo inamaanisha hata wizi ulivyofanyika hata aibu hawana kitu ambacho ni hatari na balaa kuliko Corona.
====
Idadi ya kura zilizotangazwa na Tume ya Uchaguzi kwa wagombea mbalimbali wa nafasi mbalimbali zina tofauti kubwa na uhalisia. Kwa mfano, mgombea ubunge wa jimbo la Temeke kwa tiketi ya CUF alipata kura sifuri (0) katika kituo ambacho yeye na wanafamilia yake ya watu 7 walipigia kura.
Aidha, ukichunguza matokeo ya uchaguzi kwa kuzingatia vyama utabaini kwamba matokeo yaliyotangazwa yalikuwa yameshapangwa, na hayatokani na yale ya wapiga kura. Mfano, rejea matokeo ya majimbo ya Dar es Salaam ya Mbagala, Temeke, Segerea na Ubungo. UBAKWAJI huu wa demokrasia ni kinyume na ibara ya 15 (1), ibara ya 16 (1) na ibara ya 17 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha UBAKWAJI huu unakwenda kinyume cha maazimio mbalimbali ya kimataifa ambayo Tanzania kama Nchi imeyaridhia ikiwa ni pamoja na Azimio la Jumiya ya Madola la Harare la mwaka 1991 na itifaki ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Afrika.
Hivi yule makamu wake kule Kaliua alishinda?Kwanzia sasa nakuita Pro.lipumba mwanzo nikikuwa nakuona huna utofauti na wale wa Majalalani
Anakiti kimoja cha kumshinda Hawa Ghasia huko Mtwara vijijiniHivi yule makamu wake kule kaliua alishinda?