Uchaguzi 2020 Lipumba, Shibuda kutumika kumdhibiti Lissu asigombee Urais?

Uchaguzi 2020 Lipumba, Shibuda kutumika kumdhibiti Lissu asigombee Urais?

Hivi idara ya usalama ni kwa ajili ya taifa au kwa ajili ya fissiem????
Naona idara nyeti zikitumika ndivyo sivyo, kama ndivyo basi hatuna budi kuopt option B, hatuwezi tukakaa tuone upuuzi kama huu ukifanywa na serikali, haina hadhi ya kutuongoza watanzania maana haina tofauti na majambazi!

Serikali inachopanda itavuna tu, hivi karibuni tutawaonyesha kuwa sisi sio wajinga wala wapumbavu!
 
Hata mimi, kama mpiga kura niliyejiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, nafikiria very seriously, KUMUWEKEA LISSU PINGAMIZI kwani kaanza kampeni mapema. Ninashauriana na Mawakili wangu na kuzipitia CLIP TULIZOKUSANYA wakati akiwa kwenye hiyo misafara yake ya "kutafuta wadhamini". Pia tunajaribu kuangalia kutoka kona nyingine ya KUTUMIA LUGHA YA MATUSI kwenye hiyo misafara yake. Ninataka nione huyo Amsterdam atakacho kuja kufanya kumsaidia huyu mteja wake.
Kazi kwako ndugu. Hiyo ni haki yako kikatiba
 
Tumesema humu mara nyingi sana kwamba hakuna kitu Bw. John Magufuli anakiogopa kama ushindani, atafanya kila linalowezekana asipate mshindani ktk siasa.

Ninahisi endapo mpango huo wa kijinga wa Magufuli utafanikiwa kwa kupitia kwa vibaraka wake akina Kaijage na Juma, basi watakaoumia sio Lissu bali ni watanzania wote.

Jumuiya ya nchi wahisani hawatakubali huu uhuni na uwezekano mkubwa ni utawala wake kuwekewa vikwazo rasmi baada tu ya huo 'uchaguzi'. Tusubiri tuone.
 
ukiona adui yako anafurahia au kukuacha ufanye jambo fulani ujue lina madhara kwako, polisi kumsindikiza lisu na kuruhusu mikusanyiko na kumuacha aihutubie wakati anatafuta wadhamini ni kielelezo tosha alianza kampeni kabla,
Jitahidini kutafuta usingizi kwa kujiliwaza.
 
CCM waachane kabisa na mambo ya Lissu; watayafukua mabaya mno kimataifa!!

Kumbukeni tumeingia mikataba mingi mno hasa ya haki za binadamu. Watu wanafikiri huwa haina nguvu!! Basi sawa kateni jina then mwekeni ndani kwa kosa la kuruka dhamana zake!!
 
Kupungua wapiga kura hiyo haina mjadala, lakini hiyo idadi imeongezwa makusudi ili kutoa matokeo yasiyo sahihi. Kitendo tu cha kuweka idadi isiyo sahihi, hiyo ni ishara kuwa hata matokeo yatakayotangazwa yatakuwa sio sahihi. Hapa ndio penye hoja yangu, maana tuna taasisi inayosimamia uchaguzi sio waaminifu.
Kuna umuhimu wa tume huru.Lakini hata vyombo vya usalama vinatakiwa kuwa neutral.
Nilishangaa juzi polisi anambembeleza kada wa CCM kuingia kwenye kalandinga,na huyo kada akipiga kelele kuwa yeye hatoki chama cha upinzani,kana kwamba kazi ya polisi ni kuwakamata wapinzani tu.
 
Huyo msaliti Lipumba, hiyo dhambi anayotaka kuifanya, atambue tu kuwa haitasamehewa milele na Taifa hili!

Hivi wewe Lipumba unayejiita ni kiongozi wa upinzani unawezaje kumwekea pingamizi kiongozi mwenzako wa upinzani, badala ya pingamizi hilo kuwekwa na mgombea wa CCM??

Hivi wewe Lipumba unadhani watanzania wameshasahau, jinsi ulivyomlazimisha kiongozi wa wazanzibari Seif Sharif Hamad, alazimike kukihama chama chako cha CUF, kutokana na mikakati miovu mliyopanga wewe na Jiwe wako??
Naona mnaweweseka
 
Msikilize aliyoko makanisani kwanza halafu urejee hapa
Hilo la kuendesha harambee kwa ajili ya kuwasaidia ndugu zetu Waislamu wa Chamwino kujenga nyumba ya kumuabudia Mungu, yaani Msikiti, wewe limekukera sana!? Kuna wakati nashindwa kuwaelewa wana JF, hivi unataka upendo gani Zaidi ya huu!?Au mnasema ni mbinu za kampeni? Mbona Rais alipomuomba Mwana Mfalme wa Morocco kuwajengea Msikiti waislamu pale Kinondoni hamkulisema hili, leo anachangisha pesa kwa nia kama hiyo hiyo, imekuwa nongwa! Ninyi vipi?
 
sasa cha kushangaza utasikia pingamizi limewekwa saa 10 jioni tarehe 25 /8 na wakati Lissu kapitishwa na tume usiku !
 
sasa cha kushangaza utasikia pingamizi limewekwa saa 10 jioni tarehe 25 /8 na wakati Lissu kapitishwa na tume usiku !
Zipo njama lukuki vikao kati ya jaji kaijage wa NECCCM na IGP Shibuda Lipumba na polepole haviishi week yote wanekuwa busy kupanga namna ya kumkomoa Tundu lisu, mda huu wajanja madalali wa siasa wanakula pesa nyingi tokea kwa mtukufu wakimdanganya kuwa watamsaidia kumhujumu Tundu lisu na kuidhoofisha chadema
 
Back
Top Bottom