Uchaguzi 2020 Lipumba: Mgombea Ubunge Temeke (CUF) alipata kura sifuri kwenye kituo ambacho yeye na familia yake walienda kupiga kura

Yeye na Mbatia wanavuna walichopanda.. Mrema alishajifia
Lipumba alifanya makosa kufikiria kuwa shetani anaweza kufanya urafiki wa kudumu na baadhi ya watu.

Kazi kubwa ya shetani ni kukuangamiza. Anaweza kukupa vivutio, lakini ni lazima vitakuwa vivutio vya muda mfupi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata NCCR wanalalama
Walisaliti upinzani Kwa kuahidiwa viti 20 bungeni sasa wamengundua shetani sio rafiki
 
Kura ni siri
Inawezekana kabisa hata mgombea mwenyewe hakujiamini akaona asipoteze kura ampigie Magufuli na CCM wenzake
 
Maajabu ya uchaguzi yanaendelea, Lipumba akiwa anaongea na vyombo vya habari ameshangazwa na kitendo cha mgombea ubunge jimbo la Temeke kupitia chama anachokiongoza cha CUF, Zainab Mndolwa kuambulia kura sifuri kwenye kituo ambacho yeye na wana-familia saba walienda kupiga kura.

Lipumba amesema hiyo inamaanisha hata wizi ulivyofanyika hata aibu hawana kitu ambacho ni hatari na balaa kuliko Corona.

====​

Idadi ya kura zilizotangazwa na Tume ya Uchaguzi kwa wagombea mbalimbali wa nafasi mbalimbali zina tofauti kubwa na uhalisia. Kwa mfano, mgombea ubunge wa jimbo la Temeke kwa tiketi ya CUF alipata kura sifuri (0) katika kituo ambacho yeye na wanafamilia yake ya watu 7 walipigia kura.

Aidha, ukichunguza matokeo ya uchaguzi kwa kuzingatia vyama utabaini kwamba matokeo yaliyotangazwa yalikuwa yameshapangwa, na hayatokani na yale ya wapiga kura. Mfano, rejea matokeo ya majimbo ya Dar es Salaam ya Mbagala, Temeke, Segerea na Ubungo. UBAKWAJI huu wa demokrasia ni kinyume na ibara ya 15 (1), ibara ya 16 (1) na ibara ya 17 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha UBAKWAJI huu unakwenda kinyume cha maazimio mbalimbali ya kimataifa ambayo Tanzania kama Nchi imeyaridhia ikiwa ni pamoja na Azimio la Jumiya ya Madola la Harare la mwaka 1991 na itifaki ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Afrika.

Ahahhh, maana yake hata ya mumewe alikosa, walahi CCM ni balaa
 
Si unaangalia upepo unavyovuma? Badala ya kuharibu kura, mtu na familia mnaamua kumpigia mpinzani wanu.
 
Maajabu ya uchaguzi yanaendelea, Lipumba akiwa anaongea na vyombo vya habari ameshangazwa na kitendo cha mgombea ubunge jimbo la Temeke kupitia chama anachokiongoza cha CUF, Zainab Mndolwa kuambulia kura sifuri kwenye kituo ambacho yeye na wana-familia saba walienda kupiga kura.

Lipumba amesema hiyo inamaanisha hata wizi ulivyofanyika hata aibu hawana kitu ambacho ni hatari na balaa kuliko Corona.

====​

Idadi ya kura zilizotangazwa na Tume ya Uchaguzi kwa wagombea mbalimbali wa nafasi mbalimbali zina tofauti kubwa na uhalisia. Kwa mfano, mgombea ubunge wa jimbo la Temeke kwa tiketi ya CUF alipata kura sifuri (0) katika kituo ambacho yeye na wanafamilia yake ya watu 7 walipigia kura.

Aidha, ukichunguza matokeo ya uchaguzi kwa kuzingatia vyama utabaini kwamba matokeo yaliyotangazwa yalikuwa yameshapangwa, na hayatokani na yale ya wapiga kura. Mfano, rejea matokeo ya majimbo ya Dar es Salaam ya Mbagala, Temeke, Segerea na Ubungo. UBAKWAJI huu wa demokrasia ni kinyume na ibara ya 15 (1), ibara ya 16 (1) na ibara ya 17 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha UBAKWAJI huu unakwenda kinyume cha maazimio mbalimbali ya kimataifa ambayo Tanzania kama Nchi imeyaridhia ikiwa ni pamoja na Azimio la Jumiya ya Madola la Harare la mwaka 1991 na itifaki ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Afrika.

Huyo mtu alikwenda kukipigia kura chama kingine na si chake, kwa hiyo Lipumba asilalamike.
 
Kura ni siri inawezekana mgombea alivutiwa na sera za mgombea mwingine akampigia kura.
 
Hakuna cha kushangaza hapo...

Hapo ina maana kura hazikuhesabiwa bali matokeo yalijazwa tuu...

Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom